Mauaji mkoani Simiyu yamng’oa Kamanda wa Polisi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,571
2,000
MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, amemuondoa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Deusdedit Nsimeki kwa kushindwa kudhibiti matukio ya uhalifu likiwamo wimbi la mauaji ya watoto, mkoani humo hivi karibuni.

Uamuzi huo aliutangaza juzi jioni alipozungumza na wananchi mjini Lamadi Wilaya ya Busega.

Alisema amechukua uamuzi huo baada ya kamanda huyo kulalamikiwa na wananchi kushindwa kudhibiti hali hiyo.

Alisema pamoja na hali hiyo ni lazima kila aliyepewa jukumu ndani ya Jeshi la Polisi atimize wajibu wake ikiwamo kulinda raia na mali zao.

“Kutokana na matukio hayo tayari nimemwondoa aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Mkoa, Deusdedit Nsimeki na kumleta mwingine (hakumtaja jina),” alisema IGP Sirro.

Alisema mbali na wananchi kumlalamikia kamanda huyo wa polisi, bado alionekana kushindwa kukomesha matukio hayo, kazi ambayo alitakiwa kuifanya.

“Mbali na nyie kumlalamikia RPC hata alipokuja kwangu nilimuuliza swali moja, wewe nilikuteua kwenda huko kunisaidia kukomesha uhalifu, sasa kwa nini bado matukio yanaendelea? Na mimi nikaona kazi imemshinda,” alisema.

Pamoja na kuchukua uamuzi huo aliwataka wananchi kutowalalamikia askari wanaposhindwa kutekeleza majukumu yao badala yake wawataje baadhi ya askari wahusika na si jeshi lote.

Hadi sasa imeripotiwa watoto watatu na wanawake wawili wameuawa na kunyofolewa baadhi ya viungo vyao tangu Oktoba 10 mwaka jana hadi mwaka huu.

Matukio hayo yanahusishwa na imani za ushirikina na mpaka sasa watu 12 wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kuhusika katika matukio hayo.

Kabla ya kuzungumza na wananchi hao alifanya kikao cha ndani cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kilichodumu kwa saa mbili.

Sirro alisema tayari ameongeza nguvu kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi kuweza kushughulikia matukio ya mauaji Lamadi.

Aliahidi kukomesha mtandao mzima wa wahalifu.

“Kuna watu bado wanaamini kupata samaki wengi mpaka watumie njia za ushirikina, mimi bado naikumbuka Lamadi hii tabia ilikiwapo zamani na wahusika wakuu walikuwa wazazi wa watoto.

“Sasa nimeagiza, watafutwe hata hao ambao walihusika katika matukio kama haya huko zamani, tuone kesi zao zilienda vipi na tujue wapi tunaanzia, lakini elimu inahitajika zaidi kwa wananchi,” alisema IGP Sirro.

Alisema ndani ya siku 10 atahakikisha wahusika wote wanapatikana na kuchukuliwa hatua za sheria.

- Mtanzania
 

MUSONI

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
833
1,000
CONGRATS KAMANDA SIRRO kazi nzuri sana ….sio mauaji ya watoto hao tu na WACHINA HAPO WAMEMUUA ENGINNER NA KUNA DALILI ZOTE AMESIMAMIA NA KUONYESHA KUWA KAJINYONGA na suspect number one driver wa marehemu akamtoa sero..jumla …..naomba na hilo la kifo cha ENGINER KABEZI LIFUATILIWE NA HAKI ITENDEKE SASA KWA MAANA KIGINGI KIMENGOLEWA....IGP ANAJUA LIPO OFISINI KWAKE.....
 

