CPU
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 3,863
- 687
Maulamaa wa Kishia na Kisuni wa Copenhagen nchini Denmark wametoa fatuwa ya pamoja wakiharamisha mashambulizi ya aina yoyote yanayowalenga Wakristo na makundi mengine ya kidini.
Maulamaa hao walioshiriki kwenye mkutano uliofanyika katika mji mkuu wa Denmark wametaka kutolewe adhabu kwa watu wanaohubiri utumiaji mabavu na machafuko kati ya makundi ya kikabila na kidini na kueneza chuki na uhasama baina ya wafuasi wa madhehebu tofauti. Wasomi hao wa kidini pia wameitaka serikali ya Iraq kuliweka suala la kuwalinda Wakristo katika ajenda ya mkutano wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu uliopangwa kufanyika mjini Baghdad.
Mkutano huo uliotayarishwa na Denmark ikishirikiana na taasisi ya Uingereza ya Misaada na Suluhu Mashariki ya Kati umehudhuriwa na maulamaa wa Kishia na Kisuni na wanafikra wa Kikristo. Baada ya mkutano huo Kasisi Endrew White wa Kanisa la Kianglikana la Denmark amesema kuwa fatuwa hiyo iliyotolewa na maulamaa na wasomi wa Kishia na Kisuni wakilaani mashambulizi dhidi ya Wakristo inaonesha kwamba vitendo hivyo vya ukatili ni kinyume kabisa na mafundisho ya Qur'an.
Wakati wenzetu wanahubiri mshikamano na amani sisi tunahimiza UHASAMA!!!
Wakati wenzetu wanahubiri mshikamano na amani sisi tunahimiza UHASAMA!!!