Sis kwa maswali magumu: Furaha iipo kwenye upendo usiohesabu "gharama" .......na hakuna utimilifu kwa binadamu lakini tunatakiwa tuenende kama watu wanaotafuta utimilifu huo na si bila dira yeyote
gfsonwin, ishu ni kubalance kati ya moyo na akili kipi kifanye maamuzi kulingana na mazingira husika.
maslahi, kwa case hii ni faida yoyote kutoka kwa mtu unayekuwa naye katika mahusiano ya kimapenzi ispokuwa 'hisia za kweli za kimapenzi na mtu huyo'
Hapa tunamaanisha mahusiano ya kimapenzi, maana haya ndiyo mahusiano ya mwanaume na mwanamke ambayo huleta majonzi chungu tele kila kukicha.
Hapo kwenye hao wenyewe wanoingia kwenye mahusiano huwa tayari wame-define terms zao mapema lakini in the long run, inakuja kubainika kuwa mmoja wapo hakuwa na mapenzi ya dhati, na hivyo kumtenda mwenziwe, mara nyingi huwa alivutiwa na mambo fulani fulani tu yalimlazimisha kuingia kweney hayo mahusiano. Hapo ndipo tunapotaka kujadili, nini tufanye kupunguza hii hali!
Duh, pole bana, naona leo cacico yupo kichwani mwangu sana.
Hata mtu akupende genuinely, off course kama binadamu anakuwa na mapungufu
Nachoongelea hapa ni pale unajua kabisa huyu mtu si wa muda mrefu au si match ya aina ya mwenza wangu lakini unakuwa naye tu kwenye mahusiano sababu ushampenda so unaamua kufumbia macho yale usiyoyapenda
[/B]hapokwenye bold ndipo mimi nilipokuwa nasemea Kongosho. ifike mahali dada mzuri tuache kupenda kwa hisia tpende kwa kiuhalisia
Umeona eeh, hapa ndio hutugharimu wote, wake kwa waume.
Angalia Matonya alikuwa analilia kuwa "Spare Tyre', afu akija kuumia mwishoni alalamike? lol
mdogo wangu and thats where the problems comes. katka makosa makubwa ni mtu kuona kwamba furaha yake iko established kwenye mapendo siyo kweli hata kidogo. Furaha iko established ndani ya nafsi ya mtu kwa component mja tu iitwayo amani. kama unayo amani furaha ipo tu lazima manake yawezekana usipendwe lakin ukawa na furaha.
and if this is the case basi tuangalie amani yetu twaipatia wapi ndipo utakapojua upendo uko established wapi. hakuna binadamu mtimilifu na kwakulijua hilo nafikiri hatupaswi kuumizwa na mapungufu waliyo nayo wenzetu bali tuyapokee kama changa moto
stephot hizo ni hisia tu manake wapo wenye pesa, mali akili na kila kitu lakini wamedivarce hadi mara 2 ama 3 to me kupenda inabidi kuwe ni kiuhalisia kwa kutumia akili zaid kuliko moyo. akili will look for a solution na haikupi maumivu yaletayo ugonjwa wa chuki nafsini. nilipokuwa napita go read thread ya uvumilivu you will understand what i mean.Mapenzi ya sasa wengi huwa wanatamaniana huwa hawapendani kwa dhati,wapenzi wanaangalia uwezo wa kipesa,shule ya mtu,kazi anayofanya,uzuri wa sura au maumbile,uvaaji nk.swala la tabia halitiliwi maanani kabisa na mwisho wa yote mnapokuja kugundua tabia zenu hazilingani ndio pale vurumai linapoanza.
NINGESHANGAA KAM HUJACHANGIA HII MADA MANA HAPA UWANJA WAKO WA NYUMBANI ,mambo vipi wewe TukoMapenzi ni kama kuendesha gari. Siku nyingine ugonge, uvunje taa, kioo nk. Siku nyngine ipate pancha. Siku nyingine ipate ajali, achakae kabisa. Siku nyingine uichoke... Siku nyingine uchukue tax!!!
Maumivu ni part and percel ya mapenzi, they come together...
Lakini usisahau kuwa upendo ndiyo huleta hiyo amani.....Huwezi kuwa na amani bila huo upendo! Namaanisha si tu upendo kutoka kwa mtu mwingine bali unaotoka kwanza kwako mwenyewe.
Umesema kuyaona mapungufu ya mwenzako ..ndio unaweza kuyaona kama changamoto (na si tatizo) kama una upendo ndani yako.....kama huna ni vigumu kuzibeba hizo changamoto au utazibeba kwa maumivu yasiyosemeka. Na kwa kuongezea hapa ni rahisi sana ku-torelate makosa ya mtu unayempenda au anayekupenda kuliko yule usiyempenda.
Amani ni tunda la upendo na haijisimamii yenyewe
ningeshangaa kama haujachangia hii mada gfsonwin uwanja wanyumbaninakuhakikishia usipopenda kwa akili wallah siku ya kwanza ya pili unabeba virago unaondoka, akili inakupa uvumilivu kwani inakutafutia suluhu ila si moyo utakutengenezea chumba cha ugonjwa nafsini mwako.
ngoja nikusahihishe inaelekea ualimu wangu bado sijaufanya vizuri kwako. upendo ni tunda la rohoni, upendo wakati mwingine huchangiwa na amani uliyo nayo. kama huna amani nafsini ni vigumu sana kupenda. mfano hujawah kuskia mtu akisema nilipomwona tu fulani amani yote ikaondoka? wafikiri kama amani imeondoka upendo upo tena hapo?
so amani lazima itangulie na ndio maana hata wenye imani zadini huwa waanza kwa kutakia amani ili kuleta upendo katikakti yetu.