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
5,266
2,000
Tatizo La Imani Za Kishirikina Ni La Jamii Yenyewe Kuamini Kuwa Mambo Yao Mengi Hufanikiwa Kwa Kuamini Uganga, Ulozi, Uchawi Na Ushirikina. Cha Kufanya Ni Kupiga Marufuku Shughuli Zote Za Uganga Nchi Nzima, Asionekane Mwananchi Anaenda Kuaguliwa Au Kutafuta Mafanikieo Kwa Waganga. Waganga Wamelelewa Sana Kwa Muda Mrefu Kama Sehemu Ya Utamaduni. Ifike Muda Utamaduni Huu Upigwe Marufuku Kwa Nguvu Zote
 

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
6,438
2,000
Bado sijaona mantiki ya kumwondoa kazini, yaani yeye ndiyo aliye takiwa aingie site mwenyewe kupambana na hao wauwaji au vipi?

Basi askari wa vikosi vyote vya simiyu waachishwe kazi
 

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
5,266
2,000
Serikali isisite kukomesha imani zinazohatarisha maisha ya jamii, hiyo si haki ya kuabudu. Ni kufuta shughuli zote za waganga, wakatafute shughuli zingine za kujipatia kipato. Huu si utamaduni mzuri, kwanza umejaa ulaghai na utapeli mwingi kwa wenye shida mbalimbali. Safisha nchi kwa imani hatari. Jamii ielimishwe namna ya kujiletea maendeleo kisayansi na teknolojia
 

MUSONI

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
833
1,000
Bado sijaona mantiki ya kumwondoa kazini, yaani yeye ndiyo aliye takiwa aingie site mwenyewe kupambana na hao wauwaji au vipi?

Basi askari wa vikosi vyote vya simiyu waachishwe kazi
ANAYO MENGI HUYU DESDERITI WACHA VIONGOZI WENYE MAONO WATENDE KAZI YA BWANA....CONGRATS KAMANDA SAIMON SIRRO - IGP ANAYEJIELEWA....hilo la mauaji na mengineyo….wananchi waishio naye wamethibitisha itakuwa mie na wewe...
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
26,778
2,000
Hakuna kitu, Siro sema huyu si "mwenzenu".... mbona waliompiga Lisu hujawapata na Kamanda wa polisi dodoma au wewe hujajiuzulu? Mangapi maovu yanatendeka na polisi hawawajibishwi, sema huyu "si mwenzenu"
 

Getstart

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
6,666
2,000
Sikilizeni vilio na malalamiko ya watu. Watu wanateswa na kuuawa wakiwa vituo vya polisi. Utendaji wenu wa haki utaliinua taifa.
 

Kunde Ekeke

JF-Expert Member
Feb 5, 2018
6,643
2,000
Kashindwa kufanya kazi kwa ufanisi IGP amteue atakaye leta ufanisi alafu Shinyanga na Simiyu ziwe kanda maalum vikongwe wanauliwa sana
 

MLUGURU

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
1,988
2,000
Bado sijaona mantiki ya kumwondoa kazini, yaani yeye ndiyo aliye takiwa aingie site mwenyewe kupambana na hao wauwaji au vipi?

Basi askari wa vikosi vyote vya simiyu waachishwe kazi
ni dhana ya uwajibikaji Mkuu...alikuwa anapataje usingizi yeye na familia take ikiwa watoto Wa njombe huko hawana uhakika Wa maisha yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
7,361
2,000
Tatizo La Imani Za Kishirikina Ni La Jamii Yenyewe Kuamini Kuwa Mambo Yao Mengi Hufanikiwa Kwa Kuamini Uganga, Ulozi, Uchawi Na Ushirikina. Cha Kufanya Ni Kupiga Marufuku Shughuli Zote Za Uganga Nchi Nzima, Asionekane Mwananchi Anaenda Kuaguliwa Au Kutafuta Mafanikieo Kwa Waganga. Waganga Wamelelewa Sana Kwa Muda Mrefu Kama Sehemu Ya Utamaduni. Ifike Muda Utamaduni Huu Upigwe Marufuku Kwa Nguvu Zote
Wanasiasa hawawezi kipiga marufuku waganga wa kienyeji unajua kwanini?.....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom