Kwanza mimi kwa ufupi huwa wananitia hasira sana.
Kwa wenzetu, uchambuzi wa mpira unafanywa na wakongwe ambao wamecheza ligi mbalimbali kwa mafanikio na kwa viwango vya juu kabisa.
Chukulia mf kama Sammy Kuffor, Ryan Giggs, Michael Owen,..........! Hawa watu wakichambua soka wanatoa uzoefu wao kutoka uwanjani na kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. Hawa ni wachezaji wastaafu. Hii pia ni pamoja na watangazaji wa soka kwenye TV na Radio, ni wazee wenye uzoefu wao!
Njoo kwetu sasa. Utakuta mtangazaji wa Radio au TV ana miaka 24, 25, 26! Kwa umri huo inawezekana hata Lunyamila, Nteze John, Chumila, Mohamed Hussein (machinga) amesimuliwa tu uwezo na uchezaji wao achilia mbali kina Sunday Manara.
Ukija kwa wachambuzi wa soka ktk Radio na TV za Tanzania, mtu pekee ninayemfahamu na kumuona akicheza mpira kwa kiwango cha juu ni Ally Mayay Tembele (naweza kusahihishwa).
Kwa hiyo kwa hali hii siyo ajabu kukutana na msemo maarufu 'kupata matokeo'! Labda wachangiaji tumesahau pia jinsi watangazaji wanavyochanganya lugha wakati wa kutangaza. Utasikia goli likifungwa, 'yeesssss, he has made it', 'ame switch kutoka flank ya kushoto kwenda kulia', 'amepiga square pass' na mbwembwe zingine nyingi tu! Sisi wa Tz akili zetu tunazijua sisi na zinatufaa wenyewe tu!