mauaji sehemu 5

mauaji sehemu 5

mtafuta-maisha

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2016
Posts
1,982
Reaction score
2,934
Hii story inaanzia hapa Wakala wa kifo alivyowatesa polisi katika kesi ya aina yake

Fort Lauderdale

Polisi moja kwa moja walifungua jarada la mashitaka kwa kosa la mauaji ya William na Lilian, hivyo waliweza kupata kibari cha kumkamata pamoja na hati ya kukagua gari lake. Polisi wote Forida walipewa picha ya gari la Jones nap cha ya Jones na walitakiwa popote pale watakapomuona amkamate na kutoa taarifa kwa makachero wanaohusika na kesi yake. Siku moja polisi wa doria wanaona lile gari la Ford la miaka ya 90 ambalo Jones alinunua Tennessee likiwa limeegeshwa kweye mitaa ya Fort Lauderdele, wanajongea na kutoa taarifa kwa makachero ambapo wanafika na wataalamu wa kuchunguza alama na kutafuta ushahidi usioonekana kwa macho ya kawaida na kuanza kulifanyia kazi.

Kati ya vitu vilivyokutwa kwenye lile gari ilikuwa gundi kwa ajili ya kufungia watu, vifaa vya kufanyia usafi ikiwemo kemikali na sabuni pamoja na ndoo, na ushahidi mkubwa walioupata ilikuwa ni bendera ya Puerto Rico, na kutokana na maelezo ya William Perez baba yake marehemu Carlos Perez aliwambia polisi kuwa alisafiri kwenda Puerto Rico na aliporudi moja kati ya zawadi alizorudi nazo ni bendera za Puerto Rico tatu ambapo bendera moja alimpatia Carlos Perez kama zawadi. Hivyo alikuwa bado anabendera mbili na hizo bendera tatu zote zilikuwa zinafanana na polisi waliporinganisha hiyo bendera waliokuta kwenye gari la Jones na zile mbili ni kweli zilikuwa zinafanana kwa kila kitu.

Pia polisi walikuta pete ikiwa imefichwa kwenye siti za nyuma ya lile gari, ambapo Magret mtoto wa marehemu Lilian aliitambua kuwa ile pete ilikuwa ya mama yake. Ushahidi wote unaonyesha kuwa Jones ndiye mhusika wa mauaji lakini tatizo ni kwamba kwa mudahuo Jones alikuwa hafahamiki alipokuwa. Hivyo makachero waliamua kuwahusisha wapelelezi toka kitengo cha kusaka watuhumiwa waliokimbia mkono wa sheria ili wasaidie kumnasa na kumweka mhabusu.

Tarehe 16 mwezi wa 9 mwaka 2003, Kachero Chuck Morrow toka kituo cha polisi cha Fort Lauderdele anakabidhiwa jukumu la kumsaka Jones. Chuck yeye ni mtaalamu wa kuwasaka na kuwakamata watu ambao hawataki kukamatwa hivyo wanaamua kujificha. Baada ya kupewa jukumu hilo moja kwa moja alielekea mtaani kuwaona watoa taarifa wake wa mtaani ambao ni raia wa kawaida wakiwa maeneno mbalimbali ya mitaa. Katika mahojiano na kijana mmoja mwenye asili ya Kihispania huko Mashariki mwa fukwe za Palm (West Palm Beach), alimtaarifu kuwa uwa anamuona mara kwa mara, na akija hakai sana uwa anawahi kuondoka baada ya kuonana na watu wake.

Kesho yake kachero Chuck anategesha gari kwenye maegesho ya Sunrise yaliyoko Braverd kwakuwa alikuwa amepata taarifa kwamba kuna uwezekano mkubwa kuwa jioni ya siku hiyo anaweza kuwa anaendesha gari lake dogo aina ya Ford jeupe. Baada ya kuwa pale kwa masaa manne alikata tama kuwa Jones hatatokea hivyo kwa kutumia redio yake ya upepo aliwataarifu wenzake kuwahakuna dalili yoyote ya Jones kutokea labda wajaribu siku inayofuata. Akiwa anataka kuondoka kwa ajili ya kurudi nyumbani akalale mara anaona gari jeupe aina ya Ford linaingia maeneo yale na kuelekea sehemu ya maegesho na ndani dereva anayeliendesha ni Jones.

Chuck anawasha gari na kumfuata kwa nyuma na Jones anapogundua kuwa anafuatiliwa anaondoa gari kwa kasi na wanaanza kufukuzana kama watu walioko kwenye mbio za magari. Chuck anatoa taarifa juu ya kuonekana kwa Jones na kwamba yuko kwenye mbio za kufukuzana naye hivyo anaomba msaada wa helkopta angani ya kumfuatilia kwa juu na polisi wote walioko kwenye doria eneo hilo waungane kumfukuza.

