Mauaji ya kutisha ya wanawake Wilayani Misungwi

Mauaji ya kutisha ya wanawake Wilayani Misungwi

mmh

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Posts
2,906
Reaction score
5,085
Kwa muda sasa wilaya ya Misungwi kumeibuka mauaji ya kutisha sana.

Wanawake wakiwa mashambani wanakamatwa wanafanyiwa vitendo vya kudhalilishwa kisha wanauliwa na kuchukuliwa viungo vyao vya siri.

Na kuna baadhi ya vijiji pia wanaume nao wanauliwa hivo. Lakini hasa wanawake ndo wanafanyiwa hivo.

Huu ni msimu wa kilimo kwa hiyo hali imekuwa tete sana, kwa sababu kaya zikiwa zinahangaika katika kutafuta vipato kupitia kilimo zinakutwa na madhira hayo. Sasa imefikia hatua ili mwanamke akalime lazima awe na mlinzi wa kiume.

Pia hata wasichana na watoto wa kike wakiwa wanaenda au kutoka shule, kuchunga ng'ombe, kutumwa kazi mbalimbali mambo hayo yanawakuta.

Watu washareport lakini kinachoendelea kimya! Msangi mbona Mbeya ulifanya kazi nzuri sana vipi Mwanza.

Vijiji vya Kijima, Ikoma, Misasi, Mwabuki, Buhingo, Seke, Nkanziga, Nduha, yani vyote mpaka Kolomije ni hatari!

Wito kwa serikali.
Mnaombwa sana mshughulikie hali hii kwa haraka. Maana kutatokea njaa msimu ujao kama wananchi hawatakuwa salama.

Viongozi wakuu kwa maana ya Waziri Mkuu yuko Mwanza tunaomba afahamu hilo na alifuatilie maana wahusika wanaweza funika kombe. Na wananchi wa kule huwaga sio shouter kabisa so wanaweza hata wasireact kwa PM.
 
Duh. Hiv mwanzaa kuna nini. Watu wanauliwa ovyo na sababu kubwa itakuwa imani za kishirikina kama sio biashara ya viungo.

Figo sasa bei ipo juu nasikia had m300.
 
Wasukuma na Wanyakyusa ni makabila yanayoongoza kwa ushirikina nchi hii. Huko wanaongoza kwa kuua vikongwe na albino na cha kutisha siyo kwa sababu hawana elimu ila inaonekana ni "part and parcel" ya utamaduni wao. Makabila mengine kama wafipa unaweza ukasema pengine ni ukosefu wa elimu lakini siyo haya makabila mawili.
Niliwahi kumwuuliza rafiki yangu mmoja pale Kalemela ( tena ni mwalimu wa Physics na Mathematics high school) kama hawa vikongwe ni wachawi kweli akanijibu bila kupepesa macho kuwa kuna ukweli katika tuhuma hizo. Sasa huyo ni msomi je hao wengine si ni balaa tu?
Kuna wakati jamii ilikubaliana "by implication" kwamba hawa watu wawe watumishi na wafanyakazi tu kwenye jamii ya kitanzania lakini wasiwe viongozi kwani busara ilitamalaki kwamba msukuma hata akielimika ushirikina hauodonki kichwani mwake na ataangalia pembeni hata kama anajua unaleta madhara. Kwa mantiki hiyo Mauaji haya mikoa ya Mwanza na Shinyanga ngumu kuisha kwa kuwategemea akina Paskali Mayala wayakomeshe, kwa kuwa "wasomi wa kisukuma" nao ni washirikana sana.

cc Pasco
 
Back
Top Bottom