Mauaji Ya RPC Mwanza, Barlow

Mauaji Ya RPC Mwanza, Barlow

Joined
Apr 2, 2012
Posts
73
Reaction score
59
Wana jamvi habari za asubuhi,

Naomba mwenye updates zozote za mauji ya RPC Mwanza, Barlow au mwenye site ya gazeti la Jamuhuri maana limeandika hiyo habari leo.

will appreciate
 
kinachosemekana jambazi mmoja kajisalimisha police na kueleza habari ilivyokuwa na ameomba ulizi kwa waziri nchimbi
 
Mimi nimesoma Gazeti hili la Jamhuri lakini katika link yao bado hawaja update habari hii, iko ukurasa 2 na 13. Inasisimua sana ukiisoma. Kifupi inasimulia kuwa kuna kijana anayeitwa Mohamed Edward Malele, anasema yeye ni jambazi sugu na ameshiriki katika matukio mengi na anataja tukio moja ambalo hatalisahau kuwa siku moja alikwenda kanisani akamuita mama mmoja, yule mama alivyotoka wakamteka na kwenda kumuua na kunyofoa viungo vyake sehemu za siri, matiti kwa lengo la kishirikina.

Sasa niende kisa cha Barlow, anasema aliipata amri toka kwa polisi, usalama wa taifa na baadhi ya madiwani akamuue Kamanda Barlow anasema kwa kuwa yeye alisha wahi kufanya kazi kwake na anamfahamu alikataa kushiriki kumuua. Anasema walivyoona amekataa wakamsingizia kesi ya ujambazi wa kutumia silaha akaswekwa gerezani. Siku kadhaa baadaye akiwa gerezani alisikia kuwa Kamanda Barlow ameuawa na anasema hakushituka kusikia tukio hilo. Mkuu wa gereza baadaye akaona mashitaka dhidi yake hayakuwa dhahiri kiasi cha kuendelea kumshikilia akaamua kumwachia. Anasema alikataa kuondoka gerezani akiogopa gende la ujambazi huko uraiani litamuua likijua ameachiwa huru. Anadai alipotoka alikwenda moja kwa moja kikosi cha anga cha JWTZ pale uwanja wa ndege Mwanza.

Anadai alipowasimulia wale askari walijaribu kuwasiliana na wabunge kadha bila mafanikio lakini mbunge mmoja aliwaomba wamsafirishe hadi Dodoma. Walimsafirisha hadi Dodoma ili akaonane na ngazi ya juu. Alipofika Dodoma akiwa kwenye lango la Bunge askari walimhoji alikuwa na shida gani, akaanza kuwasimulia yote wakampigia kamanda wa polisi RPC David Misime anye akaamuru aswekwe rumande na arejeshwe Mwanza kuunganishwa na wale watuhumiwa wengine wa mauaji ya Barlow. Taarifa zikafika kwa Pinda naye Pinda akaamuru kijana huyo alindwe ili aweze kutoa picha kamili. Alipowekwa katika hali nzuri kisaikolojia aliweza kueleza ushiriki wa Usalama wa Taifa, Polisi na Madiwani wa CCM na Chadema ambao wako katika genge la majambazi sugu, kuwandio hasa walioshiriki kumuua Kamanda Barlow. Anamtaja mtu mmoja kwa jina moja kuwa ni Muna ambaye anasema huyo inawezekana alishiriki moja kwa moja katika kumuua Barlow. Hadi sasa kijana huyu amepelekwa kusikojulikana kwa ajili ya ulinzi wake ili aweze kufunguka zaidi
 
Sasa Sinema hii Director ni nani? kama ni kova sitoi kiingilio hapo hakuna Movie, itakuwa haijafanyiwa editing muhimu.
 
