Daniel Mjema
Member
- Jul 23, 2007
- 77
- 84
Jeshi la Polisi mkoa Kilimanjaro limesema limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu muhimu waliohusika na mauaji ya mfanyabiashara wa Moshi ,Joseph Maole maarufu kwa jina la Tajiri mtoto aliyeuawa kwa kupigwa risasi Desemba 30,2015 nyumbani kwake eneo la Katanin. Polisi pia wamedai kukamata bunduki aina ya Shortgun Pump Action iliyotumika katika mauaji hayo ikiwa imefichwa katika shimo la choo eneo la Shirimatunda. Bunduki hiyo ndiyo inayodaiwa kutumika kuterrorise wafanyabiashara mkoani Kilimanjaro kwa miezi sita mfululizo.