Ndg, wadada na wakaka ambao mnawatafuta au kuwachumbia kwa sasa walishawahi kuwa na watu huko zamani. Kwa hiyo kitu hiyo walifanya labda tofauti ni kuwa hawakupiga hizo picha za utupu wakiwa kwenye hilo zoezi! Kikubwa ni kukaa na huyo mwenzio na kumshauri awe muwazi na huyo x wake na pengine kujuwa ni nini kilichowatenganisha.
Inavyoonyesha ni kuwa huyo x wake ameumia kuona kuwa wewe umempata la aziz wake wa zamani hivyo anatafuta namna ya kukufanya umchukie hiyo binti uliyempata ili acapitalize kwenye ugomvi wenu
Lakini pia uwe mwangalifu maana huyo binti naye kama haeleweki hivi, maana kwa akili za kawaida sidhani kama ni busara kupiga picha za namna hiyo katika ulimwengu huu wa sasa.