Matusi baada ya kumfungulia mpenzi wake facebook

Matusi baada ya kumfungulia mpenzi wake facebook

KEBULA

Member
Joined
Jan 30, 2014
Posts
17
Reaction score
3
Siku mbili zilizopita mtaani kwetu hasa katika sehemu ninayoishi yaani nilipopanga niliombwa msaada wa kufungua facebook account, dada kanifuata na kuniaambia tafadhali naomba unifungulie facebook account kwani mimi sifahamu!

Sikua na kipingamizi nikaifungua lakini katka harakati nilijikuta ninaingiza email yangu ili kuhakiki.

MAJANGA;

Baada ya siku mbili hizo yaani leo hii ya alhamis nikapokea ujumbe wa kashfa na matusi kutoka kwa bwana wa dada yule jamaa akidai, kwa nini nimechukua jukumu la kumfungulia demu wake facebook?

Katika kujitetea jamaa alizidi kuporomosha matusi juu yangu akizidi kusisitiza hakutaka demu wake awe na facebook hivyo kwa nini sikumuuliza kabla? nilijaribu kumuelewesha lakini wapi ilihali mimi simfahamu na wala sijui kama huyo dada alikatazwa kuwa na facebook.

Je kosa la nani?

Nisaidien mawazo.
 
we unahangaika na mtu asiyejitambua,umeshamjibu,basi endelea na mambo yako,atachoka mwenyewe
 
Siku mbili zilizopita mtaani kwetu hasa katika sehemu ninayoishi yaani nilipopanga niliombwa msaada wa kufungua fb account, dada kanifuata na kuniaambia tafadha naomba unifungulie facebook account kwani mimi sifahamu!, sikua na kipingamizi nikaifungua lakini katka harakati nilijikuta ninaingiza email yangu ili kuhakiki.
MAJANGA; Baada ya siku mbili hizo yaani leo hii ya alhamis nikapokea ujumbe wa kasfa na matusi kutoka kwa bwana wa dada yule jamaa akidai, kwa nini nimechukua jukumu la kumfungulia demu wake facebook? katika kujitetea jamaa alizid kuporomosha matusi juu yangu akizidi kusisitiza hakutaka demu wake awe na fb hivyo kwa nini sikumuuliza kabla? nilijaribu kumuelewesha lakin wapi ilihali mimi simfaham na wala sijui kama huyo dada alikatazwa kuwa na fb. Je kosa la nani? nisaidien mawazo.
Kumbe anakaa na demu asiyemwamini halafu anakulaumu wewe.Huo ni ushetwani wa kwanza!!pili kama ana utata na fb inabidi amnyanganye na sim.Kwa ujumla hamna mapenzi hapo huyo jamaa ni mkoloni na mnyanyasa tecnolojia na jinsia.
 
majangaaaaaa majangaaaa mbona majanga mbona majangaaa. majanga mbonambona majanga mbonambona majanga mbona majanga. kuomba aombe yeye account nimfungulie matusi nipewe mieee. honey wake simjui wala yeye hanijui jeuri afanye yeyee, demu atongoze yeye acount nimfungulie hasara nipate mieee. majangaaa majangaa mbona majangaaa mbona majangaaa
 
Amnunulie huawei
Kumbe anakaa na demu asiyemwamini halafu anakulaumu wewe.Huo ni ushetwani wa kwanza!!pili kama ana utata na fb inabidi amnyanganye na sim.Kwa ujumla hamna mapenzi hapo huyo jamaa ni mkoloni na mnyanyasa tecnolojia na jinsia.
 
fb kweli ina mambo anachoogopa nini demu wake akiwa fb? huyo mpotezee tu
 
Ukiona hivyo huyo jamaa anatumia fb kwa kumsaliti mwenzie, anafikiri au siri zitagundulika wakiwa friends on fb, au huwa anafanya ndivyo sivyo.
 
ulimwengu huu unamkataza mtu mzima kujiunga facebook?

twita si utaandamana

IG nako si utamuufoo saro mtu?

na jamiiforums ndo kabisaaa urafiki unakufa...
 
Kosa kubwa ulilofanya ni kumfungulia demu wa mwenzako facebook wakati ana bwana wake angeweza kufanya hivyo. Ukitafakari zana unaweza tuhumiwa mambo mengi, hayo matusi we yavumilie angekuwa mwanaume mwingine angekuchapa makofi ya haja.

Pole.
 
Back
Top Bottom