Mauaji ya kinyama ya Waislam BURMA

Status
Not open for further replies.

DON KILLUMINATI

Senior Member
Jan 2, 2011
193
83
Kwa masikitiko Makubwa Ulimwengu umeshuhudia mauaji ya waumini wa dini ya Kiislam yaliyofanywa na Buddhists nchini BURMA, lakini jambo la kusikitisha ni kwamba habari hii haijapewa uzito wowote katika vyombo vya habari vya kimataifa na wala hata UN haijahangaika kuhakikisha mauaji hayo yanakoma.





NOTE:

GUYS I AM A DEVOTED CHRISTIAN. DINI YANGU HAIRUHUSU MAUAJI YA NAMNA YOYOTE ILE, IWE NI KWA MKRISTO WALA KWA MUISLAM, WALA KWA DINI YOYOTE. NASHANGAA WANA JF WANAONISHAMBULIA KWA KUSEMA KWAMBA "SISI" WAISLAM TUMEZOEA KULALAMIKA.

KWA KIFUPI SIWAOMBEI MABAYA WAISLAM KWA SABABU NAO NI WANADAM, NA WAPO WAISLAM AMBAO WANABADILI DINI NA KUWA WAUMINI WAZURI WA KRISTO KULIKO WEWE UNAYEWAPONDA.

READ MY SIGNATURE BELOW .............
 
Last edited by a moderator:
Kazi ya un ni kutangaza mauaji ya waislamu ndugu?dont show your true color
 
Ulitaka UN wafanye nini? Kwani kazi ya UN ni kutetea uislamu?...........Mwambieni Ponda akawatetee huko Burma, si ndie mtetezi wenu
 
Sisi Tunachoweza Kusema na Kuhuzunika ni Watu Dhalimu wametoa roho za Watu wasiokuwa na Hatia!! Sasa Huku kusema waisalam!! Ndio Kutia msisitizo? au ni roho special Tofauti na mauaji Mengine?
 
Dah inasikitisha; hakuna mwanadamu mwenye haki ya kutoa uhai wa mwanadamu mwenzake. Sote lazima tukemee ukatili unaofanywa na mwanadamu dhidi ya mwanadamu mwenzake maana hauna uhalali kwa sababu yoyote ile!
 
Kule Syria ndio kuna mauwaji ya kinyama zaidi Bashar Al Assad anaendelea kuuwa waislamu wenzake kwa dozens kila mpaka leo jumuiya ya kiarabu wameitenga Syria. Kwahiyo UN nguvu yake iko Syria kulinda Waislamu wanaoteketezwa na Mwislamu mwenzao.
 
Ndugu mtoa mada, binafsi nadhani ungeweka kichwa cha habari yako kuwa "MAUAJI YA KINYAMA KWA RAIA BURMA"
hapo ungepata uungwaji mkono, lakini kuanza kutenganisha tena na mambo ya UDINI ndio umeharibu kabisa.
 
Wengi mliochangia humu ni mapimbi, watu wanauawa we kwako ni kicheko, acheni chuki za kidini zisizokuwa na tija.
 
Ya Waislam ndio yanaonekana 2?
Mgogoro tulionao duniani ni kuwa na watu wenye siasa kali kwa pande zote za dini. Hii inasababisha upofu pale yanapotokea madhara kwa upande usiokuwa wa dini yake. Lakini dini sahihi na hasa Uislamu unalinda maslahi ya watu wa dini na makundi yote ya jamii. Hakuna mtu mwenye ruhusa ya kujifanya mwenye haki ya kuua mwingine hata kama watatofautiana dini zao. Kwani dini, Mungu ameridhia ziwepo ili kuleta changamoto duniani na kama angetaka angetufanya wanadamu wote tuwe dini moja.
 
Sisi Tunachoweza Kusema na Kuhuzunika ni Watu Dhalimu wametoa roho za Watu wasiokuwa na Hatia!! Sasa Huku kusema waisalam!! Ndio Kutia msisitizo? au ni roho special Tofauti na mauaji Mengine?
...............yaaani Makafiri (Buddha) wamewaua Waislaam ! waabudu Sanamu hawawezi kuwa sawa na Waislaam !
 
...............yaaani Makafiri (Buddha) wamewaua Waislaam ! waabudu Sanamu hawawezi kuwa sawa na Waislaam !
Licha ya kuwa mko imani tofauti..... tafadhali jitahidi kudhibiti hali ya chuki kuwaelekea wale wa imani tofauti....
chuki pia ni ibada ya sanamu..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom