Mawakili walalamikia washtakiwa wa ugaidi Zanzibar kushtakiwa Tanzania bara

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
DSC_0219-564x272.jpg

Mawakili wa Washtakiwa wa kitoka Mahkamani.

Mawakili wa watuhumiwa waliopo kizuizini kutokana na tuhuma za makosa ya ugaidi kutoka Zanzibar, wamedai kuwa kitendo cha Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwapeleka Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam ni kuidhalilisha Zanzibar kisheria.

Mawakili hao wakiongozwa na Abdallah Juma walitoa madai hayo mbele ya Jaji Mkusa Isack Sepetu wa Mahakama Kuu Zanzibar wakati wakiwasilisha hati ya maombi ya dharura kufuatia wateja wao waliokamatwa Zanzibar na kupelekwa Tanzania Bara kushtakiwa.

Alidai watu hao wamenyimwa uhuru wao wa kikatiba kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 14 (1) (2) na kifungu cha 16 (1).

Alidai kuwa kitendo kilichofanywa na Jeshi la Polisi cha kuwaweka kizuizini wateja wao kwa mienzi miwili sasa tena nje ya Zanzibar wakati Zanzibar ni nchi, ni kinyume cha sheria ya makosa ya jinai kifungu cha 28 sheria namba 7 ya mwaka 2004 ya Zanzibar.

“Zanzibar ni nchi tena ina mahakama yake kwa nini wateja wetu wakamatwe Zanzibar wakawekwe katika kizuizi kisicho halali Tanzania bara, hivyo jaji huoni kitendo hicho ni kuidhalilisha mahakama yako tukufu,” alidai Abdallah Juma.

Aliongeza kuwa wateja wao wanne walikamatwa na polisi Zanzibar miezi miwili iliyopita kwa kuhusishwa na tukio la mlipuko wa bomu uliotokea eneo la Darajani Juni 13, mwaka huu na kuua mtu mmoja na majeruhi tisa.

Alisema kwa mujibu wa sheria za Zanzibar tukio limefanyika Zanzibar, hivyo watu hao wangepaswa kuhukumiwa katika mahakama za Zanzibar na siyo Dar es Salaam.

Aliendelea kudai kuwa wateja wao hawajapewa fursa ya kusikilizwa na kuiomba mahakama hiyo kufuata sheria.

Hata hivyo, upande wa mashitaka uliiomba mahakama kutupilia mbali madai hayo na Jaji Sepetu aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 28, mwaka huu mahakama hiyo itakapotoa maamuzi kuhusiana na maombi hayo.

Watuhumiwa hao waliokamatwa miezi miwili iliyopita kutokana na kosa la ugaidi ni Nassor Hamad Abdallah, Mohammed Ishaq Yussuf, Said Kassim Ali, Hassan Bakari Suleiman, Rashid Ali Nyange, Antar Humoud, Khamis Salum Amour na Salum Ali Salum.
CHANZO: NIPASHE
 
...........Zanzibar koloni letu Tanganyika shida iko wapi? by the way mbona wapo Dodoma wanashiriki kikamilifu kutengeneza katiba ya Tanganyika? wajiongeze, otherwise.........!!!!!!!!
 
Sasa nani hapo koloni?kutunga katiba yako huwezi mpaka waje wazanzibar kukutungieni katiba huoni kuwa tanganyika ni shamba la bibi?hata dhahabu zenu wageni wanachimba kisha nyie mnaishia kupewa net za mbu,zinduka mtanganyika.
 
Hujakosea, Ndio maana zanzibar ya wazanzibari, na Tanganyika yetu Sote,nani koloni? 4
 
Hawa mawakili hawajui suala la ulinzi na usalama ni suala la muungano¤¤? Sasa hawajui makao makuu ya muungano ni wapi?
 
