Mauaji na hisia za kiongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji na hisia za kiongozi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sijali, Sep 11, 2012.

 1. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,062
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Ni jambo sijalipatia jibu: hivi kiongozi, sema rais, anahisi vipi wakati chombo/vyombo vya serikali yake vinatwaa roho ya raia, hasa hasa bila haki?
  Nauliza hivi kwa vile mimi binafsi, ambaye sina uhusiano wowote na serikali wa mfiwa, huniwia vigumu sana kusikia raia asiye hatia, saa nyingine kijana, mtoto, mwanamama aliyeacha mtoto wake mchanga, anauawa kwa dhuluma na serikali. Nahisi ingekuwa mimi ndiye kiongozi ningeamuru bila kusita hao waliofanya hivyo wapewe adhabu kali, ikithibiti ni kwa kusudi na ubabe tu, wauawe pia. Kwa sababu kwangu hakuna hatia kubwa kama kumpotezea mtu maisha yake.
  Kwa sabau huyu hana namna nyingine ya kurudi duniani.
  Ukiangalia marais wetu wote waliokuja baada ya Nyerere, wameua. Nasema hivyo kwa sababu wao ndio wanahusika moja kwa moja na vyombo walivyoviweka. Aidha, kama wangetaka kujiondolea manza au lawama wangechukua hatua kali.
  Lakini wapi. Inaelekea kana kwamba marais wa Tanzania wamezoea kiasi wanaona mauaji ya raia ni jambo la kawaida tu.
  Angalia mauaji ya Mwembe Chai, ya kusudi kabisa (nina video ambapo askari anatoa amri: 'njoo hapa, piga huyu, ua kabisa!'
  Au mauaji ya Zanzibar........
  Lakini katika yote ni haya mauaji ya mara kwa mara katika chaguzi, au maandamano ya amani au hata mikutano tu ya usiokuwa upande wa CCM.
  Najua rais Kikwete ni Mwislamu, au anajitambulisha kuwa Mwislamu safi. Sasa namwuliza: amesoma Qur'an? Kwa maana Qur'an inaweka wazi kabisa kuwa mtu mwenye kumwua mtu mmoja asiye hatia, dhambi yake ni kama ya aliyeua dunia nzima! Nadhani atasema kuwa 'si mimi niliyeua' Hilo pia linajibiwa na Qur'an na Hadith, kwamba mtu anapokuwa kiongozi anakuwa ndiye 'mas'uul' wa raia wake, mke wake, watoto wake, wanyama wake n.k. Kuna mfano mzuri wa Khalifa wa pili baada ya Mtume Mohammad SWA. Huyu alikuwa Omar. Bwana huyu nchi ilipoingia njaa, alikuwa hali chakula chochote chenye mafuta wala nyama wala samaki. Alikuwa anakula, kama Tanzania tungesema 'bada' yaani ugali wa muhogo. Alipoulizwa kwa nini, alisema kwa vile mimi ndiye mas'ul wa watu hawa M/Mungu atakwenda kuniuliza kwa nini fulani alishindwa kula nyama na wewe ukawa unakula nyama?
  Kwa muda wa miezi yote sita ya njaa, Omar alikuwa anafungua kinywa kwa bada na kulalia bada!
  Ole wenu nyie Kikwete na Mwinyi! Kwa uchache itabidi mchukue hatua juu ya mauaji yaliyotokea katika kipindi cha uongozi wetu, otherwise, mjue fika hamtakuwa na la kumjibu Mola wetu. Wala isikubabaishe kuwa unafanya matendo mengine mema. Kutoa uhai wa mtu ni jambo halisamehewi na hata M/Mungu (kwa mafunzo ya Kiislamu) 'hana uwezo' wa kusamehe hilo, mpaka huyo aliyekosewa asamehe kwanza. Na huko twendako uwezekano wa mtu uliyemtendea maovu duniani kwenda kukusamehe huko ni 00.0001%
  Unaweza kupuuza haya na kuacha kuamini, lakini si muda mrefu nawe utaingia kwenye shimo lile lile ulilomsababishia 'raia wako' kuingia mapema! Nadhani suala hapa ni kuwa jee, wewe ni Mwislamu (by extension unaamini haya) au la?
  Siwezi kumsemea Mkapa, kwani sijui adhabu ya hilo katika imani yake. Lakini kwa ujumla imani zote (na wala si dini pekee) zinachukulia kumwua mtu bila kosa ni hatia kubwa sana. Na kwa sababu hiyo ndiyo maana bado binadamu wako duniani na hawakufikia mwisho wa kutoweka kama vile ndege yule wa Madagascar, Dodo, au mbwa mwitu wa Tasmania na Chui wa Bahari ya Caspian! Tazama: extinct animals - Google Search
   
Loading...