Matumizi ya "L" na "R" kwenye kiswahili

Ha haaa chizi wewe
Hahahaha kumbe dada una sense of humour ;)
Anyway hiri ri rugha ratubabaisha sana sisi wa Shinyanga, ira naamini rinasambaa huku kijijini, muda si mlefu utasikia kira ngosha yupo swafii kabisa...:)
 
Imefika wakati basi Baraza la Kiswahili lihalalishe tutumie "R" panapokuwa "L" na vice versa...
Maana watu tunashindwa kabisa kutumia hizi Letters panapotakiwa, mfano..
  • Karo = Kalo
  • Kura = Kula
  • Laini = Raini
  • Limbwata = Rimbwata
  • Mara = Mala
  • Leo = Reo
  • Rekebisha = Lekebisha
  • Vurumisha = Vulumisha
  • Mchele = Mchere
  • Analia = Anaria
  • Elfu = Erfu
  • Thelathini = Therathini..
  • ,,,
  • ###
  • ....
Tuongezee..
Si muda mrefu nami nafikiri ntatumbukia kwenye hili janga...:mad::(
Kumbe mleta mada umetoka MARA ngoja wenzio waje ?

brain is the beautiful part of the body.
 
Solution.
L ni konsonanti ambayo hutamkiwa pembeni mwa ulimi hii tunaita KITAMBAZA
R ni konsonati inayo tamkwa Kwa kupigapiga ulimi hii tunaita KIMADENDE

By muhadhili..

acha uongo
 
Inaudhi sana, mtu siku zote anasikia na kuona Rais wetu anaitwa Magufuli lakini utakuta yeye anaandika "Magufuri".

Halafu na yale ma "ga" wanayoongezea, yanakera sana.

Nahisi kama kuna usaliti wa lugha unafanyika kwa makusudi kabisa.
Ni "RAISI" sio "RAIS"
 
Solution.
L ni konsonanti ambayo hutamkiwa pembeni mwa ulimi hii tunaita KITAMBAZA
R ni konsonati inayo tamkwa Kwa kupigapiga ulimi hii tunaita KIMADENDE

By muhadhili..

acha uongo
Acha fix bwana mdogo. Usilete mbwembwe kwenye FONOLOJIA kama huijui. Hahahahah eti L inatamkiwa pembeni ya ulimi, hatuna konsonati ya
aina hiyo.
Pia sio "MUHADHILI" ni "MHADHIRI"
 
Kweli ndugu yangu uko sahihi utata katika lugha yetu umekithiri utasikia mtu anasema .... NIMEENDA NIMEMKUTA HAYUPO..
 
  • Stalehe (Starehe)
  • mlema (Mrema)
  • mala (mara)
  • Luge (Ruge)
  • Lahisisha
  • Lahisi (Rahisi)
  • Lekebisha (Rekebisha)
  • Laha (raha)
  • Lembuwa (Rembuwa)
  • Ramadhani (Lamadhani)
  • Lashidi (Rashidi)
  • Durra (Dulla)
  • Telemka (Teremka)
  • Sirro (Sillo)
  • Sheria (Shelia)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom