Mlaleo,
Hapana siokotezi huwa nafanya utafiti wa kutosha.
Hadi sasa nina vitabu 10 katika jina langu na miswada kadhaa inayosubiri In Shaa Allah kuchapwa vitabu.
Baadhi ya vitabu vyangu vimechapwa na Oxford University Press, Nairobi na New York.
Hawa hawachapi vitu chembelecho vya "kuokoteza."
Inawezekana roho yako inauma labda kwa hasad tu ndani ya nafsi yako.
Historia ya Rajabu Ibrahim Kirama nimepitia nyaraka zake zinazokaribia miaka 100.
Ukisoma kitabu utaziona katika rejea.
Ama kuhusu kubadili historia.
Mimi nimeweza kubadili historia.
Nimebadili historia yote ya TANU na uhuru wa Tanganyika na historia ya Nyerere yote katika kitabu cha Abdulwahid Sykes kilichochapwa London 1998.
Ukiwa hujakisoma kisome.