Mtu mmoja asiyefahamika anatafutwa kwa tuhuma za mauaji Mjini Tarime, mtu huyo ambaye anafanya matukio ya ajabu ya mauaji leo majira saa nne asubuhi amewaua watu wanne katika Kijiji cha Kemakorere. Anafanya mauaji hayo kwa kutumia Bunduki, inasemekana mtu huyo akishaua hachukui kitu chochote bali huua na kutokomea kusikojulikana.
Mtu huyo haijajulikana kama ni mwanamke ama mwanaume kwa kuwa hajapatikana mpaka sasa.
Kamanda wa Polisi Mjini Tarime amethibitisha uwepo wa muuaji na mauaji hayo ambapo watu takriban saba wameshauwawa mpaka sasa.
Mji wa Tarime umejaa taharuki watu hawana amani...
Jeshi la Polisi linahaha mpaka sasa, kwani linafanya msako wa kufa na kupona kumpata mtu huyo....
Source: Morning Star Radio
Nasikia ni watu wanne hali inatisha kwa kweli.
Kama mpaka idadi mnaijua kitu gani kinawashinda(vyombo vya usalama) kuwakamata.
Jamani kumejitokeza Mtu/ kikundi cha watu Wilayani Tarime kinachoua watu katika hali ya kusshtua na kushangaza sana, mimi binafsi nina taarifa za watu wawili waliouwawa jana na hao wauaji, jambo la kustikitisha ni kwamba wauaji hao tangu wameanza kuua yapata wiki moja sasa bado hawajakamatwa na hivyo kuwafanya wananchi kuwa na hofu kubwa na usalama wao.
Ni wito wangu kwa Jeshi la polisi kuongeza nguvu ya askari wenye utaalamu na Ujasiri kwasababu hali hii sasa inatisha kweli kweli..Polisi wa kanda maalum inaonekana bado hawajaweza kupata ufumbuzi wa mauaji haya...
Kwani kujua idadi ya waliouwawa inasaidiaje kuwakamata wauwaji, au we umeelewaje maana waliouwawa hadi hivi sasa wamefikia wanne.Kama mpaka idadi mnaijua kitu gani kinawashinda(vyombo vya usalama) kuwakamata.
Nani anamjua mchawi bwana, uchawi haundoki ila njia ya Mungu tu.kisa cha mauaji ni nini? kama watakuwa wanawaua wachawi acheni waendelee na kazi sasa uchawi tanzania umekithiri kuna haja ya kutafutiwa ufumbuzi.
Mtu aliyedaiwa kuwa ni kichaa auwa watu nane huko Tarime,Mara
Mtu mmoja ambaye hajulikana jina lake anayesadikiwa kuwa ni kichaa huko Wilayani Tarime mkoani Mara anamiliki silaha adaiwa kuuwa watu nane mpaka sasa polisi wazibitisha.source clouds radio
Heading ya uongo content ni ukweli hata mimi nimeipata toka tarime.Mtu aliyedaiwa kuwa ni kichaa auwa watu nane huko Tarime,Mara
Mtu mmoja ambaye hajulikana jina lake anayesadikiwa kuwa ni kichaa huko Wilayani Tarime mkoani Mara anamiliki silaha adaiwa kuuwa watu nane mpaka sasa polisi wazibitisha.source clouds radio
Habari zingine utata kweli, hivi kichaa anaruhusiwa kumiliki silaha kama bunduki!
Heading ni Geita na humu ndani ndo hivyo. Tulia na uandike vizuri ili ueleweka mkuu.