Poleni na majukumu wapendwa wana janajanvi, niweke wazi kuwa mimi ni Mkristo, kitambo nimekuwa nikipata shida kuhusu mavazi hasa Dada zetu. Ni wazi kuwa kanisani ni nyumbani mwa Mungu, swali langu la msingi ni Je! watu wazuiwe kuvaa mavazi yasiyo ya heshima au walishwe neno ili wakisha shiba neno mioyo yao itabadilika na hatimaye kuvaa nguo za heshima?
Mfano wale dada zetu makahaba, kahaba jumamosi kalala kwenye uzinzi kunakucha asubuhi ni jumapili huku akiwa na kinguo chake kifupi anaamua nivyema amrudie Mungu, na msukumo wa hitaji la Mungu unakuwa ndo pekee ndani ya moyo wake,anaoona hahitaji kurudi hata nyumbani badalayake anaamua aeende kanisani ili kutubu na kumrudia Mungu, je! huyu mwnzetu tunamuhukumje akiwa na kinguo chake nusu uchi ndani mwa nyumba ya Mungu?
Karibuni wachambuzi nataraji hekima na busara itatumika kwa maelekezo.