Mauji ya north mara nini hasa kilitokea? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauji ya north mara nini hasa kilitokea?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kinepi_nepi, May 26, 2011.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ndugu wana JF bila kujali itikadi zetu na hisia, ningeomba tujadili kwa undani nini hasa kilitokea kwenye mauji yaliohusisha Barricks na wananchi wa Nyamongo.

  Upande wa serikali unasema wale walikuwa wavamimizi waliotaka kuiba dhahabu. waliwazidi walinzi (Polisi) nguvu hivyo polisi iliwapasa kutumia silaha za moto.

  Hapo hapo tunaona serikali hiyo hiyo ikijihusisha na mazishi kwa kununua majeneza na kudai kusaidia kufikisha miili kwa ndugu wa marehemu. Je huu ni utaratibu wa serikali?

  Je uhusiano wa mwekezaji na wanakijiji ukoje. tatizo ni mwekezaji au serikali yetu. Mkataba wa Barricks North mara unasemaje? Je uchimbaji huu umewaongezea wananchi wa Nyamongo nafuu ya maisha au umekuwa kero na taabu.

  Nini hasa wananchi wa Nyamongo walikuwa wanakifanya mpaka mauti ilipowakuta?
  Naomba tujadili .
   
 2. n

  nyandulu Member

  #2
  May 26, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sawa Bwana kinepi nepi, maswali yako ni ya msingi ila ukweli ni kwamba hawa watu si wavamizi ila ni wadai haki yao iliyoibiwa na barrick gold ni kawaida mahali popote penye utajili kuna mauti pia wawekezaji wezi hao hutumia vyombo vya dola kulinda maslahi yao. rejea yaliyotokea cong DRC, Nigeria the same kwa hii nchi ya mwalimu
   
 3. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mimi binafsi nina wasi wasi ya kwamba kama uongozi wa juu wa jeshi letu ukiendelea kuruhusu malalamiko ya wananchi dhidi ya jeshi hilo, yaendelea kushughulikiwa kwa namna ambayo inajenga hisia miongoni mwa raia, ya kwamba kuna kulindana, imani ya raia kwa jeshi hilo itakwisha kabisa. Aina budi ikumbukwe, katika kundi lolote la jamii ni kawaida kuwepo watu wachache ambao mienendo yao haiendani na matakwa ya kundi husika, hivyo ni jukumu la kundi hilo kudhibiti mienendo ya hao watu wachache ili wasije wakalipaka matope kundi lote. Ni katika msingi huo natoa rai kwa jeshi la polisi na kwa serikali kwa jumla, ya kwamba mara zote panapojitokeza malalamiko kutoka kwa wananchi dhidi ya polisi kujichukulia sheria mikononi mwao, malalamiko hayo yashughulikiwe haraka na kwa njia iliyo wazi, na baada ya hapo taarifa rasmi juu ya tukio husika itolewa; maana ukiacha pakawepo ombwe utakuwa umejenga mazingira ya kila mtu kusema lolote lile analotaka.
   
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Haya ni matokeo ya mikataba ya madini inayosainiwa guesthouses. haina maslahi kwa umma wala kwa serikali, bali kwa kikundi kidogo cha viongozi wenye commission zao. Wananchi wamechoka na kuamua kujichukulia angalao kidogo chao. Hebu angalia, mradi wa almasi unaingiza zaidi ya 50%, halafu ule wa barick 3%. Unaonaje. Mimi na hamu na uhuru wa Tanganyika.:mod:
   
 5. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa kama ni hivyo hao viongozi wa chadema wamekwenda kufanya nini huko?
   
 6. s

  smz JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtabe,

  Usitake tuamini kuwa wewe ni kati ya tunaowaita wavivu wa kufikiri. Tumikisha akili yako, au wewe mwenzetu mambo safi. Unataka kutuambia kwamba unashangaa CDM walienda kufanya nini huko? Kwani Tarime siyo sehemu ya JMT? Na unataka kutuambia kwamba viongozi wa kisiasa wana mipaka ya kufanya kazi zao?

  Hebu tufike mahala waTZ tuangalie mzunguko wa dunia unavyoenda.
   
 7. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Maswali uliyouliza yote ni ya msingi sana. Bahati mbaya kutokana na kutowajibika kwa serikali ndio maana ktk maelezomengi sana waliotoa hakuna hata moja linalojiba hayo maswali zaidi ya kujichanganya wao wenyewe. Kwa hiyo kwa maana ya majibu sahahi we may nerver get the response from responsible authorities.

  Kuhusu wananchi walikuwa wanafanya nini mpaka mauti iwakute utaona kutoka na evidence zilizopo mpaka sasa ni kwamba walipigwa risasi kwa nyumba in cold blood i suppose, hii inaonyesha they (waliokufa) were doing nothing.

  Behavior tunayoiona inafanywa na jeshi la polisi (likiongozwa na incompetent RPC-Tarime) ya kuchukua maiti saa nane usiku na mengineyo mengi kama kuandaa majeneza is very unbecoming kwa jeshi la polisi (sijui hii ndio polisi jamii - labda IGP atakuja fafanua some day) inayoonyesha kuwa polisi ni guilty conscious kutokana na kitendo walichofanya raia.
   
Loading...