Kati ya askari waliokuwa kwenye doria siku hiyo alikuwa Carlos na aliweza kupata ujumbe kupitia redio yake ya upepo hivyo naye alijiunga kwenye mbio hizo. Carlos alifanikiwa kuliziba gari la Jones kwa mbele na hivyo jones ilimlazimu kusimaisha gari lake. Polisi walilizunguka gari lake wake na siraha tayari kwa mashambulizi kwakuwa walikuwa wanahofia kwamba Jones asingeweza kukubari kukamatwa kizembe. Walimuamuru atoke kwenye gari mikono akiwa kaiweka nyumba ya kichwa chake na baada ya kusita sita kwa sekunde kadhaa Jones alifungua mlango na kujisalimisha ambapo alitiwa pingu na kupelekwa mahabusu.

Wiki mbili baadae

Kutokana na zile nywele zilizopatikana kwenye mwili wa Perez, waliziringanisha DNA na DNA kutoka kwenye mate ya Jones na ilibainika zile nywele zilikuwa zake. Pia alama za kiatu zilizochukuliwa toka mafuni kwenye kile chumba cha hoteli, zilifanana na sole ya kiatu kilichokutwa kwenye gari lake.

Kutokana na kwamba Jones aligoma kabisa kukiri juu ya uhusika wake kwenye mauaji ya Perez polisi waliweza kuunga matukio ya ni kitu gani kilitokea siku ya mauaji ya Perez.

Kwa maoni ya polisi wanahisi kwamba baada ya Kachero Carlos kumsimamisha Yung na kumkamata, Jones alienda kazini kwake akitafuta mtu mwingine wa kumsaidia kuendesha lile gari lilikokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara. Kwakuwa Perez alikuwa ni kijana nayependa kutoa msaada alijitolea kumsaidia hivyo waliondoka wote kutoka Fort Lauderdele mpaka Melbourn, gari lilipokuwa ambapo Perez aliendesha lile gari jeupe akifuatana na Jones aliyekuwa anendeshalile gari alilokuwa kanunua. Polisi wanaamini katika safari hiyo Jones anaamua kuacha gari alilonunua mahali flani na wote wanapanda gari jeupe na Jones anaelekea mpaka pale hotelini. Na hiyo ndiyo ilikuwa mara ya mwihso ya Carlos kuonekana akiwa hai.

Mwaka 2009 miaka sita baada ya mauaji hayo, mahakama ya Tennessee inampata nahatia Henry Jones katika mauaji ya watu wawili yani William na mkewee Lilian na anapokea adhabu mbili za kunyongwa. Mwaka 2013 pia mahakama ya Florida inamkuta na hatia ya Kumuua Carlos Perez ambapo inamhukumu pia kunyongwa.

Japokuwa hakuwahi kufunguliwa mashitaka, ila Jones ndiye mtu pekee anayetuhumiwa kwenye mauaji ya kesi ambayo hajatatuliwa ya mauaji ya mwanafunzi ajulikanaye kama Keese Gloth. Ilibainika kwamba Jones alikuwa ni kati ya marafiki wa Keese ila kwenye eneo la tukio hakuna DNA wala ushahidi wowote unaomfunga Jones kama ndiye alimuua maana mhusika alihakikisha haachi ushahidi.

Polisi wanadai kwamba Jones anaongozwa na tamaa na matamanio na natumia ukarimu wa watu kupata kile anachotaka, wanazidi kudai ya kwamba mauaji ya Keese na Perez aliyatekereza kwa kuongoza na matamanio ya kufanya ngono wakati mauaji ya William na Lilian aliyatekereza akiongozwa na tama ya kupata pesa. Pia wanaongeza kwamba Jones anaburudika kuua watu kwa mateso ndiyo maana alikuwa akitekereza mauaji kwa kuatesa watu kwa kisu badala haya ya kuwapiga risasi wakafa haraka, ila yeye alichagua njia ya mateso.

Yung japo yeye alikana kushiriki kwake katika mauaji ya William na Lilian, ila alikubari tuhuma za kumsaidia Jones kutekereza mauaji hayo na alihukumiwa miaka 15 jela. Hii ni kutokana kwamba alishuhudia Jones akitenda mauaji hayo lakini hakuchukua hatua yoyote hata pale alipokamatwa na askari bado hakutoa taarifa na kwenye mahojiano alijaribu kuficha ukweli mpaka alivyobanwa na makachero ndipo akasema.

**************************************mwisho**********************************
 
Asante mkuu. Hapa nimeridhika.
Ila wenzetu wataalamu atii. Bongo hiyo kitu hamnaga tuna police wa kuzuia maandamano tuu
 
Asante mkuu. Hapa nimeridhika.
Ila wenzetu wataalamu atii. Bongo hiyo kitu hamnaga tuna police wa kuzuia maandamano tuu
Wakikusikia utasafirishwa....
Naona ulitaka kunilipa sa mbona umebadirisha mawazo
 
Back
Top Bottom