Elly official
JF-Expert Member
- Sep 16, 2018
- 767
- 1,035
MTOTO AUWAWA BAADA YA KUUZWA
NA BABAYAKE MZAZI MKOAN MBEYA.
_____________________________________
Jeshi la polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili waliofahamika kwa majina ya 1.Japhet Yahaya Nguku(37)na 2.Andrew Anganile Mwambuluma kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wa miaka sita (06) aitwaye Rose Japhet wa kijiji cha Msewe,Wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Ni kwamba mnamo tarehe 03.05.2019 majira ya saa 21:00 usiku huko Kijijini Msewe Kata ya Igurusi ,Tarafa ya Ilongo,wilayani Mbalali ,Mkoa wa Mbeya katika msitu wa hifadhi ya Chimala mtoto aitwaye Rose Japhet alikutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na kukatwa kanyagio la mguu(unyayo) wa kulia ambalo limekutwa limefukiwa huko Mbalizi ,Wilaya ya Mbeya vijijini.
Chanzo cha mauaji hayo ni tamaa ya kupata utajiri ambapo baba mzazi wa marehemu aitwaye Japhet Yahaya Nguku alimuuza mwanae kwa Andrew Anganile Mwambuluma ambaye ni mfanyabiashara kwa malipo ya Tshs 5,000,000/= ili auwawe na kutolewa kiungo hicho cha mguu wa kulia kisha kipelekwe kwa mganga wa kienyeji amtengenezee ndagu (dawa ya utajiri)ili afanikiwe katika biashara ya shule ya sekondari Ushindi anayoimiliki iliyopo Mbalizi-Mbeya.
Mfanya biashara huyo amekiri kuhusika na tukio hilo .Ufuatiliaji unaendelea ikiwa ni pamoja na msako mkali wa kumtafuta mganga huyo kwa hatua zaidi za kisheria .
Imetolewa na
Ulricho O.Matei-SACP
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.