MAUAJI NGARA: RPC:Raia alitaka kumchoma Polisi kisu

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Posts
4,225
Reaction score
869
Wakuu:

Kwa mujibu wa Taarifa za matukio RFA Kamanda wa polisi mkoani Kagera Philip Kalangi Chanzo cha Askari polisi kumpiga risasi Raia wilayani Ngara ni baada ya rai huyo kumchomolea kisu na kutaka kumchoma wakati akipelekwa kituo cha polisi ndipo askari akamfyatulia risasi iliyomjeruhi vibaya na kupoteza maisha!!!!!!!

SWALI LA MSINGI:Kama kweli raia alimchomolea kisu askari polisi alikuwa na sababu za msingi za kumpiga risasi?
Wakati anamchomolea kisu walikuwa umbali gani?,Au ndiyo yaleyale ya kitu chenye ncha kali?

Baada tu ya hiyo thread kupostiwa humu JF juzi badhi ya wadau humu walianza kuonesha wasiwasi juu ya taarifa itakayotolewa na polisi wengine wakaenda mbali zaidi na kubashiri kwamba kwa vyovyote vile taarifa ya polisi itamkandamiza raia na ndicho kinachoonekana hapa.

Tujadili pamoja!!!!!!!!!
 
Mwambieni hata RPC siku moja atakufa maana kaumbwa kwa nyama, damu mifupa na manywelenywele kichwani. Poor authority! Poor leadership ==> NO PEACE!
 
Kwa mtazamo wangu SIASA ZA TANZANIA NA WANAOJIUNGA NA UPOLISI wameachiwa watu wengi ambao sio makini na ndio maana NCHI inayumba.watu wachache sana huko ni makini na wanazingatia maadili.tufike mahali kuwe na viwango vya mtu kuwa mwanasiasa au kuwa polisi.raia alikuwa mmoja, askari wawili tena na bunduki walishindwa vipi kumdhibiti bila kuleta madhara? hata ingebidi wa mwachie tu aende kwasababu wanajua mahali anapofanyia kazi au kuishi, wangerudi siku nyingine wakiwa wamejipanga vizuri na pengine wakiwa wengi zaidi kuliko kudhani kuuwa ingekuwa ni suluhu. kamwe wasingebaki salama kama ilivyotokea.
 
... hizi scripts za movie za kusafisha polisi wetu Bongo baada ya mauaji ni za ajabu sana, yaani hata ummpe director wa Kinaijeria hawezi kuziongoza!!
 
Kwa mtazamo wangu SIASA ZA TANZANIA NA WANAOJIUNGA NA UPOLISI wameachiwa watu wengi ambao sio makini na ndio maana NCHI inayumba.watu wachache sana huko ni makini na wanazingatia maadili.tufike mahali kuwe na viwango vya mtu kuwa mwanasiasa au kuwa polisi.raia alikuwa mmoja, askari wawili tena na bunduki walishindwa vipi kumdhibiti bila kuleta madhara? hata ingebidi wa mwachie tu aende kwasababu wanajua mahali anapofanyia kazi au kuishi, wangerudi siku nyingine wakiwa wamejipanga vizuri na pengine wakiwa wengi zaidi kuliko kudhani kuuwa ingekuwa ni suluhu. kamwe wasingebaki salama kama ilivyotokea.

Kumbe wewe bado hujachoshwa na hili neno ''ifike mahali/ tufike mahali'' : teh teh!
 
leo nitakua against wengi kiukweli ifike mahali tuwaheshimu police na wao watuheshimu siye pia. haiwezekani kila siku police wawe wanakosea tuu hata siye pia tunazingua kiukweli.... nafikiri ifike mahala tuheshimiane na tuache kudharauliana
 
Kalangi Go tell it to the birds. Kila siku askari wetu hawakosei bali wanakosewa siyo? Sasa mmeona tabia ya kuwapendelea na kuwapa kiburi ilivyowatokea puani hao wenzenu waliouawa baada ya kummwangosi raia mwema. Ingawa si vizuri kushabikia visasi, kwa vile jeshi la polisi limejiona kuwa lipo pale kuua raia wasio na hatia si vibaya nao raia wakiamua kujipa jukumu la kuwalipizia kisasi askari watakaowadhulumu au kuwaonea. Jino kwa jino and tit for tat. Huenda kitaeleweka.
 
Kwanini hawakumfunga pingu.
Je suluhisho lilikuwa ni kumpiga risasi tu? Hawa polisi wetu hawana mbinu nyingine zaidi ya kuua?
 
Huu ni uongo uliokithiri!! Kwani hakufungwa pingu huyo mtuhumia? Alichomoaje kisu kama alifungwa mikono? Nijuavyo mimi huwa wanatumia kamba kama hawana pingu. Kama hawakumfunga mikono basi ni wazembe hawafai kuwa mapolisi. Pia kwani hakuweza kuzuia yule kumchoma kisu bila kumuua?? Wnajitetea tu hao. Wamezoea kutuua sasa wanataka kuhalalisha vitendo vyao!! Damu zetu zinazopotea zitawalilia ardhini!! Iko siku moja wataumbuka pale ambapo Mungu wetu atakapotutetea!!!
Wakuu:

Kwa mujibu wa Taarifa za matukio RFA Kamanda wa polisi mkoani Kagera Philip Kalangi Chanzo cha Askari polisi kumpiga risasi Raia wilayani Ngara ni baada ya rai huyo kumchomolea kisu na kutaka kumchoma wakati akipelekwa kituo cha polisi ndipo askari akamfyatulia risasi iliyomjeruhi vibaya na kupoteza maisha!!!!!!!

