Mauaji Tarime: CUF yacharuka, yaibana Serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji Tarime: CUF yacharuka, yaibana Serikali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, May 27, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Alisema Profesa Lipumba
  Katika maazimio hayo, alisema Baraza Kuu linalaani vitendo vya ukiukwaji na uvunjwaji wa haki za binadamu kwa mauaji ya raia yanayoendelea kuripotiwa mara kwa mara yanayofanywa na Jeshi la Polisi nchini, kama ilivyotokea katika mgodi wa North Mara.

  “Inaonekana sasa umejengeka mtindo wa kuonekana kuwa hilo ni jambo la kawaida, ambalo watendaji wanaweza kufanya bila ya kuchukuliwa hatua yoyote. Hivyo, Baraza Kuu linataka uchunguzi wa kina juu ya mauaji yaliyotokea North Mara ufanyike sambamba na Waziri wa Mambo ya Ndani, awajibike kutokana na mauaji hayo kwa kujiuzulu,” alisema Profesa Lipumba.

  Pia alisema Baraza Kuu linalaani vikali tabia inayoanza kujitokeza tena kwa vyombo vya dola kuwafungulia mashtaka ya uongo (kuwabambikia kesi) wanasiasa.

  Source: IPPMedia
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ungekuwa ni mfumo wa kifalme kwamba unadumu hadi kifo kinapohitimisha mtu kutawala na mrithi kuendelea na taji la mzazi wake mambo yangekuwa mabaya zaidi, lakini hii tu ya kipimo cha miaka 5 na kisha unaongezewa mingine mitano halafu unakaa kando na kuwaachia wengine kiti, mtu unajisahau kama una mamlaka yooote mbinguni na duniani.
   
 3. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Waraka wa kulaani? Badala ya kushirikiana na wanyimwa haki,wanaenda kuandika kulaani?nani asiyejua kuandika? Lipumba,uzarendo u wapi? Mnalaani?na taasisi za dini na NGO wafanyeje? Mngekuwa serious mngefika nyamogo,mambo ya kubembeleza mtu ajiuzulu nani kakwambia?acha izo!
   
 4. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Walipopigwa Wazanzibari nyinyi CHADEMA mlichukua hatua zipi Mkuu?

  Ushirikiano gani mliutoa kwa CUF na Wazanzibari walipokuwa wakihujumiwa na Majeshi ya kutoka Tanganyika?

  Nyinyi mlikuja Unguja na Pemba au mlitoa angalau hio kauli ya kulaani?

  Si mlikuwa mnatucheka na kusema sisi ni wakorofi?

  Wacheni hizo.
   
 5. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2011
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 667
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 80
  Kumbe CUF ni chama cha Zenjibar? Asante kwa taarifa!
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  May 27, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  CuF, aka ccm B, ni wanafiki ! Debe tupu.
   
Loading...