Mawakala wa ajira ni wanyonyaji wa wafanyakazi

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,461
23,735
Serikali inabidi isimamie haya makampuni yanayohusika na uwakala wa ajira. Yamekuwa ni makampuni yanayoendesha unyonyaji kwa kiasi kikubwa sana. Mengi ya Makampuni hayo ambayo yanamilikiwa na wageni yamefikia hata hatua ya kukataa kuwapa haki za msingi wafanyakazi. Mfano wa Kampuni ya NFT ambayo imekuwa na unyonyanji mkubwa sana kwa wafanyakazi walioajiliwa chini ya kampuni hii.

Wafanyakazi wake wamekuwa hawalipwi likizo za uzazi na pia hata Mara wajifunguapo wamekuwa hawapewi yale masaa ya kuwahi kwenda kunyonyesha watoto hivyo hufanya kazi kwanzia saa moja mpaka saa kumi na moja jioni.

Kama sikosei Rais alitoa tamko fulani kuhusiana na suala la makampuni haya ya uwakala wa ajira kuwanyonya wafanyakazi na kutaka yaangaliwe upya.

Hamna ambacho kimefanyika.sana sana wafanyakazi ambao wanakuwa chini ya mawakala hawa huwa wana fikiriwa miaka yote kama ni Vibarua haijalishi wamekaa miaka mingapi katika kampuni husika. Mimi binafsi nina ushahidi Mkubwa kuhusiana na Kampuni inayoitwa NFT.

Nina ndugu ambaye ameajiriwa Tigo kupitia wakala huyu wa NFT tunaiomba serikali ipate muda wa kuongea na wafanyakazi ambao wameajiriwa kupitia Wakala huyu.

Wafanyakazi hawa wanakosa Malipo ya Likizo ya uzazi, wanakosa muda wa kuwahi nyumbani kunyonyesha mtoto/ watoto pamoja na wao kufanyishwa kazi masaa mengi zaidi ya walioajiriwa na Kampuni husika moja kwa moja.

Ushahidi wa mambo haya upo na sasa imefikia hatua sisi Watanzania tunanyanyasika sana na Serikali yetu haijui au haitaki kulichukulia hatua jambo hili.

Tunaomba pamoja na kuwa na shida ya ajira, serikali iliangalie jambo hili kwa kina. Na makampuni ambayo yanaajiri wafanyakazi kupitia kampuni hizi wasiwanyanyase wafanyakazi wao.

Zaidi zaidi mambo haya wadau tusaidiane kuyapeleka katika vyombo vya sheria.
 
Kuhusu hayo makampuni si kwamba yana hasara kwa wafanyakazi tu, hata kwa makampuni 'mama' yanayofanyia kazi kwa sababu wengi wa wafanyakazi wanalipwa ujira mdogo usio na motisha unaopelekea kufanya kazi bila ufanisi. kwa mfano mtu anayefanya kazi call centre kama halipwi vizuri ataendelea kutoa majibu ya "subiri kidogo tatizo lako linashughulikiwa au kutopokea simu za wateja.
pia makampuni haya yanaongoza kwa kuchukua watu wasio na weledi au elimu ndogo ili kuwapunja mishahara. KWANGU MIMI HILI NI JANGA KUU
 
Back
Top Bottom