MAUAJI: ‘Waliomuua Sista walipora Sh20 mil’

Lamborghini

Senior Member
Joined
May 30, 2014
Posts
122
Reaction score
55
Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam imesema majambazi waliohusika na mauaji ya Sista wa Kanisa Katoliki, Clencensia Kapuli wamepora kiasi cha Sh20 milioni na nyaraka mbalimbali.

Tukio la kupigwa risasi sista huyo lilitokea juzi saa 8 mchana eneo la Riverside Ubungo, Dar es Salaam na dereva , Patrick Mwarabu alikatwa kidole gumba kwa risasi.

Sista Kapuli wa Shirika la Mtakatifu Maria wa Parokia ya Mtakatifu Gaudence Makoka jijini hapa alikuwa Mhasibu wa Parokia hiyo ambayo inamiliki Shule ya Sekondari Mwenyeheri Anwarite na Chuo cha Ufundi Stadi Makoka.

Kamanda wa Kanda hiyo alisema Kamishna Suleiman Kova alisema jeshi hilo limetangaza msako wa kuwatafuta na kuwakamata wote waliohusika na tukio hilo.

Kova alisema marehemu akiwa ameongozana na wenzake ambaye ni Sista Brigita Mbaga na dereva aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Hilux walikuwa wakitoka Benki ya CRDB, Tawi la Mlimani City kuchukua fedha.

Alisema walipofika eneo la Ubungo Kibangu ili kulipa deni la chakula katika duka la Thomas Francis ndipo walitokea majambazi wawili wakiwa na pikipiki ambayo haikusomeka namba.

Alisema kati ya majambazi hao mmoja alikuwa na bunduki aina ya SMG wakampiga risasi ya kidole gumba cha mkono wa kulia dereva wa gari hilo kisha sista huyo alipigwa risasi ya kifua na kuporwa fedha hizo Sh20 milioni.

Kova alisema jeshi hilo limebaini kuwa matukio ya ujambazi hasa unaohusiana na wananchi kuporwa kiasi kikubwa cha fedha unaanzia benki na huwafuatilia wanapoingia na kutoka.

“Ni muhimu kwa benki kuwahimiza wateja wao kutochukua kiasi kikubwa cha pesa kiholela kwani ni rahisi kuporwa na watu wasio na nia njema,” alisema Kova.

Alisema benki ziwahimize wateja wao kutumia njia mbadala za kusafirisha pesa nyingi kama vile kwa hundi, kufanya miamala bila kadi na matumizi ya kadi za ATM.

Kova alizishauri benki nchini zianzishe vitengo vya ushauri kwa wateja ili wanapokuwa na fedha nyingi wasindikizwe na polisi.
 
Kwa hiyo wanakomoa kwa sababu tu mtu umeenda kuchukua hela zako na hujawashirikisha police na ndio maana unaweza kuporwa meter chache tu kutoka sehemu iliyokua na Askari wenye silaha sio?
 
Waumini wameamua kurejesha na kuchukua sadaka zao kwa nguvu baada ya kugundua sadaka zao zinatumika kwenye biashara haramu za biashara ya unga...ukweli ndio huo hizo nyingine ni blah blah yaani bla blah nyingi...
 
Too sad..unamuua mtu kisa milioni ishirini? tena mko genge mkigawana labda kila mtu anapata milioni moja au mbili amabyao hata miezi miwili haifiki? Hii laana itawatesa maisha yao yote na watakufa vufo vya ajabu ajabu majambazi hawa.

Bado nasikitika mjamzito wa miezi tisa pia aliuwawa kwa risasi Arusha kisa simu na pete za dhahabu..watanzania tumekua wanyama zaidi ya Boko Haram...dah
 
Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam imesema majambazi waliohusika na mauaji ya Sista wa Kanisa Katoliki, Clencensia Kapuli wamepora kiasi cha Sh20 milioni na nyaraka mbalimbali.

Tukio la kupigwa risasi sista huyo lilitokea juzi saa 8 mchana eneo la Riverside Ubungo, Dar es Salaam na dereva , Patrick Mwarabu alikatwa kidole gumba kwa risasi.

Sista Kapuli wa Shirika la Mtakatifu Maria wa Parokia ya Mtakatifu Gaudence Makoka jijini hapa alikuwa Mhasibu wa Parokia hiyo ambayo inamiliki Shule ya Sekondari Mwenyeheri Anwarite na Chuo cha Ufundi Stadi Makoka.
 
