Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 440
- 3,211
Wakili Mpoki aliongozana na mawakili wake ambao ni Raisi wa TLS Boniface Mwabukusi, Dkt. Rugemeleza Nshala, Paul Kisabo kutoka THRDC na Fredrick Msaki. Baada ya kufika kituo cha Polisi Mbweni, Mkuu wa Upelelezi alieleza kuwa Wakili Mpoki anahitajika katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa Kamanda wa Upelelezi wa Kanda ya Dar es Salaam.
Hivyo, tuliondoka na kuelekea Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam. Baada ya kufika na kuonana na Kamanda wa Upelelezi wa Kanda ya Dar es Salaam, alishukuru kuwaona Wakili Mwabukusi na Wakili Mpoki kwani wote walikuwa wanahitajika kwakuwa alikuwa na taarifa za Mpoki na Mwabukusi kuhusika katika kuhamasisha maandamano ya Disemba 09, 2025 kwa lengo la kuvunja Muungano, hivyo alitaka kupata ufafanuzi kuhusu taarifa hizo ambapo baada ya mazungumzo ya kina na ufafanuzi Kamanda wa Upelelezi wa Kanda ya Dar es Salaam aliwaruhusu kuondoka bila masharti yoyote.