Kama kuna watu wana nafasi kubwa sana ya kufikisha ujumbe kwa wananchi wao kwa gharama ndogo sana basi ni waheshimiwa wabunge wa CDM walioaminiwa na wananchi mwaka 2010 na kupewa majimbo/majiji makubwa hapa nchini. Kwa jinsi sayansi na teknolojia ya ICT ilivyokua kuanzia 2010 hadi sasa, Wabunge na wananchi wanaoishi mijini wanapata taarifa za kila tukio duniani pale tu linapotokea. Mfano Mhe mbunge wa Arusha au Mbeya sijui kama wana blog ambazo zinaripoti matukio kwa wananchi wao hasa huu mchakato wa KATIBA MPYA, fursa pekee iloyobaki ya kujiimarisha kisiasa. Nampongeza Mbunge wa Iringa kwa jinsi anvyotumia fursa ya ICT kuwasiliana na vijana wake. Nadhani akina Mhe. Lissu wangeiga na kufanya vema zaidi japo natambua kwamba wananchi wengi bado hawaja na access ya smart phones au komputa. Kwa kuwa habari ni haki ya kikatiba, ni vema wabunge wakajinganisha na wananchi wao kiurahisi ili wajue mambo mema wanayoyafanya. Information is power......................nakaribisha maoni ya kujenga...