Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,417
Isipokuwa tu wale wanawake wenye mapenzi ya dhati, lakini kuna wale ambao wana sura mbili yaani ni waongo waongo hakuna mfano.
Ngoja nitaje miongoni kwa mauongo yao yanayotukera sana sisi wanaume.
1.Ni rafiki yangu tu...
Hapa utakuta anaye rafiki wa kiume anayewasiliana naye mara kwa mara pamoja na kwamba mko kwenye uhusiano na ukimuuliza anakujibu, huyu ni rafiki yangu tu, lakini urafiki wao ni wa kutiliwa mashaka. Wanakuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na mwanaume huyu anapewa kipaumbele kwa kila kitu. Je unataka kujua kinachoendelea kati yao? Kama umeuchoka uhusiano wako na yeye mchunguze.
2. Idadi ya wanaume aliowahi kuwa nao kimapenzi...
Hakuna mwanamke mwenye ujasiri wa kujibu hili swali kama akiulizwa na mpenzi wake. Ni ngumu mwanamke kukiri ni wanaume wangapi wamewahi kuuona utupu wake. Thubutuuuu..
3. Sababu ya kuachwa na mwanaume wake wa mwisho kabla yako...
Lazima atadanganya kwamba ni yeye amemuacha mwanaume. Atadanganya kwamba yeye ndiye amekosewa akaamua kumuacha mwanaume huyo.
4. Kujifanya mshamba wakati wa tendo kama vile hajawahi vile..
Huu uongo wanaume wengi wamewahi kuushuhudia kwa wanawake maana mwanzoni utadhani hawajui karufundi ka ule mchezo kumbe ni magwiji hatari. Kuna wakati wanapiga makelele wakijidai wanaumia kumbe uongo mtupu wananogewa hatari.
5. Yaani sina hata hela..
Jamani wanawake hebu mtuonee huruma basi maana hakuna siku mwanamke atakwambia ana hela kila siku atalalamika hana salio kwenye simu, hana hela ya salon, hana hela ya kyupi hana hela ya makochokocho ya ulimbwende na mambo mengine ya misosi na kadhalika.
6. Niko kwenye siku zangu...
Unakuwa na mitoko na msichana kwa kipindi kirefu labda, kakuchuna mbaya, siku inatokea anakuja maskani labda unataka ku doo anasema 'Kidundisha moyo wangu I'm on my period.' anasahau ni majuma mawili yaliyopita alikupa sababu hiyo hiyo. wakati mwingine wanaume huwa tunajiuliza hivi baadhi ya wanawake wanakuwa kwenye siku zako kila siku!
Mnatuchosha badilikeni.....