Mauaji ya mtoto wangu

Mauaji ya mtoto wangu

Afrikaaaa....yani wameon awadai kwanza milioni ili wazike...zaidi upuuzi wa hali ya juu.....inhumanity ....huyo p[olisi wao kakuweka ndani ili iweje..shida nyingine..upande wa uchunguzi taaluma imezingatiwa....sasa kingine mtoto kazaliwa tu unaletewa wakati anahitaji anyonye ziwa la mama...ni kama wamekasirika wakakusuia......pia hawajielewi....kama hadi mtu wa karibu anasema huyo mama mchawi n amazingira yale basi ni mshirikina..ila sasa isue ku prove mahakamni....etc...ila dah bya duniani mengi ya binadamu mengi
 
Salaam wakuu, habari za jioni.

Nimekaa nikatafakari nikaona nilete kisa changu hapa jukwaani ili tuwe makini na binadamu, japo mimi nimebaki sina mtoto tena, itawafaa hata wazazi wengine wenye watoto hasa wadogo.

Mwaka 2015 nilikuwa Dodoma nikifanya shughuli zangu za kujitafutia ridhiki, nilikuwa kwenye mahusiano na binti fulani, ambayo yalipelekea binti kubeba ujauzito wangu, aliponiambia sikukataa nilikubali kuwa tutalea, basi tukaanza utaratibu wa kulea mimba.

Tarehe 25.12.2015

Niliwasiliana na wazazi wa pande zote mbili, wa kwangu na wa binti kuhusiana na suala la ujauzito, kwa lengo la kuwashirikisha isije kutokea suala lolote wakiwa hawafahamu, basi tukaweka makubaliano kuwa binti atalea mimba akiwa upande wa wazazi wake akatoka Dodoma kwenda Dar es salaam.

Tarehe 10.8.2016

Niliamua kurudi shule kuongeza elimu jijini Mwanza katika chuo kimoja cha afya huku nikiendeleza mawasiliano na mzazi mwenzangu.

Tarehe 06.09.2016

Nilipokea simu kutoka kwa mpenzi wangu kuwa amefanikiwa kujifungua mtoto wa kiume, basi nikamuita jina mtoto na maisha yakaendelea.

Tarehe 26.9.2016

Nilipigiwa simu na baba wa mzazi mwenzangu kuwa nifanye utaratibu nichukue mtoto wangu, wao wanataka kusomesha binti yao hapo ni siku 20 tu baada ya kujifungua, nilisita ila niliamua kuchukua uamuzi wa kukubali, ilibidi niwasiliane na dada yangu ambaye ni shangazi wa mtoto wangu, nilimsihinsana anilele mtoto wangu, hatimaye alikubali. Nikafanya utaratibu wa kumsafirisha mwanangu na mama yake mpaka Mwanza, nilikabidhiwa mtoto na mama wa mtoto akarudi kwao, malezi yalianza pole pole mtoto akiwa kwa dada yangu, nikawa natoa kidogo nilichopata kwa ajili ya mwanangu.

Tarehe 3.06.2018

Saa 2:30 Mchana

Nikiwa chuoni nilipokea simu kutoka kwa dada yangu kuwa mtoto haonekani, ikabidi niwaambie watafute maeneo yote ya jirani, japo sio kawaida yake kuzurura mpaka kufikia Saa kumi jioni ndio alitokea mama mmoja akisema kuwa ameona mtoto anaelea shimo la choo nyumba ya jirani akiwa ameshakufa.

Nilitoka chuoni na kwenda nyumbani nilipofika nilikuta polisi wameshatoa mwili na kuupeleka hospitalini kuuhifadhi, tukio lilivyokuwa na mambo yote yaliyoendelea ndio nikasimuliwa kuwa mtoto alikuwa akicheza na wenzake ambao ni wadogo zangu, ila ghafla walipowaita kwa ajili ya chakula cha mchana yeye hakuonekana.

MAZINGIRA YA KIFO CHA MTOTO.

Baada ya kutolewa shimoni polisi walifanya uchunguzi wa haraka, tumbo la mtoto lilikuwa limenyooka kawaida na wala hakuwa amemeza maji, kitu kilichoshangaza wengi. Pili lile shimo huwa limefunikwa kwa kutumia mfuniko mzito wa zege ila siku hiyo ulikutwa pembeni na mtoto yumo ndani anaelea.

