Matumizi ya watanzania kwenye Simu

Mtumiabusara

JF-Expert Member
Nov 18, 2009
473
40
Kwa mujibu wa taarifa ya TCRA, kwa kipindi cha miezi 3 (July - September 2010) Watanzania walitumia kiasi cha shilingi bilioni 555 kwa kupiga simu na kutuma msg.

Matumizi hayo yalikuwa ni makubwa kuliko mapato ya Serikali kwa mwezi. Kwa mtazamo wangu mahitaji ya simu kwa maisha ya kawaida ni makubwa, lakini haya makampuni ya simu bado yanatuchaji bei kubwa, hivyo ni vizuri sasa bei za simu zikapunguzwa ili kukabili huu ukali wa maisha au wadau mnasemaje?

Source
Daily Nation:*- Business News*|Tanzanians spent $396m on voice, text messages: report
 
Cha msingi hapa ni kiasi gani cha mapato serikali inakusanya kama kodi ili kuboresha maisha ya wananchi wa Tanzania
 
Wakuu,
Kuna anaejua ni kiasi gani cha kodi makampuni haya ya simu yamelipa kutokana na matumizi yetu watanzania?
 
Hata hivyo sijui hawa TCRA huwa wanaletewa hizi data na makampuni ya simu au wana direct access kwenye database yao. Maana kama wanasubiri kuletewa taarifa, basi itakuwa imeshachakachuliwa ili kukwepa kodi kidogo
 
Back
Top Bottom