SWALI LA MSINGI:Kama kweli raia alimchomolea kisu askari polisi alikuwa na sababu za msingi za kumpiga risasi?
Wakati anamchomolea kisu walikuwa umbali gani?,Au ndiyo yaleyale ya kitu chenye ncha kali?

Baada tu ya hiyo thread kupostiwa humu JF juzi badhi ya wadau humu walianza kuonesha wasiwasi juu ya taarifa itakayotolewa na polisi wengine wakaenda mbali zaidi na kubashiri kwamba kwa vyovyote vile taarifa ya polisi itamkandamiza raia na ndicho kinachoonekana hapa.

Tujadili pamoja!!!!!!!!!
 
hapa naona weledi, haukutumika, najua raia nao siku hizi, tunajua saana na tuna kiburi sababu ya utandawazi, haya yanayotokea kwetu, si mageni duniani au nchi za wenzetu, na huko Mugoma ni jirani na nchi ya Burundi, eneo ambalo limeathiriwa saana na wakimbizi, wengine wakiwa bado ,nchini wakijifanya ni raia wenzetu, polisi kosa walilofanya ni kutompekuwa mtuhumiwa huyo, wakati wanampeleka kituoni. kukamatwa si mchezo,mtuhumiwa anakuwa na mawazo mengi juu ya maisha yake na familia yake, pamoja na rekodi zake za nyuma. yawezekana pia akawa na wasiwasi juu, ya matukio mbalimbali aliyowahi kuyafanya siku za nyuma, huenda nayo yakajulikana au yamejulikana ndo maana nimekamatwa kwa issue hii ndogo ya pikipiki kwa kisingizio tu. unaweza ukaona au kupima kuwa kisu na risasi ? tujikumbushe matukio yaliyojitokeza kule TARIME, ambako askari aliuwawa, kwa kuchomwa kisu na mtuhumiwa huku wengine wawili, wakijeruhiwa vibaya. na mtuhumiwa akifanikiwa kutorokea nchini Kenya. POLISI fanyeni kazi zenu kwa weledi. mpekueni mtuhumiwa na kisha mfungeni pingu mtaepusha mengi.
 
hivi siku hizi mtu akikamatwa na polisi hafungwi pingu tena?kosa ni la nani?
 
Kimaroo kinachoongelewa hapa ni polisi kujichukulia madaraka/maamuzi/uhalali wa kuua raia na sio suala la kuwaheshimu au kutowaheshimu. Wao wanatakiwa kuwalinda wananchi wote hata watuhumia. Iweje leo wanaua watuhumia? Hii si haki. Binadamu wote wana haki ya kuishi. Wao wamepewa na nani mamlaka hayo ya kutuondolea haki hii? Damu zetu zinawalilia!!!
leo nitakua against wengi kiukweli ifike mahali tuwaheshimu police na wao watuheshimu siye pia. haiwezekani kila siku police wawe wanakosea tuu hata siye pia tunazingua kiukweli.... nafikiri ifike mahala tuheshimiane na tuache kudharauliana
 
leo nitakua against wengi kiukweli ifike mahali tuwaheshimu police na wao watuheshimu siye pia. haiwezekani kila siku police wawe wanakosea tuu hata siye pia tunazingua kiukweli.... nafikiri ifike mahala tuheshimiane na tuache kudharauliana
Polisi wajiheshimu na waheshimu pia haki za binadamu na wao wataheshimiwa,vinginevyo wataisha, na kizazi kijacho kitaogopa kufanya kazi ya upolisi!!
 
kazi ndo' ishaanza akifa raia mmoja polisi watakufa zaidi ya hapo.. risasi kitu gani..,?
 
Wakuu:

Kwa mujibu wa Taarifa za matukio RFA Kamanda wa polisi mkoani Kagera Philip Kalangi Chanzo cha Askari polisi kumpiga risasi Raia wilayani Ngara ni baada ya rai huyo kumchomolea kisu na kutaka kumchoma wakati akipelekwa kituo cha polisi ndipo askari akamfyatulia risasi iliyomjeruhi vibaya na kupoteza maisha!!!!!!!

SWALI LA MSINGI:Kama kweli raia alimchomolea kisu askari polisi alikuwa na sababu za msingi za kumpiga risasi?
Wakati anamchomolea kisu walikuwa umbali gani?,Au ndiyo yaleyale ya kitu chenye ncha kali?

Baada tu ya hiyo thread kupostiwa humu JF juzi badhi ya wadau humu walianza kuonesha wasiwasi juu ya taarifa itakayotolewa na polisi wengine wakaenda mbali zaidi na kubashiri kwamba kwa vyovyote vile taarifa ya polisi itamkandamiza raia na ndicho kinachoonekana hapa.

Tujadili pamoja!!!!!!!!!

Da polisi wanakazi sana jamani duuu,sasa angefanyaje huyu askari kama raia ameonekana kukaidi amri na ametoa kisu ina maana hapo ni kila mmoja alikuwa anajihami arafu sisi raia ukiona askali ana bunduki tunasemaga hawapigi haoooo .nafikiri askari alikuwa anajihami na yeye ila raia nao tumezidi kujichukulia sheria mkononi,itafika muda tutakuwa tunasaidia ujangili kama ndo ivyo na hatutakuwa na msaada na askari kwa kukomesha uharifu hapa.
 
Back
Top Bottom