mauchafu unapohama nyumba!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mauchafu unapohama nyumba!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NasDaz, Jan 7, 2010.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Nilipokuwa Bwa Mdogo nilikuwa naishi na uncle wangu! Huyu bwana alikuwa na tatizo la kisaikolojia ambalo kitaalamu linajulikana kama Inferiority Complex! Siku moja baada ya kurudi home usiku, nikakuta uncle wangu amehama nyumba na wala sikufahamu amehamia wapi!! Lakini kilichonishangaza zaidi, ni kukuta nyumba ambayo amehama(yaani tuliyokuwa tunaishi) ikiwa chafu ile mbaya! Ma-box na matakataka yote unayoyajuwa wewe ya kinyumbani, yalikuwa hapo! Nikajiuliza maswali kadhaa, ikiwa na pamoja “ikiwa alifahamu anahama, kwanini hakuiacha nyumba ya wenyewe ikiwa safi?!” Nazani, nilikuwa “nasumbuliwa na utoto” kwani hata yeye mwenyewe mara kwa mara alikuwa ananiambia “kuwa uyaone!” Kama nilivyosema hapo awali, uncle wangu alikuwa anasumbuliwa na tatizo la kisaikolojia kwani ingawaje mchana wa siku hiyo tulionana, lakini hakutaka kabisa kuniambia kwamba hiyo siku tungehama!! Sikuwa na jinsi, bali ni kwenda kulala nyumbani kwetu, kwa baba na mama!! Siku ya pili alipokuja home, akajitetea eti hakutaka kunijulisha kwamba tunahama kwavile ningewaambia watu!!INFERIRITY COMPLEX!
  Hata hivyo, lengo la thread hii sio suala la uncle wangu kuhama bila kuniarifu, bali ni suala la kuhama na kuacha nyumba ikiwa chafu! Mimi wala si miongoni mwa watu wasafi, lakini angalu kwa jambo hilo peke yake, lilinikera! Binafsi nilihisi, baada ya kuhamisha vitu vyake, angeanza kufanya usafi na kuacha nyumba ya watu safi!
  Ama kweli, kua uyaone, ama kwa tafsiri sahihi ni kweli nilikuwa nasumbuliwa na utoto! Kwa mara kwanza, mwenyewe nilipanga chumba mwaka 2006! Chumba nilichohamia, nacho nilikikuta kichafu ile mbaya baada ya mpangaji aliekuwapo kabla nae kuhama na kuacha kama nilivyokikuta! Nikakumbuka miaka kadhaa nyuma siku ambayo uncle wangu alihama na kuacha apartment ikiwa robo dampo! Mwaka mmoja baadae, nikahamia sehemu nyingine ambako nako kulikuwa na mpangaji amehama!Nako nikakuta mauchafu kibao! Marapurapu ya kapeti, ya nguo mbovu na rundo la chupa za maji!!!! Miezi michache iliyopita, nikahamia sehemu nyingine, nako hakukuwa na tofauti sana na vile alivyokuwa ameacha uncle wangu au wapangaji wenzangu wawili walionitangulia!! Hapo ndipo nikakaa na kujiuliza, hivi huo ndio utamaduni wa binadamu au Watanzania?! Kwanini mara nyingi watu wanapohama kwenye nyumba walizopanga (probably na hata zile za waajiri wao) hawaziachi hizo nyumba zikiwa safi?! Ikiwa mtu ulikuwa unaweza kufanya usafi kila wakati kwa mwaka mzima, inakuwaje ushindwe kufanya usafi kwa siku moja ya mwisho? Mwaka nikija kujenga na kupangisha, basi moja ya masharti ya mpangaji ni kuacha nyumba yangu ikiwa safi kama alivyoikuta!
   
 2. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Wahama hama mno na weye bana! :)
   
 3. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  bongo kawaida nchi za watu mtu akikuta nyumba chafu haangaiki na wewe,anaita kampuni inasafisha kisha anapost bili kwako,na hiyo bili utakoma mwenyewe siku ingine ukihama utaikumbuka na kusafisha nyumba
   
 4. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Ajenge yake sasa
   
Loading...