Matumizi ya Kiswahili: EAC igeni mfano wa AU, Magufuli kaonesha Njia

Lakasa chika7

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
454
1,264
Licha ya Kiswahili kuwa lugha inayotumika na Nchi zaidi ya tano ukanda wa afrika mashariki lakini bado Kiswahili hakijawepa Hadhi ya juu km English. Lugha rasmi ya Jumuiya ya afrika mashariki ni English. Licha ya kiswahili kufahamika sana na Watanzania, wakenya, warwanda, waburundi pamoja na kidogo waganda bado Kiswahili kinaitwa ni lingua franca. Wanajeshi na askari polisi wa Uganda wanajua sana Kiswahili.

Haya ni matusi kwa wanajumuiya ya afrika mashariki. Kwanini kiswahili kisiwe lugha Rasmi Haiwezekani Kiswahili kisitumike kwenye vikao vya Jumuiya. Haiwezakani Kiswahili kiishie kuwa lingua franca tu. Tunatakiwa tuvalue vya kwetu.

Upande wa AU Kiswahili moja wapo ya lugha rasmi ikiwa samba samba na English na kifaransa. Ni jambo la kupongeza kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika na Rais wa JMT kutumia Kiswahili katika Mkutano wa AU. Ni jambo linalopaswa kupongezwa na watanzania kwakuwa kuongea Kiswahili ni kukivalue sana na kukiuza Kiswahili chetu. Kama ingekuwa Kiswahili kiameanzia Kenya, nakwambia leo lugha ingekuwa kubwa sana barani Afrika.

Ni jambo la kupongezwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika mashariki kwa kutumiwa Kiswahili katika forum kubwa ya Afrika.

Kiswahili ni kikubwa sana. Wakenya wanafaidika sana na Kiswahili ambacho siye tunakidharau. IPO Kamisheni ya Kiswahili ya afrika mashariki ipo Zanzibar katibu mtendaji wake ni Mkenya. Sitoshangaa hata wahariri/editors km wakiajiariwa watakuwa Wakenya. Vyuo vikuu duniani wakenya wengi wameajiriwa kufundisha Kiswahili.. Hata kuna baadhi ya court za China, honkong wameajiriwa wakenya kufanya kazi za kutafsiri Kiswahili.

Hongera tena sana kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Rais wa JMT kwa kuki value Kiswahili katika forum kubwa Afrika.
Na vyema pia lugha ya Kiswahili iweze kutumika katika vikao vya afrika mashariki.

Watanzania tupende na tuvitukuze vya kwetu lakini pia tuvijue na vya wengine(English) pia.


Update baada ya reply za watu.

Great thinker tunajadili nn sijui humu..kwann tuna attack personality. Kwa AU Kiswahili ni official language km English lakin tunaponda Mkubwa wetu kutumia kiswahili.

Soma pia hizi

Attack za CCM Mtandao vs. CHADEMA Mtandao

Mjue mshauri wa Rais Magufuli anayedumaza uchumi
 
Kenya,Rwanda na Burundi wanajitahidi sana kuongea kiswahili,Uganda bado saana
 
Kwan hiyo ilimfanya mkuu wetu akashindwa kuhutubia. Na fatilia YouTube vizuri.

Mkuu mleta post hata mimi naunga mkono sana kukuza lugha ya kiswahili. Ni ukweli mchungu mkuu wetu kwenye lugha ya kiingereza hayuko vizuri kwenye kukiongea. Kwa sababu ya mapungufu hayo ndio inabidi ionekane ana uzelendo kwa kuongea kiswahili. Ila kesho au keshokutwa akitoka madarakani akaingia anayeweza kuongea vizuri kiingereza ataendeleza kukitumia. Kama kweli kuna nia ya dhati basi iwe ni sera ya taifa kutumia kiswahili kwa kila jambo, na sio kuchorana kwa kujifanya kuongea kiswahili mtu mmoja ambaye watu tuna mashaka na uwezo wake katika lugha hiyo, huku viongozi wote wa serekali wakiona fahari kupeleka watoto wao shule zinazofundisha kwa kiingereza na wanaoweza kupata ajira hasa huko serekali ni wale wanaojua kiingereza vizuri.

Umesema wakenya sijui wanafundisha na kutangaza kwenye mashirika ya nje kwa kiswahili. Ukweli ni kuwa wakenya wako vizuri kwenye kiingereza na habari nyingi wanazipata kwa kiingereza na kisha kuzitafsiri kwa kiswahili kisha kuzisoma. Hata hao waalimu wanaofundisha kiswahili huko nje wana msingi mzuri wa kiingereza kisha wanakuwa waalimu wazuri wa kiswahili, kwani ni rahisi kuwasaidia na kuwapata wanafunzi vizuri wanaotumia kiingereza tu. Hili la kujifanya eti kiingereza ni uzalendo ni usanii wa mchana kweupe, wakati ni mtu mmoja tu anayekitumia tena kwa madhaifu yake binafsi.
 
Kenya,Rwanda na Burundi wanajitahidi sana kuongea kiswahili,Uganda bado saana

Wanajitahidi, lakini sio lugha yao ya kwanza. Dunia hii ni kiingereza/kifaransa/kijerumani/Spanish kama lugha za kwanza. Hizi nyingine zinafuata baadae. Ni utani usiomithilika viongozi wote kupeleka watoto wao shule zinazofundisha kwa kiingereza kisha kujifanya wanakienzi kiswahili. Ukienda maofisini ili uweze kupata kazi nzuri ama inayohitaji ujuzi barua na cv yako unapeleka kwa kiingereza, halafu leo mtu anatuletea maigizo ya kiswahili. Huu udhaifu uko wazi na wala hauna mahusiano yoyote na uzalendo.
 
..kiswahili hakipaswi kutumika zaidi ya kinavyotumika sasa hivi.

..waTz tuna udhaifu mkubwa sana ktk matumizi ya lugha ya KIINGEREZA.Tujitahidi kupambana na udhaifu huo.

..pia hatupaswi kuzitupa mkono lugha zetu za makabila.

..Utafiti wa kitaalamu unaonyesha kwamba mtoto anayezungumza lugha zaidi ya moja huwa
mwepesi kujifunza mambo mapya ukubwani.

..kwa hiyo kwa maoni yangu, waTz tunapaswa kuzungumza kwa ufasaha at least lugha tatu, lugha ya kabila, kiswahili, na kiingereza.
 
Angekuwa ameongea Kiswahili na wakati huohuo yai linapanda ningesema ni uzalendo. Ila kwa vile ameongea kiswahili ili kuficha udhaifu wa kutojua kiingreza, hoja ya uzalendo haina mashiko. RAS Simba arudishe hela ya watanzania
 
Angekuwa ameongea Kiswahili na wakati huohuo yai linapanda ningesema ni uzalendo. Ila kwa vile ameongea kiswahili ili kuficha udhaifu wa kutojua kiingreza, hoja ya uzalendo haina mashiko. RAS Simba arudishe hela ya watanzania

Wewe umezungumza ukweli hata kama unauma.
 
Back
Top Bottom