Waumini wameamua kurejesha na kuchukua sadaka zao kwa nguvu baada ya kugundua sadaka zao zinatumika kwenye biashara haramu za biashara ya unga...ukweli ndio huo hizo nyingine ni blah blah yaani bla blah nyingi...

Ujambazi wa aina yeyote ule hauwezi kuchekelewa kama unavyofanya wewe.
 
Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam imesema majambazi waliohusika na mauaji ya Sista wa Kanisa Katoliki, Clencensia Kapuli wamepora kiasi cha Sh20 milioni na nyaraka mbalimbali.

Tukio la kupigwa risasi sista huyo lilitokea juzi saa 8 mchana eneo la Riverside Ubungo, Dar es Salaam na dereva , Patrick Mwarabu alikatwa kidole gumba kwa risasi.

Sista Kapuli wa Shirika la Mtakatifu Maria wa Parokia ya Mtakatifu Gaudence Makoka jijini hapa alikuwa Mhasibu wa Parokia hiyo ambayo inamiliki Shule ya Sekondari Mwenyeheri Anwarite na Chuo cha Ufundi Stadi Makoka.

Polisi jipangen vizur kuzuia matukio kama hayo hiyo ndo kazi yenu sio msubir kutangaza huku watu washapoteza uhai! kinga ni bora kuliko tiba
 
Unamuua mtu kwa 20mil? Ila mi kwa uzoefu wangu angebanwa dereva wao nahisi yeye anajua kuna siku wataenda kuchukua pesa bank japo inaelekea hakujua ni kiasi gani? Akujuae ndiye akumalizae
 
Mbona taarifa zinapingana zenyewe kwa zenyewe..!?
Kanisa si limetoa maelezo yake..!?
Hawa polisi huwa wanabahatisha habari zao..?
Nani tumuamini sasa?

rip marehemu.
 
We we unayesema waumini wameamua kurudisha sadaka zao..... Uwezo wako was kufikiri ni mdogo sn,embu jaribu kuwa na busara au ufunge kinywa chako
 
Waumini wameamua kurejesha na kuchukua sadaka zao kwa nguvu baada ya kugundua sadaka zao zinatumika kwenye biashara haramu za biashara ya unga...ukweli ndio huo hizo nyingine ni blah blah yaani bla blah nyingi...

Kama huumwi akili, baasi mm naona umeshakunywa ile pombe ya peponi kama kitabu chenu kinavyosema, kile kilichokuja na mafuriko mkasema kimetoka mbinguni
 
Matatizo sana, hali mbaya, ukata umezidi mpaka tunakabwa watu wanachuku hata buku mbili ikiwezekana
 
Waumini wameamua kurejesha na kuchukua sadaka zao kwa nguvu baada ya kugundua sadaka zao zinatumika kwenye biashara haramu za biashara ya unga...ukweli ndio huo hizo nyingine ni blah blah yaani bla blah nyingi...

mfano nikisema wewe ni mpumba vu nitakuwa nimekosea?
 
Admin funga na thread hii kabla mjadala haujashika kasi. Kwa sababu nimegundua kama mjadala unahusu kanisa na hasa kaa mjadalam huo unaelekea kudidimiza hija zake, fasta fast unaufunga. Kwa mpango huu utatukosa wengi kwa sababu tutahamia MWANA.HALISI.Forum. Wewe ubakie na jambi lako la kikanisa kanisa.
 
Waumini wameamua kurejesha na kuchukua sadaka zao kwa nguvu baada ya kugundua sadaka zao zinatumika kwenye biashara haramu za biashara ya unga...ukweli ndio huo hizo nyingine ni blah blah yaani bla blah nyingi...

Kichwa chako kina mafuta ya taa?
 
Admin funga na thread hii kabla mjadala haujashika kasi. Kwa sababu nimegundua kama mjadala unahusu kanisa na hasa kaa mjadalam huo unaelekea kudidimiza hija zake, fasta fast unaufunga. Kwa mpango huu utatukosa wengi kwa sababu tutahamia MWANA.HALISI.Forum. Wewe ubakie na jambi lako la kikanisa kanisa.

Mjadala hauwezi kufungwa kwa ajili mpmbv mmoja
 
Sio kwamba nalituhumu kanisa ila ni uzembe, kuna maswali najaribu kujiuliza nakosa majibu.

1. Je hiyo mwenye Tender hakuwa na account kiasi kwamba kanisa lingefanya TISS?

2. Kulikuwa ulazima wa kumpatia mwenyw Tender Cash?

3. Kwanini asingepewa Cheque?

Ni uzembe wa hali ya juu
 
Back
Top Bottom