Kwa mawazo yangu sidhani kama kuna tatizo kuwekeana kila kitu wazi. Kwanini uweke pin code? Hii inaashiria kuwa wewe bado hujaweka makazi yako pale, bali umetia kambi tu ambayo huenda ikahamishwa muda wowote. Kuhusu massage zinazoingia, hupaswi kuyafanyia maamuzi, bali ukiziona, just take note to the number na usubiri jinsi mwenzio atakavyojibu ile message akiwa mbali nawe. Hiyo ndiyo itakayokupa picha halisi.
Mimi kwa mfano nikiwa na kazi nafanya na mke wangu yupo karibu, nampatia anishikie hata kwa masaa sita, ikiita naweza kumwaagiza aniletee nipate kuongea, message ikiingia na labda kuna kitu nimeshikilia naweza kumwomba aifungue hiyo message na kuniwekea nisome! Sina wasiwasi kabisa. Na kama kuna uwezakano wa kupata software ya kumonitor simu ya mwenzio, basi sioni wasiwasi hata yeye akiipata kwa ajili yangu.
Kama mwenzio anakucheat utamjua tu, hasa ukiwa mtaratibu na kufuatilia mambo kama vile;
1. Muda anayofanya mawasiliano mengi, mf. akiwa njiani kwenda kazini au akirudi nyumbani au usiku wa manane. Mara nyingi mawasiliano haya si mema kabisa. Utatakiwa kuwa makini.
2. Je, anaowasiliana nao mara kwa mara unawafahamu? Wana mahusiano ya undugu na mwenzio? Anaweza akatambulisha kama rafiki yake wa kawaida, lakini mawasiliano huwa na mipaka. Kama ni ndugu, je na wengine wanamfahamu kama mwenzio anavyodai?
3. Je, Message anazopokea zinajibiwa? Au ukiiangalia inbox yake unakutana na message zako tu? Ni lazima message nyingi zijibiwe, na majibu pia zionekane, na haiwezekani akawa na message zako tu.
4. Anabadili tabia yake ya uvaaji, mafuta ya kupaka, style ya maisha? Kama ndivyo, basi huenda anafanya hivyo kwa ajili ya someone arround.
5. Anaowasiliana nao wanakuwa huru kumpigia hata wewe ukiwepo? Kama sio, basi ni dhahiri kuwa kuna kitu, na unatakiwa kujiuliza nani anampatia taarifa kuwa you are arround?
Lakini unapohisi hivi, hupaswi kufanya maamuzi haraka au kuonesha kwa mwenzio kuwa una hisia fulani, bali ufanye uchunguzi wa kina hadi pale utakapojitosheleza kuwa ukimbana hatoki, bali kwa huruma na msamaha wako tu.
______________________________________________________________
Normally, a true love has no reasons, but it is associated with unlimited and unconditional forgiveness.