Sasa nani hapo koloni?kutunga katiba yako huwezi mpaka waje wazanzibar kukutungieni katiba huoni kuwa tanganyika ni shamba la bibi?hata dhahabu zenu wageni wanachimba kisha nyie mnaishia kupewa net za mbu,zinduka mtanganyika.
.........nani azinduke!!!! mimi ama wewe! ushawahi kuona ama kuskia tu Mtanganyika anashtakiwa Zanzibar? thubutu!!!!! tutaendelea kuvaa koti la Muungano mpaka mpate akili; hapa Dodoma mnafikiri mnatunga Katiba ya Tanzania, kumbe Tanganyika, ndo maana hata sura ya ardhi ambayo kimsingi haiwahusu sana tumeiingiza!!!!! Chuma kilikuwa Karume (baba), nyie wengine mdebwedo tu... Koti tutvaa sisi, kubanwa mtabanwa nyie "MAJANGA"
 
Hawa mawakili hawajui suala la ulinzi na usalama ni suala la muungano¤¤? Sasa hawajui makao makuu ya muungano ni wapi?
.......wanajua sana, katiba yao inasema mpaka baraza la wawakilishi likae, sasa limekaa lini kuruhusu mashtaka yaje Tanganyika? hapa katiba ya Zenji imevunjwa
 
Ni chuki tu inakusumbua nadhani kama wangekuwemo akina john usingethubutu kusema hivyo.

hata kama angekuwepo mjomba wangu.
we.hu hao jamaa; yani ww unawatetea kwasababu ni wenzako ktk.imani?
 
Mawakili wa watuhumiwa waliopo kizuizini kutokana na tuhuma za makosa ya ugaidi kutoka Zanzibar, wamedai kuwa kitendo cha Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwapeleka Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam ni kuidhalilisha Zanzibar kisheria.

Mawakili hao wakiongozwa na Abdallah Juma walitoa madai hayo mbele ya Jaji Mkusa Isack Sepetu wa Mahakama Kuu Zanzibar wakati wakiwasilisha hati ya maombi ya dharura kufuatia wateja wao waliokamatwa Zanzibar na kupelekwa Tanzania Bara kushtakiwa.

Alidai watu hao wamenyimwa uhuru wao wa kikatiba kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 14 (1) (2) na kifungu cha 16 (1).

Alidai kuwa kitendo kilichofanywa na Jeshi la Polisi cha kuwaweka kizuizini wateja wao kwa mienzi miwili sasa tena nje ya Zanzibar wakati Zanzibar ni nchi, ni kinyume cha sheria ya makosa ya jinai kifungu cha 28 sheria namba 7 ya mwaka 2004 ya Zanzibar.

“Zanzibar ni nchi tena ina mahakama yake kwa nini wateja wetu wakamatwe Zanzibar wakawekwe katika kizuizi kisicho halali Tanzania bara, hivyo jaji huoni kitendo hicho ni kuidhalilisha mahakama yako tukufu,” alidai Abdallah Juma.

Aliongeza kuwa wateja wao wanne walikamatwa na polisi Zanzibar miezi miwili iliyopita kwa kuhusishwa na tukio la mlipuko wa bomu uliotokea eneo la Darajani Juni 13, mwaka huu na kuua mtu mmoja na majeruhi tisa.

Alisema kwa mujibu wa sheria za Zanzibar tukio limefanyika Zanzibar, hivyo watu hao wangepaswa kuhukumiwa katika mahakama za Zanzibar na siyo Dar es Salaam.

Aliendelea kudai kuwa wateja wao hawajapewa fursa ya kusikilizwa na kuiomba mahakama hiyo kufuata sheria.

Hata hivyo, upande wa mashitaka uliiomba mahakama kutupilia mbali madai hayo na Jaji Sepetu aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 28, mwaka huu mahakama hiyo itakapotoa maamuzi kuhusiana na maombi hayo.

Watuhumiwa hao waliokamatwa miezi miwili iliyopita kutokana na kosa la ugaidi ni Nassor Hamad Abdallah, Mohammed Ishaq Yussuf, Said Kassim Ali, Hassan Bakari Suleiman, Rashid Ali Nyange, Antar Humoud, Khamis Salum Amour na Salum Ali Salum.

Na Rahma Suleiman
 
Ukiwaambia huu muungano ni utata mtupu hwatakuelewa. Zanzibar ni nchi kwa nini watu wake wakamatwe Zanzibar kwa makosa waliofanya Zanzibar halafu wawekwe kizuizini ana kufunguliwa kesi Tanganyika, nchi nyingine kabisa!
 
Akina seif Ali Iddi wanatoka sura mbaya tu, sasa hii ndio nini yaani udhalilishaji unafanyika wakati huu Katiba ipo kwenye mchakato ata ccm hawagundui chochote basi hata hili hawajaliona
 
Tatizo wazanzibar wana CCM wanaogopa sana uhuru wa nchi yao. wanataka watanganyika tuendelee kuwatawala.(slave mentalty)
 
Back
Top Bottom