Ikiwa ni makaridio ya nusu saa baada ya kutoweka nyumbani katika namna ya kutatanisha. Zilionekana alama puani na shingoni zenye rangi nyekundu zikiashiria vidonda fulani, maana mtoto alikuwa na rangi nyeupe. Maandalizi ya msiba yalifanyika.

Tuliazimia kufanya uchunguzi wa maiti kujua kama mtoto amekufa maji kweli ama ameuawa ndipo akatupwa shimoni. Asubuhi tuliamkia polisi kwa ajili ya kwenda polisi na mahakamani kwa ajili ya kupata kibali cha kufanya uchunguzi wa kidaktari kwa mtoto wangu.

HALI YA KUSHANGAZA.

Baada ya kufika polisi muda mchache baadae alifika yule mwanamama aliyesema kuwa amemuona mtoto shimoni amekufa, ikumbukwe kuwa huyu mama usiku ule wa msiba kuamkia siku hii tuliyokuja polisi hakuwepo msibani, na vijana wa mtaa waliokuwepo kwenye msiba usiku huo walionekana kumtaja kwenye hili suala.

Alifika polisi kwa usafiri wa piki piki, baada ya sisi kupata kibali tulianza kuelekea mahakama kwa ajili ya kumalizia taratibu, ndipo yule mama akasema na yeye anataka kwenda na sisi mpaka mortuary, nikapata wasiwasi maana yule mama nilishasikia anatuhumiwa na mambo ya kishirikina, nikamgomea kwenda nae ila watu wazima wakaniambia nimuache.

Tulipofika mahakama tukafanya taratibu zote, nilishindwa kujizuia nikamzuia yule mwanamke asipande kwenye gari, maana nilihisi amehusika na kifo cha mwanangu na anataka kwenda kumalizia mambo yake huko mortuary kwa mwanangu, basi tukawa tumemuacha, moja kwa moja safari ya kuelekea sekou toure ikaanza.

RIPOTI YA UCHUNGUZI WA KIDAKTARI.

Baada ya kufika maiti ya mtoto wangu ilivutwa kutoka kwenye jokofu nilihamaki baada ya kuona alama nyeusi puani na shingoni, ikioneshwa mtu aliyekwaruzwa na kucha, nikanyamaza na kuacha ripoti ya daktari itoke.

Ripoti ilipokuja ni kuwa marehemu aliuwawa kwa kukosa hewa (suffocation) na sio kwa kunywa maji (Drowning) maana mapafu yalipowekwa kwenye maji hayakuzama yalielea tu. Alifanyiwa upasuaji, mimi nikiwa shuhuda na mapafu ya mtoto hayakuonesha kuwa alimeza maji hata kidogo, daktari alitukabidhi ripoti safari ya kurudi nyumbani kwenye msiba ikaanza.

CHANGAMOTO.

Baada ya kurudi tulikuta ndugu upande wa mwanamke wameshafika, nilipewa taarifa na ndugu zangu kuwa walipofika wakapewa chakula walifyonza na kukisukuma pembeni. Sikujali sana hilo, tukawaelezea jambo zima lilivyokwenda na ripoti ya madaktari ilivyo, basi wakaelewa ila wakatoa sharti la kwamba wanataka pesa Taslim Shilingi Milioni Moja, bila hivyo hatuziki, ilinishangaza sana, pesa ya kulipia nini? ikabidi niwaombe wawe na subira tumalize mazishi ya mtoto wangu hayo mambo tutayaongea baadae.

KUKAMATWA NA POLISI.

Wakakasirika wakaondoka baada ya muda waliita polisi ambaye ni ndugu yao nikakamatwa mimi na mfanyakazi wa ndani njiani tulipoondoka alikamatwa na yule mwanamke aliyetufuata polisi mpaka mahakamani.

Nikakamatwa na kuwekwa mahabusu kwa sharti ya kwamba nilipe ile pesa niliyokuwa nimeambiwa, nikalala siku mbili mahabusu siku ya tatu niliomba mawasiliano nao na kuwaomba niwatangulizie laki mbili ili nizike mtoto wangu maana msiba ulikuwa umesimama.

Basi pesa ilitolewa laki 2 nikabaki nadaiwa laki 8 nikatolewa nikashiriki mazishi, ambapo mpaka sasa ninadaiwa hiyo laki nane ambayo hata sielewi ni pesa ya nini, ina maana ni kama ninalipia marehemu mtoto wangu aliyeko kaburini, na sio kwamba nikiwa nimeoa binti yao binti nilikuja kusikia hata chuo hakwenda alikuwa tu mtaani, huku mimi nikiwa nimekabidhiwa mtoto wa siku 20.

