Mavunde: Vyama vingi nchini vimesababisha kushuka kwa uzalendo kwa wananchi

Huyu naye ni kilaza tu,majizi yote yako chama kimoja,kilicho madarakani,majizi yote yamepita JKT,majizi yalikuwepo hata kabla ya 1992,
Uzalendo hausihani na vyama vyingi,uzalendo umeporomoka kutokana na uongozi mbaya,mbovu,wa waliotuongoza tangu Uhuru,
 
Hayo kayasema leo Bungeni,pia amedai vyama vingi vimesababisha kuongezeka kwa pesa ya Ruzuku kutoka serikalini kwenda kwenye vyama vya siasa
Uzalendo kwa tafsiri ya awamu ya ni kuunga mkono fikra "sahihi" za jiwe. Hata hivyo wasichoelewa CCM ni kuwa upinzani uliowekewa utaratibu kwenye katiba ni bora zaidi kuliko upinzani wa ndani kwa ndani. Nyerere alishanusurika kupinduliwa mara kadhaa wakati wa chama kimoja tofauti na zama hizi za vyama vingi
 
Umesema kweli Mavunde; Mh. Rais anatuhimiza kuunga mkono rasilimali zisiporwe na mabeberu lakini CHADEMA kupitia Lissu wanatetea wezi wa rasilimali zetu. Kuna uzalendo hapo jamani ktk vyama hivyo?
 
Ndugu The Icebreaker hata usipoteze muda wako kurudi kuchangia. Kuchangia hoja hii ni sawa na kujishusha hadhi kuwa na sawa mtoa hoja (sio aliyei-post). Kumbuka msemo wa wenzetu "usibishane na mjiga, vinginevyo wanaowasikiliza hawataona tofauti kati yako na yeye"

Pongezi zote kwako.
Ni mjinga badala ya Mjiga.
 
Msalimie mkulu kulu , mwambie akupandishe akupe uwaziri kamili angalau ufaidi zaidi mema ya nchi. Hawa wapinzani wameingiza nchi katika mikataba ya ajabu , siwapendi kabsa. CCM mbele Kwa mbele
 
Vijana tulitegemea wataleta mabadiliko chanya wakipewa nafasi za uongozi kumbe ndiyo kwanza vijana ndiyo nyanya mbovu kabisa mwenye uongozi.

Usishangae mwisho wa siku mzee Chenge anakuwa kiongozi bora kuliko huyu kijana Mavunde.
 
Hayo kayasema leo Bungeni,pia amedai vyama vingi vimesababisha kuongezeka kwa pesa ya Ruzuku kutoka serikalini kwenda kwenye vyama vya siasa
Daaaah!!! Rafiki yangu,schoolmate, learned bro, ndugu ni ww kweli au tumbo ndio linaongea.. !!?? Siwezi amini
 
Back
Top Bottom