Mauaji ya watu 17 Musoma mwaka 2010

madeinmusoma

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
322
386
Zinapigwa Story mbili kuhusu jambo hili.
Story rasmi na Isiyo rasmi.

Nianze na isiyo rasmi.

2005
Katika mtaa wa MGARANJABO ,wilaya ya MUSOMA walipita vijana watatu kutokea naeneo ya ZANAKI wakiwa wamebeba nyama za NUNGUNUNGU walizotoka kuwinda kwenye vinavyozunguka maeneo yale. KAWAWA KINGUYE akawashuku wale vijana kuwa ni wezi wa mifugo yao inayoibiwa kila mara. Vijana wale wakajitetea kuwa wao sio wezi bali ni wawindaji. Katika kuthibitisha kuwa wao ni wawindaji wakafunguza viroba zao kuonyesha nyama ya Nungunungu waliyopata mawindoni.

KAWAWA KINGUYE hakuamini utetezi wao bali alipandwa na Munkari akapiga MWANO kujulisha wakazi wengine kuwa kuna wezi kwa sauti ya juu. Wakajitokeza kina "mura" wakiwa na mapanga. Ndani ya dakika tano wale vijana wakawa wamechanganyika na nyama waliyowinda. Haikujulikana ipi nyama ya nungunungu na ipi ni nyama za wale vijana watatu. Hata baiskeli wazokuwanazo, haikujulikana ipi ni pedali na ipi ni spoketi. Vijana wale waliuwawa ugenini kinyama kabisa. Wakati wanaendelea kuwakatakata, akatokea jirani wa "mpiga mwano" alishuhudia haya ambaye tutakuja kuona uhusika wake kwenye mkasa huu mbeleni.

Stori Rasmi
Mnamo tarehe 27 October 2005,KAWAWA KANGUYE aliibiwa mbuzi 25 kijijini mwake Mugarabajo,Msoma mjini. Bwana KAWAWA KANGUYE aliwapigia mwano wa wizi vijana watatu ambao walikuwa eneo la tukio. Wananchi wenye hasira wakatoka na kuwaua. Mmoja aliyeuwawa aliitwa FRED MGAYA.

Baada ya tukio hili ndugu wa FRED MGAYA wakajenga chuki na familia ya KAWAWA KANGUYE na walinuia kulipa kisasi dhidi ya familia ya KAWAWA KANGUYE.

Ilipita miaka minne na watu waliamini hali ile imepoa.

Hawakujua....Hawakujua

UZI

MAKABURI KAMA MATUTA

Usiku wa huzuni tarehe 16 February mwaka 2010 ambapo watu 17 waliuwawa kikatili na watu wasiojulikana wenye siraha za kijadi(mapanga na mikuki) walivamia eneo lililokuwa na nyumba tatu za familia moja mtaa wa MGARANJABO eneo la BUHARE wilaya ya MUSOMA.
Nyumba ya kwanza, mali ya KAWAWA KANGUYE KANGUYE iliyokuwa ikikaliwa na watu 10, Waliuwawa watu 8 akiwemo mtoto aliyekadiriwa kuwa na miezi 7 au 8 Nyumba ya pili mali ya MORIS MGAYA,waliuwawa watu 6 na mmoja kujeruhiwa.
Nyumba ya tatu mali ya DORICA MGAYA waliuwawa watu Watatu na sita kuponea chupuchupu.
Ingawa tukio hilo liliacha walionusurika na unyama huo ili kuja "To tell a Tale",Hakuwepo hata mmoja aliyewatambua wauaji.

Tetesi pekee kuhusu wahusika wa mauaji haya ilipatikana kutoka kwenye maelezo ya mtoto mdogo KULWA KAWAWA(mmoja wa wanusurika katika nyumba ya KAWAWA KANGUYE). Binti huyu KULWA alitoa maelezo yake kwa Detective Constable DC JAVILA Kwenye maelezo yake kwa DC JAVILA ,ambaye alikuja kuwa shahidi wa kwanza wa jamuhuri kwenye kesi hii(PW1) Kulwa alieza kuwa, siku ya tukio alimsikia baba yake akimuuliza mmoja wa wauaji "DIWANI MBONA UNANIUA"?

Hata hivyo,Pamoja na maelezo haya,hakuna yeyote aliyemjua "DIWANI


Askari polisi walipofika eneo la tukio, walikubaliana ni kwa matumizi ya mbwa mwenye mafunzo tu, ndipo wataweza kuwabaini wahusika wa unyama ule.
Hivyo aliletwa mbwa mwenye mafunzo(Tracer Dog No. 1495) aliyekuwa akidhibitiwa na STAFF SERGEANT HASHIMU
Mbwa akanusishwa eneo la tukio.


Kisha Mbwa alimwongoza Assistant Superintendent of police ASP KAKOKI (alikuja kuwa shahidi wa tatu PW3) pamoja na askari wengine umbali wa kilomita tano.

