Maumivu makali mwilini ya muda mrefu (miaka 10)

georgeallen

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
4,118
1,868
ndugu yangu ana maumivu makali mwili mzima kwa miaka 10 sasa. Maumivu ni makali zaidi usiku. Anajisikia kuchoka sana na kujisikia usingizi hasa mchana. Anatoka jasho kwa wingi na lina harufu kali. Hapati choo sawasawa licha ya kula vyakula vya asili, mbogamboga na kunywa maji mengi. Je ana tatizo gani ndugu yangu huyu? Naombeni msaada jf doctors.
 
labda ungesema kaenda kwa madaktari kadhaa, katumia dawa kadhaa. Kifupi utashauriwa mkamwone daktari tu maana mwisho wa siku ni taiba inahitajika. Mpe pole
 
Ilikujua medical diagnose ya tatizo kuna mambo mengi wala siyo Dalili tu anazoonesha mgonjwa ili kujua tatizo la ugonjwa anaoumwa kitu cha kwanza ni historia ya mgonjwa , cha pili Kufanya physical assessement (feeling,listening na looking) katika mifomo ya mwili yote kuanzia kichwa hadi miguu, tatu -vipimo vya maabara , x-ray, CT- scan . Mwambie akapime magonjwa haya turbeculosis( TB) , Ugonjwa wa moyo(Heart attack), kisukari(diabetics) , cancer ya tumbo , na HIV .
 
Nashurukru kwa ushauri wenu mzuri. Nitamfanyia vipimo vyote kama mlivyoshauri na nitawajulisheni matokeo asanteni sana. Cheers
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom