Msaada: Mke wangu mjamzito anapata maumivu chini ya kitovu

Kaiche

Senior Member
Jan 23, 2017
141
269
Habari JF,

Kwanza namshukuru Mungu kwa kuamka salama na kunipa uwezo huu wa kueleza changamoto iliyopo.

Naenda kwenye mada, Wife wangu ni Mjamzito, ila changamoto iliyopo ni maumivu ya tumbo chini ya kitovu, na maumivu haya yapo kama kuna kitu kinataka kutoka.

Jana niliongozana nae kwenye hosptal ya wilaya, na dokta akamchek Malaria na U.T.I ,,ila hana hata kimoja, Na akamuandikia Pcm na Amoxylin.

Tupo nyumbani na bado hali ni tete, tumbo linavuta sana na hii mimba ni miezi saba sasa.

Msaada wenu tafadhali
 
Mimba ya ngapi jomba?

Mtoto anacheza? Mapigo ya moyo ya mtoto yanasomaje kwa dakika?

Ana tokwa na maji au uchafu wenye harufu au dam huko chin?

Presha ya mkeo na Joto mwili vinasoma ngapi?

Hapo wilayan mmefanya Ultrasound ?
 
Mimba ya kwanz kwake
Pia hajapimwa pressure wala mapigo ya moyo
Ok
Hakuna uchafu wowote wala damu kiongoz ,, lakin pia kwa jana hajafanya utra sound
Nashaur Uende Hosp uwaambie wamfanyie US , kuangalia Maendeleo ya mimba kwa upana wake pia Ni haki ya mama kufanyiwa vipimo vidogo vidogo mf presha, wingi wa damu n.k

Lkn pia hawa mimba za kwanza, huwa wanapatwa na maumivu ya uchungu wa Uongo yaan anaweza hisi anataka kuzaa kumbe hamna ... Mama aendelee kuchek km Mtoto anacheza .
 
OkNashaur Uende Hosp uwaambie wamfanyie US , kuangalia Maendeleo ya mimba kwa upana wake.

Lkn pia hawa mimba za kwanza, huwa wanapatwa na maumivu ya uchungu wa Uongo yaan anaweza hisi anataka kuzaa kumbe hamna .
Ahsante kiongoz kwa ushaur wako
 
Back
Top Bottom