Heri ya sikukuu ya wafanyakazi, nyongeza za mishahara ni msingi wa mafao Bora

Apr 11, 2024
21
52
Kulingana Na Historia Ndogo Kutoka Kwa Walimu Wetu wa Historia... Sikukuu Ya Wafanyakazi Ni Matunda Ya Mapinduzi Yaliyochochewa na Unyonywaji (Excessive Exploitation) Waliopitia Wafanyakazi Wakiwa Kazini, Mfano;
Kufanya Kazi Kwa Saa Nyingi Na Kulipwa Kidogo, Kufanya Kazi Katika Mazingira Hatarishi, Lakini Pia, Wafanyakazi Kutozingatiwa Hata Baada Ya Kuathiriwa Na Mazingira Mabaya Ya Kazi; Mbadala Wake, Walisimamishwa Kwa Kutokukidhi.

Sababu Mbalimbali Za Kinyonyaji (Exploitive) Ikiwa Pamoja Na Hizo Sababu Chache Nilizozitaja Hapo Juu, Zilikuwa Miongoni Mwa Sababu Zilizopelekea Wafanyakazi Kuandamana Kwa Madai Ya Haki Zao Za Msingi Kutoka Kwa Waajariwa Wao.

Mafanikio Ya Maandamano Hayo Ya Wafanyakazi, Yalifanikiwa Kuchochea Mabadiliko Ya Sheria, Na Kuwa Ya Kumlinda Mfanyakazi, Ikiwemo; Kuzingatia Muda wa Kufanya Kazi, Kuwepo Kwa Mazingira Rafiki Kwa Usalama wa Wafanyakazi, Mfano; Uwepo wa Miundombinu Rafiki Kwa Wafanyakazi Wawapo Kazini, Pamoja Na; Uwepo wa Mikataba Rafiki Isiyoumiza Wafanyakazi.

Lakini Pia, Kwenye Karne Ya 20 (1919) Kutokana Na Umuhimu wa Kuwepo Na Haki Kwenye Jamii, Kuliweza Kuanzishwa Kwa Shirika La Kimataifa La Wafanyakazi, “International Labor Organization”, Linalolenga Zaidi Kukuza Ajira, Na Kuwalinda Wafanyakazi Wote Duniani.

Kwa Nchini Tanzania. Sikukuu Hii Ni Siku Ya Kutathmini Maisha Ya Wafanyakazi Mbalimbali, Wakiwemo wa Sekta Binafsi, Na Sekta Za Umma... Lakini Pia, Ndiyo Siku Maalumu Ya Kufanya Maboresho Mbalimbali, Mfano; Maboresho Ya Sheria, Ili Kumuwezesha Mfanyakazi Kuishi Maisha Bora, Ikiwemo; Kuwapandisha Daraja, Kuwapa Likizo Wanawake Wafanyakazi Kulingana Na Hali Zao Za Uzazi Wanapojifungua, Lakini Pia Kuwaongezea Mishahara Wafanyakazi, Ili Kuendana Na Uchumi wa Dunia.

Nachukua Nafasi Hii Kuwatakia Heri Ya Sikukuu Ya Wafanyakazi, Wafanyakazi Wote Duniani.

“Nyongeza Za Mishahara Ni Msingi Wa Mafao Bora, Na Kinga Dhidi Ya Hali Ngumu Ya Maisha”

#KAZIIENDELEE 🇹🇿
 
Back
Top Bottom