Isingekuwa mimi kukamatwa na ndugu yao askari nisingetoa chochote ila nililazimika kuwalipa ili nitoke maana mazishi yalishindwa kuendelea huko nyumbani, isingeleta picha nzuri mimi kama baba wa mtoto kutoonekana, maana hata mama yake pia yeye hakuja kwenye mazishi.

Mimi na dda wa kazi tulitoka ila yule mama niliyekuwa ninamshuku yupo mahabusu mpaka sasa.

Nilimshukuru Mungu kwa kushiriki kusindikiza mwanangu salama, nilimpenda sana ila ameshakwenda, mpaka leo ninapata ugumu wa kusema kuwa ni mipango ya Mungu ilihali ninaiona mikono ya shetani katika mwili wa Mwanangu.

Alikuwa ni mwanangu wa pekee, mrithi wangu, ila ninaamini aliyemuondoa akiwa na mwaka mmoja na miezi 9 ilihali hata kuongea bado alijuwa hajajua kusema alimtukana au kumkosea, na yeye atalipwa duniani hapa hapa, ninaweza kulipiza ila nitamkosea Mwenyezi mungu.

Baada ya mazishi kwisha nikarudi masomoni ila niliendelea kupokea taarifa za uchunguzi kutoka kwa polisi, mpelelezi aliniambiwa kuwa kuna mtu aligoma kutajwa jina alimuona mwanamke huyo maeneo ya getini na mwanangu, halafu pia mume wa zamani wa yule mama aliwatafuta askari na kuwaambia kuwa mwanamke yule ana tabia za kishirikina ananyonga watoto na kukausha damu, na kwao walipowapigia walikataa kumsaidia maana wameshamchoka, ndio sababu ya kuwa ndani mpaka sasa hivi.

Jamani tuwe makini zaidi kuna watu wenye nia ovu juu ya watoto wetu.

Jioni njema.
RIP young boy, Mungu atakulipia ndugu, pole sana!
 
Mchawi no 1 ni Mzazi mwenzio? Mtoto wa siku 20? Hii inaingiaje akilini? Hata angeenda kusoma anaacha mtoto?

Hivi Mungu anasubiri nini kuadhibu watu kama hawa? Watu hatujazaa tunalea watoto wa watu kwa upendo Leo huyu mshenzy anamtelekeza mtoto kijinga? Hii imeniuma sana uchungu wa mtoto aujuae sio mama
 
aisee!ngumu kusahau!muangalie na wanawake wa kuzaa nao!we kitoto kina siku 20 umekomaza msuli kukiachisha jamani !arggggh!pole sana
kaka
nimeumia mno
 
Mchawi no 1 ni Mzazi mwenzio? Mtoto wa siku 20? Hii inaingiaje akilini? Hata angeenda kusoma anaacha mtoto?

Hivi Mungu anasubiri mini kuadhibu watu kama hawa? Watu hatujazaa tunalea watoto wa watu kwa upendo Leo huyu mshenzy anamtelekeza mtoto kijinga? Hii imeniuma sana uchungu wa mtoto aujuae sio mama

sema wew3e!sijui wengine labour hawapatagi uchungu?
 
Mkasa unasisimua balaaa...!!!
Hadi nakosa chakusema.
But all in all pole kwa maswaibu
 
Salaam wakuu, habari za jioni.

Nimekaa nikatafakari nikaona nilete kisa changu hapa jukwaani ili tuwe makini na binadamu, japo mimi nimebaki sina mtoto tena, itawafaa hata wazazi wengine wenye watoto hasa wadogo.

Mwaka 2015 nilikuwa Dodoma nikifanya shughuli zangu za kujitafutia ridhiki, nilikuwa kwenye mahusiano na binti fulani, ambayo yalipelekea binti kubeba ujauzito wangu, aliponiambia sikukataa nilikubali kuwa tutalea, basi tukaanza utaratibu wa kulea mimba.

Tarehe 25.12.2015

Niliwasiliana na wazazi wa pande zote mbili, wa kwangu na wa binti kuhusiana na suala la ujauzito, kwa lengo la kuwashirikisha isije kutokea suala lolote wakiwa hawafahamu, basi tukaweka makubaliano kuwa binti atalea mimba akiwa upande wa wazazi wake akatoka Dodoma kwenda Dar es salaam.

Tarehe 10.8.2016

Niliamua kurudi shule kuongeza elimu jijini Mwanza katika chuo kimoja cha afya huku nikiendeleza mawasiliano na mzazi mwenzangu.

