Maujanja ya Computer haya(Must read)-No 3

Tuendelee na maujanaja namba 3 wa makomyuta na masoftware na mengineyo kama ifuatavyo:

1. Kutumia trial version software Forever!!

Ujue sofware nyingi ni za kununua na kama huna fedha basi utatumia hiyo software kama trial tu(siku 15 au 30) halafu muda ukiisha huwezi tena kuzitumia(expire date). Sasa hapa ndio umefika. Njia hii haina expire date kabisa. Kivipi Ungana nami.

-Hii njia inaitwa Time stopper. Time stopper ni software(just google it) ambayo inasimamisha muda kwa try out version software. Sasa unaposimamisha muda wa hiyo software basi utaitumia hiyo software 4-eva!!Muda wa hiyo software itarun kwenye hii time stopper na muda wa kawaida wa computer yako na tarehe zitaendelea kama kawaida.
-Jinsi ya kufanya:
-Download na install hiyo time stopper, then ifungue kwa double click.
-Sasa ifungue(browse) hiyo software yako(trial version), ukute kifile cha .exe
-Right click,fungua properties
-Chagua new date(tarehe yoyote kabla ya expiration date, unaweza kuchagua tarehe siku 2 kabla ya kuexpire)
-Hapo gonga choose any time
-Click open sofware katika tarehe uliyochagua hapo juu.
Hapo kuna angalizo kidogo, unaweza kutengeneza icon kwa hiyo modified icon ya trial version yako kwa kubonyeza ile button ya mwisho ya time stopper yako
.



2. Jinsi ya kuformat USB with NTFS

Kwenye window XP,Vista na 7 unaweza kuformat USB iende kwenye NTFS. Hapa ujue kuwa ukiformat hiz USB option iliyopo default ni FAT na FAT32 tu!! Hamna option ya NTFS.
Kivipi, twende:
-Connect USB yako kwenye computer
-Right click 'My Computer' halafu nenda Manage'
-Click device manage halafu expand Disk Drives
-Nenda kwenye USB drive list under Disk Drives halafu gonga properties
-Halafu nenda kwenye Policies tab
-Sasa hapa default policy ipo kwenye Optimize for quick removal. Hiyo badilisha na weka Optimize for performance.
-Sasa fungua Windows Explorer na right-click USB yako halafu chagua format.
-Hapo utakutana na option ya NTFS.
Kushney.


3. Andika Jina lako kwenye Saa.

Hapa unaweza kuandika kitu chochote unachotaka kwenye saa yako ya computer. Hii inaondoa lile neno la AM au PM na kuandika neno lako unalolitaka.(mfano 5:00AM itakuwa 5:00 MziziMkavu...hahaaaa!! So Fun)
(Kumbuka hilo jina/neno liwe na herufi 8...sometime zinakuwa chini ya 8).
Kivipi, twende!!
-Nenda hapa start->Run->halafu andika Regedit kweny hilo box
-halafu nenda hapa HKEY_CURRENT_USER\Control Panel\International
-Hapa ongeza new string ie "s1159" and "s2359"(mara nyingi utaziona, ila kama hazipo ziandike, hiyo moja ni ya AM na nyingine ni PM).
-Kama muda ni PM basi right clik hiyo halafu kwenye box futa PM halafu andika jina utakalo.(ziwe nane, zikiwa pungufu jaribu pia)
Kushney


4. Jinsi ya kuijua IP address ya connection yako.

Members wengi wanatumia tu internet bila kujua IP code zao, twende sasa!!
-Nenda hapa start/run, halafu andika 'cmd'.
-Halafu andika 'ipconfig'
-Halafu ongeza hii kitu '/all'
You're done!!
Tuishie hapo kwa leo:

Ijumaa njema

1 na 2 hizo hapa...
Maujanja ya Mirosoft haya hapa. No2.
Yajue Maujanja ya Computer hapa(should see this): No 1

2q1iefq.gif

2i9m911.jpg

jidhjp.gif
Asante mkuu kwa somo zuri...ila naomba information kuhusu hiyo NTFS; yaani itaperform namna gani kama USB flash itakuwa converted from FAT/FAT32 kwenda NTFS?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom