WATANZANIA WENGI TUNAJITENGENEZEA MAZINGIRA YA KUTAPELIWA/RUSHWA SISI WENYEWE. laini hiyo/hizo inatolewa BURE. kikubwa ni wewe kutimiza vigezo na masharti: kitambulisho chako, picha, leseni hai ya biashara, nambari ya utambuzi ya mlipa kodi (TIN-tax identification number). zaidi utaulizwa eneo lako la kazi na uwezo wako wa mtaji na/au uelewa wako kuhusu biashara husika. ukitumia middle-man (dalali) ujiandae kulipia atakachokuhudumia iwe direct/indirect.
*sio mbaya endapo utaamua kununua laini iliyotumika moja kwa moja toka kwa mteja endapo tu utakuwa tayari kubeba athari zake (bare risks). na hizi sio laini za kawaida kama tunavyosajiliwa mitaani kwa 500. itategemea na bei anayoitaka muuzaji na pengine soko la eneo ama yeye alinunuaje. yaweza kukuhitaji mamia kadhaa ya maelefu (100,000+)
*voda wanakupa line/cheap 2-ya stoo na ya kazi
[HASHTAG]#ukiamua[/HASHTAG] kuchukua USED IN USE. utaitambuaje kuwa ni till au laini ya kawaida? chunguza nyuma ya laini zote 2. zina chapa ya 64 sio 32.
*airtel na tigo wanatumia line 1
##kuwa huru kuuliza mengine nitakumegea kile nikijuacho. uliza hapa hapa sio pm ili na wengine wawe huru kuelewa au kunikosoa.