Tarehe 06.09.2016

Nilipokea simu kutoka kwa mpenzi wangu kuwa amefanikiwa kujifungua mtoto wa kiume, basi nikamuita jina mtoto na maisha yakaendelea.

Tarehe 26.9.2016

Nilipigiwa simu na baba wa mzazi mwenzangu kuwa nifanye utaratibu nichukue mtoto wangu, wao wanataka kusomesha binti yao hapo ni siku 20 tu baada ya kujifungua, nilisita ila niliamua kuchukua uamuzi wa kukubali, ilibidi niwasiliane na dada yangu ambaye ni shangazi wa mtoto wangu, nilimsihinsana anilele mtoto wangu, hatimaye alikubali. Nikafanya utaratibu wa kumsafirisha mwanangu na mama yake mpaka Mwanza, nilikabidhiwa mtoto na mama wa mtoto akarudi kwao, malezi yalianza pole pole mtoto akiwa kwa dada yangu, nikawa natoa kidogo nilichopata kwa ajili ya mwanangu.

Tarehe 3.06.2018

Saa 2:30 Mchana

Nikiwa chuoni nilipokea simu kutoka kwa dada yangu kuwa mtoto haonekani, ikabidi niwaambie watafute maeneo yote ya jirani, japo sio kawaida yake kuzurura mpaka kufikia Saa kumi jioni ndio alitokea mama mmoja akisema kuwa ameona mtoto anaelea shimo la choo nyumba ya jirani akiwa ameshakufa.

Nilitoka chuoni na kwenda nyumbani nilipofika nilikuta polisi wameshatoa mwili na kuupeleka hospitalini kuuhifadhi, tukio lilivyokuwa na mambo yote yaliyoendelea ndio nikasimuliwa kuwa mtoto alikuwa akicheza na wenzake ambao ni wadogo zangu, ila ghafla walipowaita kwa ajili ya chakula cha mchana yeye hakuonekana.

MAZINGIRA YA KIFO CHA MTOTO.

Baada ya kutolewa shimoni polisi walifanya uchunguzi wa haraka, tumbo la mtoto lilikuwa limenyooka kawaida na wala hakuwa amemeza maji, kitu kilichoshangaza wengi. Pili lile shimo huwa limefunikwa kwa kutumia mfuniko mzito wa zege ila siku hiyo ulikutwa pembeni na mtoto yumo ndani anaelea.

Ikiwa ni makaridio ya nusu saa baada ya kutoweka nyumbani katika namna ya kutatanisha. Zilionekana alama puani na shingoni zenye rangi nyekundu zikiashiria vidonda fulani, maana mtoto alikuwa na rangi nyeupe. Maandalizi ya msiba yalifanyika.

Tuliazimia kufanya uchunguzi wa maiti kujua kama mtoto amekufa maji kweli ama ameuawa ndipo akatupwa shimoni. Asubuhi tuliamkia polisi kwa ajili ya kwenda polisi na mahakamani kwa ajili ya kupata kibali cha kufanya uchunguzi wa kidaktari kwa mtoto wangu.

HALI YA KUSHANGAZA.

Baada ya kufika polisi muda mchache baadae alifika yule mwanamama aliyesema kuwa amemuona mtoto shimoni amekufa, ikumbukwe kuwa huyu mama usiku ule wa msiba kuamkia siku hii tuliyokuja polisi hakuwepo msibani, na vijana wa mtaa waliokuwepo kwenye msiba usiku huo walionekana kumtaja kwenye hili suala.

Alifika polisi kwa usafiri wa piki piki, baada ya sisi kupata kibali tulianza kuelekea mahakama kwa ajili ya kumalizia taratibu, ndipo yule mama akasema na yeye anataka kwenda na sisi mpaka mortuary, nikapata wasiwasi maana yule mama nilishasikia anatuhumiwa na mambo ya kishirikina, nikamgomea kwenda nae ila watu wazima wakaniambia nimuache.

Tulipofika mahakama tukafanya taratibu zote, nilishindwa kujizuia nikamzuia yule mwanamke asipande kwenye gari, maana nilihisi amehusika na kifo cha mwanangu na anataka kwenda kumalizia mambo yake huko mortuary kwa mwanangu, basi tukawa tumemuacha, moja kwa moja safari ya kuelekea sekou toure ikaanza.

RIPOTI YA UCHUNGUZI WA KIDAKTARI.

