Mawakili Mwanza njaa kali

Kweli ni njaa sana hao tena wana tabia ya kupokea hata rushwa

Kuna dada mmoja jengo la ccm, kama akikuwakilisha mahakamani lazima atoe papuchi, cha msingi ukienda ofisini kwake wekundu wekundu wasicheze mbali,jamaa yangu mmoja alikula mpaka akatosha
 

Jk huwa ana utaratibu wa kuteua majaji kutoka kwa watu wanaofanya uwakili wa kujitegemea,sijawahi kusikia hata mmoja kutoka mwanza
 
... Hata Dar napo njaa kali


UnaishI Gongo la mboto. Unaamka saa 11 alfajiri. Unapambana na foleni. Kesi (ya mteja wako) iko High Court. Imepangwa kusikilizwa saa 3 asbh. Unafika nusu saa kabla. Unapiga soga na mawakili "wasomi" kwenye corridor, huku kesi zikiendelea kuitwa....

.... saa 4. Kesi (ya mteja wako) bado haijaitwa. Unaendelea na soga, malumbano na majuzano ya sheria na kesi....

.... saa 5 asubuhi. Wenye kesi za madai kwa Mheshimiwa Jaji Kanyabayonga waende kwa msajili chumba nambari 65 kuahirisha kesi. Jaji Kanyabayonga yuko safarini. Amepata safari ya ghafla. Kesi (ya mteja wako) inaahirishwa kwa siku 14 mbele...

.... saa 6 mchana. Hukunywa hata chai. Unaanza safari ya kurejea ofisini kwako, mbali kidogo na katikati ya jiji. Safari inaanza...

.... mteja wako alikulipa tshs. 50, 000/= (fukara tu, hata kesi yake ni dhidi ya benki inayotaka kupiga mnada nyumba anayoishi baada ya kushindwa marejesho ya mkopo) apate uwakilishi. Huruhusiwi kumkataa eti kwa kuwa hana pesa. Cab rank rule. Justice for all...

Hapo unapitia HELSB wanakwambia ulipata mkopo asilimia 100 kwahiyo unadaiwa milion 28 kwa miaka minne.

Ukigeuka law school wanakudai milioni 8, za mkopo.


.... Mawazo tele kichwani. Unafika mataa ya Selander bridge unavuka na taa ya njano ukiwahi ofisini. Afande anakusimamisha kwa shangwe na furaha kuu. Anakulima makosa 2: i. kutoheshimu alama halali (na taa) za barabarani, NA ii. kuzuia watumiaji wengine wa barabara. Unapigwa faini ya tshs. 60, 000/=. Huna hiyo pesa. Unaandikiwa "kifurushi cha wiki." na unapewa risiti ya kielektroniki. Ulipe ndani ya siku 7. Jua kali sana, unamwomba afande akusamehe lakini kumbe alishaingiza nambari ya gari na leseni yako kwenye kile kimashine kabla hata ya kuongea na wewe...

... unaondoka. Unawaza sana. Una njaa. Huna pesa. Ada kubwa za TLS zakusubiri. TRA, Manispaa, landlord wa ofisi na nyumba unayoishi nao pia. Wakili msomi.

Lakini umevaa suti. Na unaijua vyema sheria. Na unaamini kesho itakuwa afadhali ya jana na leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…