Kumekuwepo na mfululizo wa matukio ya mauaji yanayoacha shaka kuhusu hali za afya ya akili zaa watu wanaotekeleza mipango hiyo.
Mauaji mengi yameacha simanzi kwa watu kwa kuwa wengi wao walioua, kujiua au waliouwa wazazi wao au wenza wao walionesha dalili ambazo jamii ilizitafsiri kama viashiria vibaya. Bahati mbaya viashiria hivyo hushtukiwa baada ya utekelezaji wa matukio.
Viashiria vingi vinavyojitokeza na kuelezewa huwa ni dalili za magonjwa ya akili. Lakini kwa kuwa jamii haina utambuzi wa kuoanishi dalili hizo na ugonjwa, inapotezea na mwisho wa siku tatizo likiwa sugu husababisha madhara makubwa.
Kama wananchi watapata elimu kuhusu magonjwa yanayoathiri afya ya akili huenda wakanusulu matukio mengi yanayotokea katika jamii.
Jitihadi za haraka zifanyike katika ngazi ya jamii kwa kuwapatia elimu.
Wahusika wote wa visa vya mauaji ya kutatanisha watapelekwa hospitali ya Mirembe ili kufanyiwa uchunguzi wa kuthibitisha hali ya afya ya akili ya watuhumiwa.
Endapo watakutwa na ugonjwa wa akili watapatiwa matibabu na kurudishwa uraiani. Kama utaratibu huu wa matibabu unafanyika ni wakati mwafaka sasa Wataalamu hao wasambae kwenye jamii kwa lengo la kutoa elimu itakayosaidia kung'amua wagonjwa wa akili na kupatiwa matibabu stahiki kabla ya majuto.
Wizara ya mambo ya ndani haitoweza kudhibiti haya mauaji bila kushirikiana na wizara ya afya.