Lumbi9
JF-Expert Member
- Oct 12, 2014
- 8,747
- 12,466
HAKUNA mtu aliyeamini anachokiona mbele yake, kila aliyepita njia alitikisa kichwa na wengine kuangusha machozi. Polisi kutoka kituo cha kati cha Nairobi walikuwa hapo mbele ya kanisa hilo kubwa wakifanya uchunguzi wa hili na lile. Mwili usio na uhai ulikuwa umelala chini na majeraha makubwa kifuani yakiwa yameganda damu nzito. Hakuna asiyejua mwili ule ni wa nani, kila aliyepita alisikitika, wengine hata walighairisha safari zao za kazini, vilio vilitawala eneo lile. Kila mtu alionekana kuguswa kwa namna moja au nyingine na mauaji ya Kasisi huyu wa kanisa la Roman Catholic, Rev Fr Frederick Gichuru, hakuna aliyejua kwa nini na ni nani aliyetekeleza mauaji haya ya kinyama.
Baada ya kumsachi hakuna cha ziada walichokikuta katika kanzu ya kasisi huyo zaidi ya rozari iliyokuwa mkononi mwake. ?Bila shaka alikuwa katika sala zake za asubuhi? sauti ya kukwaruza kutoka kwa koplo Otholong?ong?o ilipenya sikioni mwa sajenti Maria Kariuki ambaye kwa muda huo alikuwa bado amepigwa na butwaa. Sajenti Maria alisikitika na kujutia nafsi yake, alijiona kama mwenye makosa mbele ya Mungu kwa kifo hicho. ?Ndiyo, afande, daima asubuhi kabla ya misa makasisi wa kikatoliki huwa na wajibu wa kusali kwanza wao weyewe? Sajenti Maria alimjibu koplo Otholong?ong?o huku ukungu mzito ukimtoka kinywani mwake kuashiria baridi kali ya mwezi wa sita hapo Nairobi.
Bado sajenti Maria alikuwa kajiinamia jirani kabisa na mwili ule akiuangalia kwa makini jinsi ulivyoharibiwa kwa risasi, maganda saba ya Colt 45 yalikuwa mkononi mwake, huku akiyarusharusha alijinyanyua taratibu na kuamuru mwili ule uondolewe na kupelekwa chumba cha maiti cha hospitali ya rufaa. ? Inspekta Simon Saitoti alimkazia macho sajenti Maria aliyekuwa ameketi mbele yake akiwa na jalada moja la khaki lililoandikwa juu ?MAUAJI YA KASISI?, alionekana kama mtu ambaye haelewi anachoelezwa, alilivuta jalada lile na kuliperuzi kurasa zake chache kwa dakika kadhaa, kisha akainua macho yake kutazama ukutani ambako kulipambwa kwa picha ya muasisi wa taifa hilo, hayati Jomo Kenyatta. ?Umesema paroko wa kanisa hilo hamjamkuta, sivyo?? Inspekta Saitoti alimtwanga swali sajenti Maria. ?Ndiyo afande, na tulipowauliza masista walisema kuwa kawaida wanakuwa na zamu ya kufanya misa za asubuhi vigangoni, hivyo paroko alikuwa amekwenda kigangoni? Maria alijibu kwa ukakamavu wa kipolisi. ?Ok, mauaji kama haya hayajawahi kutokea hapa kwetu hii ni mara ya kwanza, na naomba sana iwe mara ya mwisho, endelea kufanya uchunguzi wa tukio hili kwa kina ukishirikiana na koplo Otholong?ong?o na mnipe taarifa za kina, ili tuwatie mbaroni wauaji.? ?Sawa afande? sajenti Maria alisimama na kurudi nyuma hatua mbili na kupiga saluti ikiwa ni kitendo cha kuonesha heshima kwa mkubwa wake kadiri ya nidhamu za kipolisi.? Kijua cha haja kililing?aza jiji kubwa la Nairobi, jiji lenye pilikapilika za kila aina katika ukanda wa Afrika ya Mashariki.
Watu walionekana wakitembea na kuvuka barabara kwa haraka haraka kuashiria kuwa ukichelewa tu matatu itakugonga. Bado hali ya ubaridi ilikuwa ikiendelea na kila mtu alionekana kujidhatiti kwa hali hiyo. Kwenye kituo kimoja cha basi, mwanaume mmoja mrefu alikua amesimama akisubiri matatu, mara tu matatu moja ikafika na muziki mkubwa ndani yake, akaikaribia na kupanda ndani yake, mkononi alikuwa na mfuko wa plastiki ulioandikwa UCHUMI, bila shaka alikuwa akitoka supermarket , safari yake kwa matatu hiyo iliishia katika kitongoji cha Uthiru Kenoo barabara kuu ya kwenda Uganda. Kwa mwendo wa wastani alivuka kwa kupitia daraja kubwa na kufika upande wa pili wa barabara hiyo ambapo kuna biashara nyingi, aliliendea gari aina ya Hammer lililokuwa limepaki hapo, ndani yake hakukuonesha dalili yoyote ya kuwapo mtu, alifungua mlango kwa kidubwasha maalum na kuuweka ule mfuko katika kiti cha mbele kisha akatokomea kusikojulikana. Takribani nusu saa hakuna aliyeisogelea gari ile, mara akaja mtu mwingine mnene wa haja pamoja na mwanamke mmoja mrefu na mwenye mwii ulioumbika vizuri, wakaingia ndani ya gari ile na kujifungia milango. ?Shit, washakosea tena? alisikika Yule mtu mnene aki