Maumivu makali kwenye kitovu

Veronica7598

JF-Expert Member
Jan 2, 2017
361
408
Wakuu habari zenu wapendwa.

Nimerudi tena kwenu kuomba ushauri na kubadilishana mawazo,

Najua humu ndani kuna madaktar na wenye uelewa wa mambo ya afya na wanawake wenzangu waliopitia hali kama yangu.

Jana usiku mishale kama ya saa5 usiku, niliumwa sna na tumbo lilikua linavuta kwenye kitovu kwa ndani kama nimechomwa sindano ya kitovu yaan.
basi mr. akanitafutia dawa za maumivu nikanywa lakini sikupata nafuu, ikabidi aangaike ile usiku mala anikande tumbo labda vitaacha wapi, akapata wazo akanipikia uji ile usiku nikanywa baada ya kunywa ule uji wa moto kidogo nikalala..kuamka asbh maumivu nayasikia yapo ila kwa mbali.

Basi nikawasiliana na dkt wangu nikamweleza, akashangaa maana jana hiyo ilikua siku yangu ya clinic nilikua nae hospital mida ya jion nikapima vipimo vyote nipo ok, sina tatizo. Basi akanishauri nitumie buscopan, nimemeza asbh na mpaka sasa bado nasikia maumivu kwa mbali.

Yaan nimeshindwa hata kwenda kazin kwa haya maumivu, natembea kama vile kikongwe nimeinama.

Je? wataalam wa afya hali hii kwangu ya kawaida au nirudi tena hospital nikapige utrasound maana sielewi maumivu haya vepe! nasijawah kuumwa na kitovu namna hii, Isitoshe ni mjamzito wa miezi5.

wataalam naomba ushauri wenu, Nisamehen kwa maelezo marefu.
 
Ndio maana kakaa kimyaaa mwaya, nisamehe kama nimekosea kukuita boy, au girl
 
Back
Top Bottom