Mimi nimesoma Gazeti hili la Jamhuri lakini katika link yao bado hawaja update habari hii, iko ukurasa 2 na 13. Inasisimua sana ukiisoma. Kifupi inasimulia kuwa kuna kijana anayeitwa Mohamed Edward Malele, anasema yeye ni jambazi sugu na ameshiriki katika matukio mengi na anataja tukio moja ambalo hatalisahau kuwa siku moja alikwenda kanisani akamuita mama mmoja, yule mama alivyotoka wakamteka na kwenda kumuua na kunyofoa viungo vyake sehemu za siri, matiti kwa lengo la kishirikina.
Sasa niende kisa cha Barlow, anasema aliipata amri toka kwa polisi, usalama wa taifa na baadhi ya madiwani akamuue Kamanda Barlow anasema kwa kuwa yeye alisha wahi kufanya kazi kwake na anamfahamu alikataa kushiriki kumuua. Anasema walivyoona amekataa wakamsingizia kesi ya ujambazi wa kutumia silaha akaswekwa gerezani. Siku kadhaa baadaye akiwa gerezani alisikia kuwa Kamanda Barlow ameuawa na anasema hakushituka kusikia tukio hilo. Mkuu wa gereza baadaye akaona mashitaka dhidi yake hayakuwa dhahiri kiasi cha kuendelea kumshikilia akaamua kumwachia. Anasema alikataa kuondoka gerezani akiogopa gende la ujambazi huko uraiani litamuua likijua ameachiwa huru. Anadai alipotoka alikwenda moja kwa moja kikosi cha anga cha JWTZ pale uwanja wa ndege Mwanza.
Anadai alipowasimulia wale askari walijaribu kuwasiliana na wabunge kadha bila mafanikio lakini mbunge mmoja aliwaomba wamsafirishe hadi Dodoma. Walimsafirisha hadi Dodoma ili akaonane na ngazi ya juu. Alipofika Dodoma akiwa kwenye lango la Bunge askari walimhoji alikuwa na shida gani, akaanza kuwasimulia yote wakampigia kamanda wa polisi RPC David Misime anye akaamuru aswekwe rumande na arejeshwe Mwanza kuunganishwa na wale watuhumiwa wengine wa mauaji ya Barlow. Taarifa zikafika kwa Pinda naye Pinda akaamuru kijana huyo alindwe ili aweze kutoa picha kamili. Alipowekwa katika hali nzuri kisaikolojia aliweza kueleza ushiriki wa Usalama wa Taifa, Polisi na Madiwani wa CCM na Chadema ambao wako katika genge la majambazi sugu, kuwandio hasa walioshiriki kumuua Kamanda Barlow. Anamtaja mtu mmoja kwa jina moja kuwa ni Muna ambaye anasema huyo inawezekana alishiriki moja kwa moja katika kumuua Barlow. Hadi sasa kijana huyu amepelekwa kusikojulikana kwa ajili ya ulinzi wake ili aweze kufunguka zaidi