Mauaji ya kikatili kanda ya Ziwa

My Son drink water

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
4,932
13,283
Baada ya kupewa Taarifa hii niliamua kwenda mwenyewe kushuhudia hao wajane walioachwa baada ya waume zao kuuawa kikatili kwa kosa la kufanya uvuvi haramu .

Hakuna chombo Chochote cha Habari chenye uwezo wa kuripoti hili Tukio na kikabaki salama, hakuna, na ndio maana watu hawajui ukatili unaotendwa kwenye mkoa tarajiwa kanda ya ziwa.

Karibia na Ziwa kuna mbuga ya wanyama (iliyozinduliwa na wanyama kibao, wakiwemo Twiga na Simba kupelekwa huko).

Wale wavuvi wakisha kurupushwa ziwani na askari pori huwa wanakimbilia msituni ili kujiokoa wasikamatwe kwa sababu hawana access ya kutorokea zaidi ya msituni, lengo la wale askari ni kuwafanya wakimbilie msituni ili waliwe na Simba na ndicho ambacho hutokea.

Wanaokamatwa hupigwa risasi baada ya kutundikwa msalabani Kama Yesu kwa mateso makali.

Ananieleza X mvuvi aliyenusurika nikiwa nyumbani kwake pamoja mjane aliyekuwa akilia muda wote wa simulizi hii ya kweli, na ya kutisha.

Maelezo yote nime record, na kwa sababu za kiusalama siwezi kuyaweka hapa kwa sababu sauti yangu itasikika ikiwahoji, sitaki kumfuata Azory Gwanda.

Nilipata Taarifa hizi nikiwa Kisumu Kenya na kwa kuwa nilipanga kula Christmas Tanzania nikaamua niende kupiga kambi eneo hilo lenye majasusi wengi wa Serikali, nilitumia mbinu exceptional kupata hizi Taarifa.

Najua hii inaweza isidumu humu kwa sababu ya Udikteta wa Habari uliopo Tanzania, lakini kabla ya kuifuta naiomba Management ya JamiiForums itume kikosi kazi cha siri ili kwenda huko kupata Taarifa hizi, watumie ujasusi kuzipata wahakikishe hawajulikani kwa sababu adhabu ni kupotezwa kama Azory Gwanda.

Nilifikia Guest House yenye hadhi duni sana na mwonekano wangu nilivyojiweka haikuwa rahisi kunistukia lengo langu.

Wanawake wamebakia wajane, watoto wanateseka na njaa.

Mungu iponye Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app

=====

 
JF ni social media, wao wenyewe sidhani kama wana tafuta na kupasha watu habari unless wafanye hivyo kwa habari ambazo zimeletwa hapa na mdau, alafu wazifanyie fact checking kabla ya kuzisambaza, naonaga wakifanya hivyo twitter. waache waendelee namna hiyo wasijejiingiza matatizoni.

Ama sivyo, hiyo habari nimeisikia majuzi geita. taratibu zitakuwa wazi.
 
Mwanza eneo gani, kijiji gani weka majina ya hao wanawake ,tuliambiwa wewe uko Kenya unauza bia umerudi lini


USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabla ya Christmas mkuu ndo Nimerudi, majina yao ya nini? ili na wao muwaue kwa kutoa Taarifa?
Namalizia kuiandika kimombo kwa kirefu ili niwatumie mabeberu Marekani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza kuta unatafuta Kiki tu..coz siku zote ili habari iwe habari inapaswa iangalie pande zote mbili, sasa kutokana na njaaa..tetesi siku hizi nazo zimekua Ni habari na kujifanya umetumia ujasusi kumbe umesoma kwenye insta pages. Habari yako hainatofauti na Ile aliyotoa Zito kuhusu CAG mstaafu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…