Walimfata kwa nyuma mbwa ambaye alipita watu wengi tu mitaani.

Walipofika kijiji cha NYENGINA walikutana na Mwanaume akiendesha baiskeli huku akiwa amempakia mtoto wa kiume.

Mbwa alimrukia mwanaume yule kumaanisha uwepo wake kwenye eneo la tukio.

Mtu huyu alikuja kuwa mtuhumiwa wa pili na jina lake aliitwa ALOYCE NYABASI NYAKUMU aka DIWANI

Kwenye mahojiano aliyofanyiwa na Detective Corporal DCPL OBEID, mtuhumiwa huyu akamtaja JUMA MGAYA(alikuja kuwa mtuuhumiwa wa kwanza)

Kazi ya kumkamata JUMA MGAYA alikabidhiwa Detective sergeant DSGT LAURENT ambapo alibaini JUMA MGAYA amekimbilia SHINYANGA.

Kwa mbinu za kipelelezi JUMA MGAYA alikamatwa SHINYANGA na akasafirishwa kwenda mkoani Mara ambapo ASP KAKOKI(PW3) alimpokea katika kituo cha Police Bunda. Mtuhumiwa huyu JUMA MGAYA wakati wa mahojiano aliwataja NYAKANGA WAMBURA BIRASO(3rd Accused),KUMBATA BURUHAI(7th Accused),SADOKI IKAKA aka NYABUGIMBI NYAKUMU na wengine ambao nao walikamatwa.

Pia JUMA alipopekuliwa nyumbani kwake walikuta panga na mkuki vilivyohusishwa na tukio.


Nyumbani kwa mtuhumiwa NYAKANGA WAMBURA(3rd Accused), baada ya upekuzi uliosimamiwa na ACP NELSON SUMARI(PW7) walikuta Magodoro mawili ya Tanfoam,simu ya Nokia C 1200 na shati la blue vilivyoaminika kuibiwa eneo la tukio. Pia kulifanyika upekuzi nyumbani kwa KUMBATA BURUAI (7th Accused) uliosimamiwa na SSP KIBONA(PW9) ambapo walikuta suruali nyeusi,track suit ya bluu,Jacket na shati la jeupe lenye maandishi "Paradigm" navyo vikihusishwa na eneo la tukio.

Upekuzi kwa watuhumiwa wengine haupata kitu.

Vitu hivi vilivyopatikana kwenye upekuzi vilichukuliwa kama vizibiti.
Vizibiti hivi vilichukuliwa na Assistant Inspector SIMKOKO(PW10) na kupelekwa kwa mkemia wa serikali.

Kwenye ofisi ya mkemia,kazi hii alikabidhiwa GLORIA MACHUMVE(PW23)

GLORIA alifanya FORENSIC DNA PROFILING TEST kwa kulinganisha DNA samples zilizopatikana eneo la tukio,Damu za majeruhi,mate(buccal swabs)ya majeruhi na ndugu zao,Vitu vilivyopatikana kwenye upekuzi wa watuhumiwa,mate na damu za watuhumiwa n.k.

Miaka nane baadae, watuhumiwa 16 kwa pamoja, walisomewa makosa 17 ya mauaji ya watu 17 kinyume cha sheria ya makosa ya jinai namba 196 na 197 sura ya 16 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002.

Kesi hii namba 56 ya mwaka 2018 ilikuwa maarufu kama MAUAJI YA MGARANJABO


Wakati wa kusikilizwa na kuhairishwa kwa kesi hii,watuhumiwa saba walifia mahabusu hivyo kubaki watuhumiwa tisa tu.
Upande ma jamuhuri ulisimamisha mashaidi 23 na vielelezo 44 ambabyo ni vizibiti na nyaraka mbalimbali(maungamo ya kukiri kosa,DNA reports n.k)

Jopo la mawakili wa jamuhuri liliongozwa na WALLACE MAHENGA na YESE TEMBA huku Jopo la mawakili tisa wa utetezi liliongozwa na wakili msomi OSTACK MULIGO.

Katika kesi hii jamhuri ilijenga kesi yake kwa kutoa mlolongo tangu matumizi ya mbwa kumpata mtuhumiwa mmoja hadi mwingine

Ni katika kesi hii tulishuhudia mbwa akiletwa mahakamani kutoa ushaidi jambo ambalo lilizua hoja mbalimbali za kisheria kuwa mbwa hataweza kuhojiwa ushaidi wake

Shaidi wa 23 wa jamuhuri ambaye ndiye alifanya uchunguzi wa mahakama alielezea mahakama matokeo ya uchunguzi wake.
Ni katika kesi hii tulishuhudia mbwa akiletwa mahakamani kutoa ushaidi jambo ambalo lilizua hoja mbalimbali za kisheria kuwa mbwa hataweza kuhojiwa ushaidi wake

Shaidi wa 23 wa jamuhuri ambaye ndiye alifanya uchunguzi wa mahakama alielezea mahakama matokeo ya uchunguzi wake.

