Maurice: Jogoo mwenye kelele nyingi ashinda kesi dhidi ya majirani zake

Jollie

Member
Jul 26, 2019
35
64
Mahakama ya Ufaransa imetoa hukumu ikumuunga mkono mmiliki wa jogoo mmoja baada ya kelele za alfajiri za kuku huyo kuwakera majirani zake.

Maurice kutoka kisiwa cha Oleron katika pwani ya Atlantic alituhumiwa kwa kuwakera wanandoa waliostaafu wanaomiliki nyumba ya likizo katika eneo hilo.

Habari za matatizo yaliomkabili zilisambaa kote duniani na kupata mashabiki chungu nzima.
Mmiliki wake Crinne Fesseau alifurahia uamuzi wa kesi hiyo.

''Ni ushindi wa kila mtu aliyepo katika hali yangu .Natumai uamuzi huo utakuwa wa kuigwa'' , alinukuliwa na gazeti la AFP akisema.

Wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo mwezi Julai, mawakili wake walikuwa wamehoji kwamba malalamishi hayo ni hafifu kwa kuwa kuwika kwa kuku huyo ni hali ya kawaida ya maisha ya taifa hilo.

Bi Fesseau ambaye aliishi katika kisiwa hicho cha Oleron kwa miaka 35 katika pwani ya Atlantic angelazimika kuondoka eneo hilo ama kumnyamazisha kuku wake iwapo jaji angetoa hukumu dhidi ya jogoo hilo.

Sasa atalipwa Yuro 1000 kama malipo ya kumpotezea wakati wake mawakili wake walisema siku ya Alhamisi.

Leak hiyo iliungwa mkono na watu 140,000 katika mitandao ya kijamii waliowasilisha ombi la kuipinga.
Jogoo mwenye umri wa miaka minne amekuwa maarufu nchini Ufaransa ambapo jogoo yupo katika nembo ya taifa.

Biashara zimefanya kwa niaba yake huku barua za kumuunga mkono zikitoka kutoka umbali wa Marekani kulingana chombo cha reuters.

Kesi hiyo iliopata umaarufu imezua wasiwasi mkubwa kati ya wakaazi wanaoishi mashambani nchini Ufaransa na wale wanaohamia mashambani ili kutoroka maisha ya mijini.

"Huu ndio uvumilivu - lazima ukubali mila za mitaani," Christophe Sueur, meya katika kijiji cha Bi Fesseau, aliiambia AFP.

Meya wa mji mwingine, Bruno Dionis du Sejour, aliandika katika barua ya wazi mnamo mwezi Mei akitaka kelele za maisha ya vijijini - ikiwemo zile za ng'ombe na kengele za kanisani - ziandikwe kwenye orodha ya urithi wa Ufaransa ili kuwalinda dhidi ya malalamishi kama hayo
IMG_2210.JPG

IMG_2211.JPG
 
jogoo ashinda kesi dhidi ya wale wasiojua umhimu wa uumbaji wa mungu. Hapa ni sawa na kumwambia mtu kilema atembee mwendo unaoutaka wewe ikiwa ni kawaida yake kuwa hivyo. Hawa wamestaafu mpaka kufikiri. Dah! Wastaafu oyeeee
 
Ili kulielewa suala hili, ni vyema ukachagua approaches mbili (labda mjongeo wa kifikra):

1. Haki za wanyama.

2. Haki za binadamu.

Ukweli ni kwamba msingi wa Sheria ni mahusiano baina ya mtu na mtu. Mtu anaweza kuwa mtu halisi au mtu kisheria: mfano: kampuni nk. Mtu anaweza pia kumaanisha watu.

Msingi wa shauri hili kushinda:

MUDA. Muda bado haujataja kwamba jogoo kuwika ni kero (nuisance).

Utata wa uamuzi huu:

Tayari baadhi ya vitoaji sauti vingine (tofauti na binadamu) vimewekewa ukomo wa ukubwa wa sauti. Ukomo huo ukizidi, miliki anawajibika.

Utamu wa uamuzi:

Pamoja na jukumu la Sheria kuleta amani na kupunguza kadri iwezekanavyo kero, Sheria inatambua kwamba kero ni sehemu ya Maisha yetu. Hili ni muhimu sana.

Kero inakuwa kero kwa kipimo cha kijumuiya siyo kwa 'very individual': reasonable person in ordinary environment. Abnormalities sio kipimo.

Asante kwa kusoma.
 
Back
Top Bottom