Mimi nimesoma Gazeti hili la Jamhuri lakini katika link yao bado hawaja update habari hii, iko ukurasa 2 na 13. Inasisimua sana ukiisoma. Kifupi inasimulia kuwa kuna kijana anayeitwa Mohamed Edward Malele, anasema yeye ni jambazi sugu na ameshiriki katika matukio mengi na anataja tukio moja ambalo hatalisahau kuwa siku moja alikwenda kanisani akamuita mama mmoja, yule mama alivyotoka wakamteka na kwenda kumuua na kunyofoa viungo vyake sehemu za siri, matiti kwa lengo la kishirikina.

Sasa niende kisa cha Barlow, anasema aliipata amri toka kwa polisi, usalama wa taifa na baadhi ya madiwani akamuue Kamanda Barlow anasema kwa kuwa yeye alisha wahi kufanya kazi kwake na anamfahamu alikataa kushiriki kumuua. Anasema walivyoona amekataa wakamsingizia kesi ya ujambazi wa kutumia silaha akaswekwa gerezani. Siku kadhaa baadaye akiwa gerezani alisikia kuwa Kamanda Barlow ameuawa na anasema hakushituka kusikia tukio hilo. Mkuu wa gereza baadaye akaona mashitaka dhidi yake hayakuwa dhahiri kiasi cha kuendelea kumshikilia akaamua kumwachia. Anasema alikataa kuondoka gerezani akiogopa gende la ujambazi huko uraiani litamuua likijua ameachiwa huru. Anadai alipotoka alikwenda moja kwa moja kikosi cha anga cha JWTZ pale uwanja wa ndege Mwanza.

Anadai alipowasimulia wale askari walijaribu kuwasiliana na wabunge kadha bila mafanikio lakini mbunge mmoja aliwaomba wamsafirishe hadi Dodoma. Walimsafirisha hadi Dodoma ili akaonane na ngazi ya juu. Alipofika Dodoma akiwa kwenye lango la Bunge askari walimhoji alikuwa na shida gani, akaanza kuwasimulia yote wakampigia kamanda wa polisi RPC David Misime anye akaamuru aswekwe rumande na arejeshwe Mwanza kuunganishwa na wale watuhumiwa wengine wa mauaji ya Barlow. Taarifa zikafika kwa Pinda naye Pinda akaamuru kijana huyo alindwe ili aweze kutoa picha kamili. Alipowekwa katika hali nzuri kisaikolojia aliweza kueleza ushiriki wa
Usalama wa Taifa, Polisi na Madiwani wa CCM na Chadema ambao wako katika genge la majambazi sugu, kuwandio hasa walioshiriki kumuua Kamanda Barlow. Anamtaja mtu mmoja kwa jina moja kuwa ni Muna ambaye anasema huyo inawezekana alishiriki moja kwa moja katika kumuua Barlow. Hadi sasa kijana huyu amepelekwa kusikojulikana kwa ajili ya ulinzi wake ili aweze kufunguka zaidi

Duh hii ni kali kwelikweli!!! Yaleyale aliyosema Sugu bungeni!! Bold ya blue
 
Wamempima akili? Mkuu wa Gereza anaweza kuamru mtu aachiwe?

Watendaji wengi wa serikali na vyombo vya dola wanafanya kazi kwa vi-memo toka kwa viongozi wa CCM; kama hujui hilo fanya uchunguzi.
 
Wamempima akili? Mkuu wa Gereza anaweza kuamru mtu aachiwe?

"Mjumbe hauawi" nimeandika kile ninachokikumbuka baada ya kusoma hiki kijigazeti nikiwa katika mshangao hivyo hivyo kama wewe Mkuu wangu. Nikajiuliza je kwa kuwa alikuwa katika tuhuma bila mashtaka ya msingi au naye Mkuu wa gereza alipata amri toka kwa wakuu wake amwachie!! Ni maswali ambayo majibu yake inabidi uyajibu mwenyewe wee acha tu. Shukrani kwa kuliona hilo.
 
wamempeleka wapi sasa.?

kuna hatari ndugu zake wasilione hata kaburi lake!!!
 
Back
Top Bottom