Matumizi ya airplane mode

Matumizi ya airplane mode

Jitu la kienyeji

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,445
Reaction score
7,987
AIRPLANE MODE Ni mfumo uliopo katika simu zetu janja(Smartphone)laptop na iPad.

Aiplane mode huwakilishwa na alama ya ndege inayopaa, mfumo huu unapokuwa umewashwa kwenye kifaa chako Cha mawasiliano, huzima mifumo yote ya kiredio Kama Bluetooth, WiFi pamoja na mitandao ya simu.

Ukiwasha Airplane mode hutoweza kupata huduma za mitandao ya simu (kupiga na kupokea simu)Bluetooth na WiFi. Huduma hii iliwekwa kwa watu walio katika Safari ya ndege kutumia simu zao kwa huduma nyingine bila kulazimika kuzima kabisa simu zao,hii ina maana abiria atatumia huduma Kama kupiga picha,kusikiliza mziki isipokuwa kufanya mawasiliano ya simu,kushare kwa Bluetooth na WiFi na huduma ya GPS.

Teknolojia hii imerahisisha watu wenye vifaa vya elektroniki kuvitumia ndani ya ndege huku wakihakikisha vifaa hivyo vimewekwa kwenye Airplane mode,inasemekana muda wote simu zinatuma signal kutafuta mnara wa mawasiliano na Kama ndege yenye abiria wengi ndani yake na wote wakiacha simu zao bila kuwasha Airplane mode simu zao zitakuwa zinatuma signal nyingi kutafuta mawasiliano na Hilo linaweza kuingiliana na mfumo wa mawasiliano wa ndege na kuleta tatizo kwa rubani katika ufanisi wake.

Airplane mode husaidia kuendelea kutumia kifaa chako kwa kazi nyingine bila utumiaji mwingi wa chaji, Kama utatumia huduma hii hata Kama sio kwenye ndege, itakusaidia kifaa chako kukaa na chaji kwa muda mrefu zaidi, kitendo Cha simu kutafuta signal kila wakati huigharimu simu chaji kubwa.kuna baadhi ya simu janja unaweza kutumia WiFi ukiwa ndani ya ndege.

FB_IMG_1626438908498.jpg
 
Back
Top Bottom