Baada ya kufika maiti ya mtoto wangu ilivutwa kutoka kwenye jokofu nilihamaki baada ya kuona alama nyeusi puani na shingoni, ikioneshwa mtu aliyekwaruzwa na kucha, nikanyamaza na kuacha ripoti ya daktari itoke.

Ripoti ilipokuja ni kuwa marehemu aliuwawa kwa kukosa hewa (suffocation) na sio kwa kunywa maji (Drowning) maana mapafu yalipowekwa kwenye maji hayakuzama yalielea tu. Alifanyiwa upasuaji, mimi nikiwa shuhuda na mapafu ya mtoto hayakuonesha kuwa alimeza maji hata kidogo, daktari alitukabidhi ripoti safari ya kurudi nyumbani kwenye msiba ikaanza.

CHANGAMOTO.

Baada ya kurudi tulikuta ndugu upande wa mwanamke wameshafika, nilipewa taarifa na ndugu zangu kuwa walipofika wakapewa chakula walifyonza na kukisukuma pembeni. Sikujali sana hilo, tukawaelezea jambo zima lilivyokwenda na ripoti ya madaktari ilivyo, basi wakaelewa ila wakatoa sharti la kwamba wanataka pesa Taslim Shilingi Milioni Moja, bila hivyo hatuziki, ilinishangaza sana, pesa ya kulipia nini? ikabidi niwaombe wawe na subira tumalize mazishi ya mtoto wangu hayo mambo tutayaongea baadae.

KUKAMATWA NA POLISI.

Wakakasirika wakaondoka baada ya muda waliita polisi ambaye ni ndugu yao nikakamatwa mimi na mfanyakazi wa ndani njiani tulipoondoka alikamatwa na yule mwanamke aliyetufuata polisi mpaka mahakamani.

Nikakamatwa na kuwekwa mahabusu kwa sharti ya kwamba nilipe ile pesa niliyokuwa nimeambiwa, nikalala siku mbili mahabusu siku ya tatu niliomba mawasiliano nao na kuwaomba niwatangulizie laki mbili ili nizike mtoto wangu maana msiba ulikuwa umesimama.

Basi pesa ilitolewa laki 2 nikabaki nadaiwa laki 8 nikatolewa nikashiriki mazishi, ambapo mpaka sasa ninadaiwa hiyo laki nane ambayo hata sielewi ni pesa ya nini, ina maana ni kama ninalipia marehemu mtoto wangu aliyeko kaburini, na sio kwamba nikiwa nimeoa binti yao binti nilikuja kusikia hata chuo hakwenda alikuwa tu mtaani, huku mimi nikiwa nimekabidhiwa mtoto wa siku 20.

Isingekuwa mimi kukamatwa na ndugu yao askari nisingetoa chochote ila nililazimika kuwalipa ili nitoke maana mazishi yalishindwa kuendelea huko nyumbani, isingeleta picha nzuri mimi kama baba wa mtoto kutoonekana, maana hata mama yake pia yeye hakuja kwenye mazishi.

Mimi na dda wa kazi tulitoka ila yule mama niliyekuwa ninamshuku yupo mahabusu mpaka sasa.

Nilimshukuru Mungu kwa kushiriki kusindikiza mwanangu salama, nilimpenda sana ila ameshakwenda, mpaka leo ninapata ugumu wa kusema kuwa ni mipango ya Mungu ilihali ninaiona mikono ya shetani katika mwili wa Mwanangu.

Alikuwa ni mwanangu wa pekee, mrithi wangu, ila ninaamini aliyemuondoa akiwa na mwaka mmoja na miezi 9 ilihali hata kuongea bado alijuwa hajajua kusema alimtukana au kumkosea, na yeye atalipwa duniani hapa hapa, ninaweza kulipiza ila nitamkosea Mwenyezi mungu.

Baada ya mazishi kwisha nikarudi masomoni ila niliendelea kupokea taarifa za uchunguzi kutoka kwa polisi, mpelelezi aliniambiwa kuwa kuna mtu aligoma kutajwa jina alimuona mwanamke huyo maeneo ya getini na mwanangu, halafu pia mume wa zamani wa yule mama aliwatafuta askari na kuwaambia kuwa mwanamke yule ana tabia za kishirikina ananyonga watoto na kukausha damu, na kwao walipowapigia walikataa kumsaidia maana wameshamchoka, ndio sababu ya kuwa ndani mpaka sasa hivi.

Jamani tuwe makini zaidi kuna watu wenye nia ovu juu ya watoto wetu.

Jioni njema.
Pole sana mkuu,muachie Mungu yeye ndiye mlipaji
 
Back
Top Bottom