Maumivu ya kichwa huanza pole pole | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maumivu ya kichwa huanza pole pole

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kichakoro, Mar 10, 2009.

 1. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2009
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,548
  Likes Received: 1,307
  Trophy Points: 280
  Wandugu

  Nimesoka habari ya Mh. Mwinyi kupigwa kibao shavuni kwa masikitiko makubwa.


  Watu walianza kwa kuwasema mafisadi hadharani bila hofu, watu wakasubiri shubiri ingefuatia kukawa kimya, ikawa asubuhi ikawwa jioni siku ya kwanza.

  Baadae watu wakaanza kuwa zomea viongozi wakuu wa nchi na hata kuwauliza maswali magumu hadharani, watu wakasubiri hamsa kumi nambili hakuna chochote kilichotokea. Ikawa asubuhi ikawa jioni siku ya pili.

  kama vile haitoshi watu wakampiga rais wa nchi Mawe kwa kushindwa kusikiliza kero zao, tukasubiri watu walubishwe, hakuna kilichotokea ikawa asubuhi ikawa jioni siku ya tatu.

  Leo tena mkuu wa zamani wa nchi na amiri jeshi mkuu mstaafu kavutwa sharubu na kupigwa vibao nae akasema chukua na ubavu mwingine, nalo litapita hivi hivi ikawa asubuhi ikawa jioni siku ya nne.

  Je ni nini kinafuatia???????? Sehemu zilizowahi kuwa na vita na mitafaruku mikubwa, migogoro yao ilianza kwa style kama hii mwishowe tutakuwa wakimbizi sijui wapi maana hatuna pa kukimbilia japo tumezungukwa na nchi nane tofauti

  hata maumivu ya kichwa huanza hivyo hivyo mwishowe.......... Tusipoziba ufa.....


  kichakoro,
  Wazee wa Kuchoma Ndizi
   
 2. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  SAFI SANA bado Mpaka!
   
 3. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0


  Usipozipa ufa utajenga ukuta!....i guess
   
 4. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #4
  Mar 11, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kelly01 mimi natafuta nauli tu
   
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  Mar 11, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Hichi ndiko tunachoita click generation -- kila kitu mtu apati tabu ana click tu kasoma maoni ya jf wee anaenda kutekeleza mitaani , nyumbani kazini
   
 6. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nauli ya kwenda wapi shy?..Ahera? au?
   
 7. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2009
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,548
  Likes Received: 1,307
  Trophy Points: 280
  Sio kwamba watakulia chabo....???  wazee wa kuchoma ndizi
   
 8. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tafsiri ya usipoziba ufa utagenga ukuta manayake nini? Unamaanisha hawa vijana wanasolubu wachapa viongozi waadhibiwe ama walinzi wao? Napata woga sana, pale napoona jamii lengo lake kuu ni kulinda usalama wa viongozi tu no matter what! kwanini hatujiulizi kwanini watu wanapata kibri cha kuibuka na kupiga watu au kutishia amani wa viongozi wao? Inamaanisha waliopita walikuwa hawatishiwiwi? Matishio ya aina gani yalikuwepo kipindi cha nyuma? Je yanabadilika? Na kama yanabadilika maana yake ni nini? Tukijijibu ndio hizo nyufa tutazigenga, ama sivyo mafuriko yatakuja tu wakati ndio tumepachika udongo, tukabaki na historia tu!
   
 9. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2009
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,548
  Likes Received: 1,307
  Trophy Points: 280
  Mkuu Good question,
  Kikubwa hapa ni watu kukata tamaa na wanaowakatisha tamaa ni viongozi ambao wamefanya maisha ya watu kuwa magumu. wakti wa Nyerere hali ya maisha haikuwa ngumu kama sasa, hata ukilinganisha miaka 5 nyuma hali sio mbaka kama sasa.

  Lakini wame wameanza kufahamu kwa nini wako hapa tulipo mifano michache Ufisadi hatuoni hatua zikichukuliwa dhidi ya mafisadi, mikataba mibovu kuanzia IPTL na wengine unawawekea wanainch mzigo hakuna hatua zinazochukuliwa.

  Je kuwavuta sharubu, kuwapiga mawe, kuwazomea kumesaidia????? kama haijasadia nini kinachofuata????

  WAZEE WA KUCHOMA NDIZI
   
Loading...