Daby
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 33,894
- 76,805
Naomba tujadili juu ya hili kosa la kifonolojia ambalo watumiaji wa kiswahili wamekuwa wakilitenda panapo au pasipo kulijua na namna ya kuliepuka. Nitaeleza halafu kisha nguli wa hii lugha wataongezea.
Kwanza Sauti r na l ni zipi: hizi ni sauti ghuna ambazo hutamkwa panapokuwa na mrindimo wa nyuzi sauti wakati wa utamkaji. Yaani wakati mtu anapotamka hewa hutikisa nyuzi za sauti na hivyo kufanya kuwe na mrindimo katika ala za utamkaji. Kosa hili la kimatamshi la sauti r na l hutendwa saana na watumiaji ambao lugha yao mama haina sauti Aidha r au l mfano wasukuma na wakurya.
Nini kinapelekea kosa hili kutokea :
Athari ya lugha mama : kama lugha mama ya mtumiaji wa kiswahili haina sauti r au l uwezekano wa kufanya kosa hili ni mkubwa saana kwasababu ujifunzaji wa lugha ya kwanza hutegemea sana sayansi iliyopo kichwani ya lugha mama. Mifano nimetoa hapo juu.
Ufanano wa mahali pa matamshi : sauti r na l zote hutamkiwa kwenye ufizi...ulimi unapogusa ufizi. Licha ya r hutamkwa kwa kupigwapigwa na kukwaruzwa kwa ufizi wakati l hutamkwa kwa kukutanisha ncha ya ulimi na ufizi. Jaribu kutamka utaona.
Namna ya kuondokana na kosa hili la kimatamshi:
Mtumiaji wa lugha anapaswa Kuelewa hizi ni sauti mbili tofauti.
Pia anapaswa kuelewa utamkaji wake na mahali pa matamshi. r hutamkwa kwa kupigwapigwa na kukwaruzwa kwa ufizi. l hutamkwa kwa kukutanisha ncha ya ulimi na ufizi. Nimeleta hili hapa maana ukichungunza unaona matumizi ya r kwenye l na kinyume chake yamesharasimishwa na hadi kwenye machapisho na vyombo vya habati haya makosa yapo.