Pia alieleza DNA sample za Mkuki na panga vilivyopatikana kwa mshatakiwa wa kwanza JUMA MGAYA zilifanana na samples zilizochukuliwa kwenye nyumba ya MORIS MGAYA.
Upande wa mashtaka ulimaliza kuweka kesi yake mbele ya mheshimiwa Jaji na sasa ukafata upande wa utetezi kuweka hoja mezani.

1. Kuhusu kula njama kutenda kosa, washtakiwa(kasoro ndugu wawili) walikana kabisa kujuana kabla ya tukio bali walijuana rumande wakshtakiwa kwa kesi hiyo.

Kutokana na hili walipinga vikali hoja za upande wa mashtaka kuwa walikuwa na kikao walichopanga awali ili kutekeleza kisasi. Inawezekana vipi kwa watu msiojuana kupanga kikao?

2.Pia walijitetea kwa ALIBI. Alibi ni utetezi unaegamia kukana kuwa eneo la tukio wakati wa tukio. Hapa kila mtuhumiwa alikana kuwa hakuwepo kwenye mji wa MGARANJABHO usiku wa tukio. Wengine walidai walikuwa Bunda, Wengine Mwanza na wengine Sirali siku ya tukio. Yaani kila mtu alijitahidi kutema ndoano

3.Pia walikana hati zao za maungamo(Extra judicial statements) kuwa zilichukuliwa kwa njia ya mateso na kulazimishwa kusaini nyaraka hizo.

4.Pia washtakiwa wawili(wale ndugu) walijitetea wakati wanakamatwa walikuwa MINORS (of the age below majority)

Ndugu hawa walisema haki zao kama watoto zilikiukwa na waliwekwa kwenye kesi sawa na watu wazima.

5.Utetezi ulitoa hoja kukwa kilikuwa kuna udhaifu katika kuweka kumbukumbu za vizibiti. Kizibiti cha godoro kilitajwa na shaidi wa police ni No 44 huku mkemia akikitaja No 29

Katika vizibiti utetezi ulitia shaka uchukuaji wa vizibiti kwani kuna jacket lilichukuliwa kwa kuwa lilikuwa na damu lakini mikuki na mapanga yasiyo na damu nayo yalichukuliwa kama vizibiti

Hoja nyingine ilikuwa utembeaji wa vizibiti toka mtu hadi mtu (CHRONOLOGICAL HANDS) washatakiwa walikana kutambua vizibiti vilivyoletwa mbele ya mahakama wakidai ndio mara ya kwanza wanaviona pale.

Ilijengwa hoja ya IDENTITY kuwa polisi waliwapa washtakiwa majina yasiyo yao. Mfano mshtakiwa wa pili anasema alikamatwa na kuambiwa yeye ndie anaitwa DIWANI wakati halitambui jina hilo.

Kiufupi kesi iliunguruma mpaka na kuna kipindi iliendeshwa kwa mtandao wakati wa janga la Corona. Hukumu ilikuja kutolewa mwezi January mwaka huu ambapo washtakiwa sita walikutwa na hatia na kuhukumiwa Kifo. Watatu waliachiwa baada ya kutotiwa hatiani.

MWISHOView attachment 2132398View attachment 2132399View attachment 2132400
20220226_231523.jpg
 
Wakajitokeza kina "mura" wakiwa na mapanga. Ndani ya dakika tano wale vijana wakawa wamechanganyika na nyama waliyowinda. Haikujulikana ipi nyama ya nungunungu na ipi ni nyama za wale vijana watatu
 
Ila dada zako wanawapenda wanaume wa pande hizo hadi wanatetemeka.
Nilisikia Wanawake wa Kilimanjaro waliaswa na Wazee wao kuwa wasikubali kuolewa na Wakurya, hasa wa Tarime

Ila Wawachune tu lakini Ndoa hapana.

Ni ya kweli haya?
 
Ushahidi wa mbwa uwa una mapungufu sana, hata huko kwa wenzetu kuna scenarios za kesi nyingi ambapo askari anayemwongoza mbwa uwa anamdirect.

Kuna scenario moja huko Marekani, polisi mmoja aliwafungisha watu wengi sana kwa kutumia mbwa baadae ikaja gundulika karibu wote hawakuwa na hatia isipokuwa yeye alikuwa akimwongoza mbwa anavyotaka ili tu apate sifa.

Halafu Tanzania, askari wakishakutuhumu kuwa wewe ndiye mtuhumiwa, aisee utakula kipigo na mateso mpaka ukubali.

Yani wakisema ni wewe basi ni mwendo wa kuteswa mpaka ukubali uwe umefanya au hujafanya.

Utagongwa miguu, misumari, ubanwe mapumbu mpaka ukubali.
 
Back
Top Bottom