Mawakili wataka kesi ya CHADEMA Arusha ufutwe

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
29 NOVEMBER 2011



Queen lema, na Pamella Mollel, Arusha

UPANDE wa utetezi katika kesi inayowakabili viongozi waandamizi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umewasilisha
pingamizi la kuitaka mahakama kufuta kesi hiyo kwa madai kuwa haoni utoshelezi wa kisheria ya mashitaka yanawakabili wateja wake.

Mawakili wa upande wa utetezi katika kesi hiyo Bw. Methody kimomogoro na Bw.Albert Sando, waliwasilisha pingamizi hiyo mahakamani hapo jana mbele ya hakimu Daudi Magesa.

Baada ya pingamizi hiyo kuwailishwa Hakimu Magesa aliahirisha kesi hiyo hadi December 20 atapotoa maamuzi kuhusu pingamizi hilo.

Bw. Kimomogoro alidai mahakamani hapo kuwa mashitaka yanayowakabili watuhumiwa ambao ni wateja wake hayana msingi kisheria kwa madai kuwa toka hapo awali walitoa taarifa kwa jeshi la polisi kwa masaa mengi zaidi kabla.

Wakili Kimomogoro aliendekea kudai mahakamani hapo kuwa kosa na shitaka la pili ambalo linawakabili wateja wake ambalo ni kufanya mkusanyiko ambalo ni la kukaidi amri halali ya polisi alidai kuwa nalo halina msingi kwa madai kuwa hati imeshindwa kutaja na kufafanua zaidi juu ya amri hiyo kutoka kwa jeshi la polisi.

Alidai kuwa makosa mengineyo nayo yanayowakabili wateja wake pia hayaioneshi na kufafanua zadi juu ya makosa ya nayowakabilikwa mujibu wa sheria jambo ambalo halina maslahi kwa mujibu wa sheria.



 
Huo ndio ukweli lakini magmba ni vilaza hawaoni huo uhalisia
 
Upande wa mashtaka waliomba mpaka jana J'tatu 28/nov kujibu hizo hoja,je ni majibu gani waliyatoa hiyo jana?
 
Yaaani magamba ni vilaza sana, wanajitahidi sana kupindisha ukweli lakini inashindikana.
 
Back
Top Bottom