Mauaji Pwani: Ukweli utatuweka huru

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,318
Kuna dhana mbalimbali kuhusiana na mauaji ambayo yamekuwa yakitokea Mkuranga. Kwanza lazima tukiri kuwa ni dhahiri shahiri wahusika ni watu wenye mafunzo mazuri na si kuwa ni wezi wa kawaida. Hili jambo linaleta ukakasi. Dhana kadhaa-
1. Kuna kikundi cha ugaidi ambacho kina operate kwa sababu flan ambazo pengine zimefichwa ambacho kimeamua ku deal na viongozi mfano wenyeviti wa vijiji n.k pia katika hilo hilo wameamua ku deal na askari

2. Askari wa mkuranga wafuatiliwe kama wamewah kufanya matendo yasiyo stahili kwa raia. Si binadamu wote wenye kusamehe.wengine huamua kulipiza kisasa pale wanapofanyia vibaya na katika hilo wanaingia wote waliofanya mabaya na wema waliokuwa sehem isiyo sahihi,wakati usio sahihi na watu wasio sahihi.

3. Pengine kuna ujumbe watu flan wanatuma kwa serikali na wananchi. Jiulize mkoa wa pwan ambao ni mdogo na usio na watu wengi kwa nini huko?yamewezekana kuna kundi kubwa lenye mafunzo sehem flan likifadhiriwa na watu flan.

Askari polisi tendeni haki, msiwaonee raia,tengenezen urafik na raia hbr nying wanazo wao. Lakin mkitengeneza uadui nao msidhan mtakuwa salama hata kama mtakuwa na silaha nyingi na kali.
 
Tusiwape jukwaa magaidi,ndicho wanachotaka, kututia hofu ili tukubaliane na masharti yoyote watakayotoa, maadam vyombo vinashugulikia (nadhani wote tunaamini), tujifanye kama hatuju (ushauri ili jamii isipate hofu "terror"), na wakikamatwa wauwawe kimya kimya, hatutaki matangazo!!!

Na kama ni jamii ya wahamiaji mf. Wasomali, lazima " victimization" ifanyike, kwa kila msomali mmoja wafukuzwe 1000, hapo abadan hawatarudia!!!
 
nchi yetu si inaitwa kisiwa cha amani? Hiyo ndio inatuponza tunashindwa kutangaza kuwa hawa ni magaidi tunaendelea kuficha mambo huku "tukifa na tai shingoni"
majambazi hawawezi kuiba silaha za polisi,kukaa maporini na kuuwa watu wa serikali hapo kuna jambo.
na wataendelea kufanya unyama mkubwa kwa kutumia style ya ualifu
 
Nimemsikia mkuu wa polisi pwani akidai ni majambazi wa kawaida saba wala sio magaidi
 
Nimemsikia mkuu wa polisi pwani akidai ni majambazi wa kawaida saba wala sio magaidi
Aliwahesabu muda gani kuwa ni saba? Basi itakuwa pia anawafahamu. Na kama ni wa kawaida, askari wake nao ni wa kiwango gani? Ukakasi kidogo, majambazi ya kawaida yanaua askari 8 na hayajakamatwa na ukawaida wao??
 
Nimeshangaa kuona Rais nchi kwa 2kio la kuuwawa askar katoa pole lkn kutekwa kwa Roma Mkatoliki na kupotea kwa Ben Saa Nane mkulu kauchuna kana kwamba halijamuumiza vle,hakikika napata pcha tofauti kwa mazira haya! au police wanaumuhm zaid ya akina Ben Saa Nane? kwa ujumla tengenezeni mazingira mazur na raia make police wakikukamata watakunyanyasa kama vle umeua cjui kwa nn? may their soul rest in peace!
 
Jamani polisi wengine tuna watoto wetu polisi hebu fanyeni operesheni safisha pwani hawa majambazi si ya kawaida, Tanzania hatujazoea askari kuvamiwa na kuuwawa, haya mambo yameanza hivi karibuni, tulikua tunasikia Al-shabab kwa jirani wakifanya vitendo hivi, majambazi ya kuua askari wetu.na kupora silaha hapo napata shida kidogo kuita ujambazi wa.kawaida hawa ni MAGAIDI
 
Tusiwape jukwaa magaidi,ndicho wanachotaka, kututia hofu ili tukubaliane na masharti yoyote watakayotoa, maadam vyombo vinashugulikia (nadhani wote tunaamini), tujifanye kama hatuju (ushauri ili jamii isipate hofu "terror"), na wakikamatwa wauwawe kimya kimya, hatutaki matangazo!!!

Na kama ni jamii ya wahamiaji mf. Wasomali, lazima " victimization" ifanyike, kwa kila msomali mmoja wafukuzwe 1000, hapo abadan hawatarudia!!!
Masuala serious kama haya hatuwezi kufanya maamuzi kupitia dhana lazima uchunguzi wa kina ufanyike. TISS ifanye kazi......!
 
Tusiwape jukwaa magaidi,ndicho wanachotaka, kututia hofu ili tukubaliane na masharti yoyote watakayotoa, maadam vyombo vinashugulikia (nadhani wote tunaamini), tujifanye kama hatuju (ushauri ili jamii isipate hofu "terror"), na wakikamatwa wauwawe kimya kimya, hatutaki matangazo!!!

Na kama ni jamii ya wahamiaji mf. Wasomali, lazima " victimization" ifanyike, kwa kila msomali mmoja wafukuzwe 1000, hapo abadan hawatarudia!!!
Kuwaambia watu wanyamaze si vyema sana kwani swala hili liko miongoni mwa watu so acha waseme, watu semeni chochote mkijuacho kuhusu udharimu huu
 
Nimeshangaa kuona Rais nchi kwa 2kio la kuuwawa askar katoa pole lkn kutekwa kwa Roma Mkatoliki na kupotea kwa Ben Saa Nane mkulu kauchuna kana kwamba halijamuumiza vle,hakikika napata pcha tofauti kwa mazira haya! au police wanaumuhm zaid ya akina Ben Saa Nane? kwa ujumla tengenezeni mazingira mazur na raia make police wakikukamata watakunyanyasa kama vle umeua cjui kwa nn? may their soul rest in peace!
Siasa zitakupotez one day... Si kila jambo la kuchukulia kimzaa mzaa...
 
Tiss inachekesha. Ukiona mambo wanauaowafanyia raia ambao hata si tishio Kwa taifa. Usalama gani sasa wataifa. Ndio maana hata hawa majsmbaz wamewadharau na kuwaua ndugu zetu polisi kikatili.

Tiss ya serikali ya Somalia ambauo Bado dhaifu iko fiti hata kuliko hii yetu.
 
Back
Top Bottom